Hii ni kwa mafundi professional wa magari tu

Hii ni kwa mafundi professional wa magari tu

dustless

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2016
Posts
796
Reaction score
714
Habari zenu wakuu
Leo naomba kufahamishwa mambo machache kuhusu gari za automatic

Oil ya gia box inapaswa kumwagwa kila baada ya km ngapi?

Je ni kwel engine oil inatofautiana, yaani zipo za kumwaga kila baada ya 3000km na zingine 5000km. Kama ni hivyo kuna sehem zimeandikwa kiwango cha km katika oil husika au ni uzoefu wa mafundi tu unafuatwa.

Ukifunga mziki mkubwa unaua battery ya gari?

Gari ikiwa silence inakula mafuta kama kawaida ama hakuna

Ni muda wa kuiacha gari silence pindi unapoiwasha asubuhi.

Mtu anaweza kutempa na mileage za gari hiz kirahis?

Ni vizuri kuwa na utamaduni wa kuosha engine mara kwa mara. Na kama ndio hao wa car wash wanapaswa kuliwasha gari au hata likiwa limezimwa? Na ni mara ngapi baada ya muda gani?

Mtu anaweza kufanya uhuni kubadil usajili wa gari, say, kutoka namba B kwenda D ili lionekane jipya na auze kwa bei kubwa.

Ni mileage ngapi ukitembea kwa gari zenye 1500cc ujue gari imechoka uanze kujipanga?

Je gari ikichoka unaweza badili engine na ukaendelea kufurahia maisha kama mwanzo? Au ni bora kuuza skrepa tu baada ya engine kuchoka.

La mwisho ni kwa wajanja wa mjini wazoefu wa kutembelea mak.lio, ni zipi seat cover nzuri kati ya dukani ama za kuchagua material mazuri kisha unashonewa na mafundi wa kitaa. Jibu kwa kuzingatia muonekano na uimara wake pamoja experience yako kwenye magari wajanja wengi unaowaona.

Ahsanteni sana, japo nimekuja kama mtu asiyejulikana ila naomba majibu yanayofahamika.
Kejeli, dharau na hata matusi kwangu ni ruksa maana hunijui sikujui ila naamini waungwana watanipatia majibu stahiki.

Hiz gari za kupewa na ndugu ni tabu sana, naomba nisaidien nisije pokonywa.
 
Wakuu mjitokeze basi kwa msaada, au nimechanganya jukwaa
 
Hivi hamna mafundi ambao ni wataalamu hasa humu ndani wajibu haya maswali??
 
Gari ikiwa silence inakula mafuta zaidi kuliko ikiwa ktk mwendo.
2. Ni kweli engine oil zina tofautiana na zinaandikwa maelekezo nnje ya mkebe wa kuhifadhia toka kwa mtengenezaji,mf Total,Puma nk. Kila mmoja huwa anaandika maelekezo ya uwezo fanisi wa oil yake.
3. Gari unaweza kuibadili Engine na ukaendelea kudunda bila shida endapo hali ya body nnje inakuruhusu.
4. Ukiwasha gari na kuiacha silence kama dk 3 mpaka 5 nivizuri kwakuwa mudaunapokuwa umeizima oil nyingi hurudi chini kwenye sampo hapo unaipa nafasi yakuanza kurejea ktk mzunguko wake wa kawaida ktk sehemu maalum ilizo pangwa kitaalamu.
 
Kubadili mileage ktk gari inawezekana pia kabisa na kuna baadhi ya watu walikuwa wanafanya
 
Kuhusu mileage ambazo zitakufanya uhujuwe gari imechoka.1 hiyo gari iwe imenunuliwa mpya kabisa.2upate maelekezo ya mtengenezaji. Mf kuna kampuni ya trucks hapa Dar wao wananunuwa scania mpya toka kiwandani na wanazitumia kwa km ambazo wameelekezwa na mtengenezaji,ikifikia hizo km wanaziuza kama mtumba wao wanachukua nyingine mpya.
 
Nimejaribu kujibu kwa kadiri ya uelewa wangu,nakubali kukosolewa nilipokosea
 
Gari ikiwa silence inakula mafuta zaidi kuliko ikiwa ktk mwendo.
2. Ni kweli engine oil zina tofautiana na zinaandikwa maelekezo nnje ya mkebe wa kuhifadhia toka kwa mtengenezaji,mf Total,Puma nk. Kila mmoja huwa anaandika maelekezo ya uwezo fanisi wa oil yake.
3. Gari unaweza kuibadili Engine na ukaendelea kudunda bila shida endapo hali ya body nnje inakuruhusu.
4. Ukiwasha gari na kuiacha silence kama dk 3 mpaka 5 nivizuri kwakuwa mudaunapokuwa umeizima oil nyingi hurudi chini kwenye sampo hapo unaipa nafasi yakuanza kurejea ktk mzunguko wake wa kawaida ktk sehemu maalum ilizo pangwa kitaalamu.
Asante sana mkuu
 
Back
Top Bottom