Hii ni CCM tunayoijua kweli?

Hii ni CCM tunayoijua kweli?

Joined
Jul 4, 2025
Posts
15
Reaction score
54
Polepole hajamshambulia mtu, yeye ametoa hoja kuwa mchakato wa upatikanaji wa mgombea wa CCM ulikosewa

Haukufuata katiba na taratibu za chama, lkn badala yake watu wanaomjibu wamejikita kumzungumzia mtoa hoja

Kwa Gwajima vile vile alitoa hoja kuhusu utekwaji wa watu, watu wanapotea lkn serikali inakuja na majibu mepesi, watu wakajikita kumzungumzia Gwajima badala ya hoja ya utekaji

Ni nini kipo CCM miaka hii kwamba haina watu wa hoja kwa hoja!?
Kwanini hawajibu hoja

Ipo hivi mfano umeme umekatika siku nzima akijitokeza mtu kuzungumzia ukatikaji wa umeme, jibu si ni simple tu

"Bwana ni kweli umeme ulikatika siku zima na sababu zilikuwa ni hitirafu kwenye mitambo ya uzalisha" na kisha mnaomba radhi inaisha

Badala ya kuanza kumsema mtoa hoja aliyesema kuwa umeme ulikatika
 
Back
Top Bottom