mashimbamang'oma
Member
- Feb 21, 2012
- 53
- 23
Hii ni aibu kwa taifa... Badala ya bunge kujadili hatma ya wananchi wao wabungee waccm wanaonyesha upuuzi wao hadharan kwa kumzawadia hela mpuuzi mwenzao mwigulu nchemba.. Hivi kweli tumefikia hapa? Mtu badala ya kuchangia hoja katika bajeti anatoa mipasho alafu mwisho wa siku tunamchangia hela kama hadija kopa,offside trick na mzee yusufu tunavyowachangia wakiwa wanatumbuiza ukumbini? Hii ni aibu sana kwa taifa.... Embu tukumbuke tulipotoka... Walikuwa wazee wa kupiga makofi na ndiooo kwa kila jambo linaloletwa bungeni, wakawa wazee wa kuzomea watu wanapofanya maamuzi yenye tija kwa taifa... Ila mkutano wa mwezi wa nne wa bunge waliamka wakawa watu wa kutoa hoja.. Hapo ndipo walipozaliwa kina deo flikunjombe na saini 70 za kutokuwa na iman na waziri mkuu... Ila baada ya kupewa semina na chama chao wameamua kuwa watu wa mipasho na maigizo bungeni... Mpaka kutuzana bungeni... Kweli watanzania hawa ndio viongozi tunao waitaji?