Hii ngumu kumeza

Hii ngumu kumeza

Status
Not open for further replies.

MNEKI

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
992
Reaction score
1,310
Ni miezi kama miwili imepita tangu nimalize chuo na kurudi nyumbani.....lakini hata hivyo nilikuwa narudi kipindi cha likizo kuonana na familia.

Kwanza niseme tu wazi,,,sina desturi ya kukagua simu ya mkewangu lakini baada ya kumtilia mashaka ilibidi nifanye hivyo.

Nikweli nilichokikuta inbox ya Facebook ni hiyo conversation kati ya wife(chati ya bluu)

na jamaa ambae namjua na ni mfanyakazi mwenzangu pia na nlikuwa namheshim sana.
Hiyo conversation inaonesha watu hawa ni wapenzi wala haihitaji nguvu ya ziada kugundua hilo.

Wadau hii kitu nilikuwa nasikia tu kwa watu kumbe ni kweli aisee inauma sana usiombe yakukute....

Imagine mtu tuko nae over ten years sasa pamoja na watoto wawili Leo hii ananifanyia hichi kitu..

Afadhali hata ningekuwa na tabia ya kuchepuka nisingeumia sana.....ningejisemea tu moyoni kwamba malipo ni hapahapa duniani , muosha huoshwa.

Lakini kinachoniuma Mimi nimekuwa mwaminifu tangu nilipomuoa sijawahi msaliti hata Siku moja.

Wakuu embu nisaidieni experience kwa wale mliopata maswahibu kama haya au hata kama hayajakupata nishauri tu kabla sijaharibu Niko na hasira sio ya kawaida ingawa sijionyeshi kwake.....View attachment 897325
 
Last edited:
Mwanaume ni kiumbe wa kwanza kuongea na Mungu na mwanamke ni kiumbe wa kwanza kuongea na shetani pale mitaa ya bustani ya Edeni, kwa hiyo Mkuu onyesha busara ikiwezekana muulize wife kuhusu hii kitu akikaza fuvu waone wazee wake na itakuwa rahisi maana una ushahidi wote.
pole sana Mkuu
"NO WOMAN NO CRY"
 
Mkuu muache huyo mwanamke, kuna mengi sana ya kufanya inatakiwa ujikite ili uyakamilishe hakuna haja ya kukumbatia vitu vinavyoumiza moyo, hata maandiko yameruhusu kumuacha mke ambaye ni mzinzi (ukimfumania kwa uzinzi), ukiendekeza utakuja lia sana na kuumia moyo sana. Huo ni mtazamo wangu, yaani mimi mke wangu achepuke lakini nisijue hapo sawa ila nikija kujua namuacha hapo hapo asije akanimaliza. But all in all Mke anauma sana mkuu.
 
Mkuu muache huyo mwanamke, kuna mengi sana ya kufanya inatakiwa ujikite ili uyakamilishe hakuna haja ya kukumbatia vitu vinavyoumiza moyo, hata maandiko yameruhusu kumuacha mke ambaye ni mzinzi (ukimfumania kwa uzinzi), ukiendekeza utakuja lia sana na kuumia moyo sana. Huo ni mtazamo wangu, yaani mimi mke wangu achepuke lakini nisijue hapo sawa ila nikija kujua namuacha hapo hapo asije akanimaliza. But all in all Mke anauma sana mkuu.
Wewe nahisi umenielewa......inauma sana Braza!!! Inaniumaaa
 
Kaka sidhani kama atatoa jibu litakalofanya nimuelewe

Kuna uzi humu unasema usiguse simu ya mwanaume/ mwanamke kuna privacy zake.

Nilikuwa nawaza sana hizo privacy ni zipi, hatimae nimejua kwa nini hawataki washikiwe simu zao.

Nasema hivi, huyo kesha kuwa mke wa stuff mate hata ukikomaa utagongewa hadi mnazeeka nakuomba umwachie jamaa aoe.

Kwa vile ushahidi upo nenda kamkabidhishe kwao uendelee na maisha yako.

Ukiilazimisha hiyo ndoa itakugharimu maisha yako( huyo yuko radhi akuue ili aendelee na huyo jamaa, sio kwa kitendo hicho alichokifanya).
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom