Hii ndoto inamaanisha nini?

Mama Mwana

JF-Expert Member
Jun 6, 2023
1,463
4,720
Siku kama nne nyuma niliota nipo napita njia ambayo kiuhalisia naijua hiyo njia lakini sikuwahi kuipita, yaani unaiona njia inaelekea huko ila sijajua inaishia wapi nasjawah kujishughulisha kisha nikajikuta nimefikia kwenye kitongoji nimekaa kibarazani nje.

Mbele yangu kuna minazi kwa idadi ni mitatu nikishtuka kulipokucha sikuifatilia sana nikaendelea na shughuli zangu, kimbembe ni leo nimeipita hiyo njia na hiyo nyumba pia ndio nilipofikia na idadi ya minazi ipo vilevile kama nilivyoota sasa nimekuwa najiuliza hii sehemu niliiona wapi nikagundua niliota jaman inanitatiza inawezekanje na inamaanisha nini?
 
siku kama nne nyuma niliota nipo napita njia ambayo kiuhalisia naijua hiyo njia lakini sikuwah kuipita, yan unaiona njia inaelekea huko ila sjajua inaishia wapi nasjawah kujishughulisha kisha nikajikuta nimefikia kwenye kitongoji nimekaa kibarazani nje,mbele yangu kuna minazi kwa idadi ni mitatu nikshtuka kulipokucha sikuifatilia sana nokaendelea na shughuli zangu, kimbembe ni leo nimeipita hio njia na hiyo nyumba pia ndio nilipofikia na idadi ya minazi ipo vilevile kama nilivyoota sasa nimekua najiuliza hii sehem niliiona wapi nikagundua niliota jaman inanitatiza inawezekanje na inamaanisha nn?
Ulivyofika maeneo hayo, mtu wa kwanza kabisa kuonana nae alikuwa ni nani? Na unakumbuka maneno ya kwanza huyo mtu kuyatamka yalikuwa maneno gani? Na je, kati yenu nani alianza kumuongelesha mwenzake?
 
kwenye ndoto nilikua nimekaa kama ninayeshangaa hapa ni wapi na trust me mwenye nyumba hakutokea mpaka mwisho wa ndoto na uhalisia n the same, na maneno sikumbuki alikua mwanamke,
 
siku kama nne nyuma niliota nipo napita njia ambayo kiuhalisia naijua hiyo njia lakini sikuwah kuipita, yan unaiona njia inaelekea huko ila sjajua inaishia wapi nasjawah kujishughulisha kisha nikajikuta nimefikia kwenye kitongoji nimekaa kibarazani nje,mbele yangu kuna minazi kwa idadi ni mitatu nikshtuka kulipokucha sikuifatilia sana nokaendelea na shughuli zangu, kimbembe ni leo nimeipita hio njia na hiyo nyumba pia ndio nilipofikia na idadi ya minazi ipo vilevile kama nilivyoota sasa nimekua najiuliza hii sehem niliiona wapi nikagundua niliota jaman inanitatiza inawezekanje na inamaanisha nn?
NDugu yangu wewe utafika mbali sana kisiasa, hiyo njia inaashiria unatoka chini kabisa kisiasa mpaka juu kabisa, hiyo minazi mitatu ni Rais, waziri mkuu na Makamu wa rais mnajadili jambo kwa pamoja....kwa kifupi hiyo sehemu ni Ikulu....umetusua kijana.
 
Unatakiwa ujue,

Unapowaza au kupanga safari kwenda Mahali Fulani ambapo hujawahi fika,

Mtu wa Rohoni, yaani wewe, huenda huko kabla ya MWILI, na ndoto ni taarifa ya kitu halisi ulichofanya katika Ulimwengu wa Roho wa NDOTO.

Ndoto ni HALISI,

Na mtu ndiyo ndoto yenyewe, kamwe usipuuzie ndoto, ni HALISI.

Ubarikiwe.
 
Unatakiwa ujue,

Unapowaza au kupanga safari kwenda Mahali Fulani ambapo hujawahi fika,

Roho Yako huenda huko kabla ya MWILI, na ndoto ni taarifa ya kitu halisi ulichofanya katika Ulimwengu wa Roho wa NDOTO.

Ndoto ni HALISI,

Na mtu ndiyo ndoto yenyewe, kamwe usipuuzie ndoto, ni HALISI.

Ubarikiwe.
amina kwahiyo haina maana yoyote hii? sikumbuki kuwa na ndoto ya aina hii inanifikirisha mana ndoton naumiza kichwa hapa n wapi uhalisia hivyohivyo tena nikasema kabisambona kama hapa sio pageni machoni mwangu
 
Ebana eeh wiki kama moja nyuma pia niliota kitu inataka fanana na hii ila mimi niliota sehemu ambayo nilishawahi kuipita sasa ajabu ni kwamba hiyo sehemu sio route yangu ya kila siku na niliwahifika kwa mara moja tu.

Ajabu ni pale kesho yake nikiwa nimesahau kabisa si ni kajikuta nipo sehemu ile ile sasa nikawa naona kabisa hiyo sehemu nilikuepo ila sikumbuki vizuri, wakati navuta kumbukumbu nikaiona picha kamili ya vile niliota na ndio sehemu nilipo, nilistaajabu kwa muda.
 
Siku kama nne nyuma niliota nipo napita njia ambayo kiuhalisia naijua hiyo njia lakini sikuwahi kuipita, yaani unaiona njia inaelekea huko ila sijajua inaishia wapi nasjawah kujishughulisha kisha nikajikuta nimefikia kwenye kitongoji nimekaa kibarazani nje.

Mbele yangu kuna minazi kwa idadi ni mitatu nikishtuka kulipokucha sikuifatilia sana nikaendelea na shughuli zangu, kimbembe ni leo nimeipita hiyo njia na hiyo nyumba pia ndio nilipofikia na idadi ya minazi ipo vilevile kama nilivyoota sasa nimekuwa najiuliza hii sehemu niliiona wapi nikagundua niliota jaman inanitatiza inawezekanje na inamaanisha nini?
Inamaanisha soon utalamba uteuzi kama wewe ni kada
 
Ukifundishwa,

Au ukiamua, unaweza kuchunguza ya sirini Kwa kuomba kabla ya kulala Ili uende katika Roho kufahamu Siri au taarifa Fulani,

Mfano, limetokea tukio la wizi nyumbani kwako, unaweza kuomba kabla ya kulala Ili uonyeshwe ni ni kilitokea uwajue wezi,

Ndoto ni kama tu CCTV camera, unarudisha nyuma na kuona matukio yote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom