Hii ndo motisha pekee kwa walimu

Hii ndo motisha pekee kwa walimu

The golden

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2018
Posts
1,383
Reaction score
2,587
Walimu wa tanzania wana motisha moja tu, nayo ni kwenda kusimamia mitihani ya taifa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka. Mwalimu anaweza kukaa hata miaka saba hajapata nafasi hii maana yake hana motisha kwa mda wa miaka saba.

Baada ya ongezeko la 15% la makato ya bodi ya mikopo kuna baadhi ya walimu wanapokea mshahara chini kabisa ya laki tatu.

Mazingira magumu ya kazi huko vijijini yamewafanya baadhi yao kupoteza kabisa matumaini. Wengine wamekuwa walevi wa pombe za kienyeji . Huko kwenye vilabu vya pombe walimu hao wakishalewa huanza kuongea kiingereza na kuwatambia walevi wenzao kuwa wao ni wasomi wa vyuo vikuu.

Kufikili kuwa tunaweza kuboresha hali ya elimu nchini bila kuwajali walimu ni kujidanganya. Kwanza kabisa wanafunzi watawadhalau walimu kutokana na hali zao duni za maisha. Wanafunzi watajenga dhana kuwa elimu haiwezi kumkomboa mtu kutoka katika lindi la umasikini hasa wakiwatazama walimu wao.

Siku hizi huwezi hata kujua mamlaka ya nidhamu kwa walimu ni ipi. Kila kiongozi amegeuka kuwa mamlaka ya nidhamu. Imefika mahali hata wanasiasa wasio na taaluma yoyote leo wanakemea walimu na kuwadhalilisha.

Taifa huandaliwa shuleni. Taifa la watu makini haliwezi kupuuza elimu. Watu wanaopuuza elimu hutawaliwa na watu wenye elimu. Tutafakari.
 
Write your reply...
umeongea ukweli niliona juz kilaza mmoja arumeru eti ataitisha rokoll kuhesabu waalimu,Mara atamfukuza kaz najiuliz kazi ya afisa elimu nnn,tume ya utumishi wa waalimu nnn? vilaza wengine shida
Mkuu, hii sekta imevamiwa. Kila mtu anatafuta umaarufu wa kisiasa kupitia walimu.
 
Mhh
kuna motisha zaidi mkuu wewe huijui tu
 
Upo sahihi mtoa mada nilikaa ktk ualimu miaka 7 nilisimamia mara 1 mtihani tena 2012 tena mpk utengeneze network mpk 2017 baada ya mambo kubadilika kabisa na hali kuanza haieleweki nilipo amua kupga chini ualimu sekta ya uma na Mola kufungua milango mengine ya rizki bado cjajuta
 
Mhh
kuna motisha zaidi mkuu wewe huijui tu
motisha zipi mkuu? Kikubwa ktk ualimu kumejaa fitna na majungu tena baadhi ya halmashauri izo nafasi za usimamizi mpk uhonge ndiyo utoke.... Mwaka mzima unpgania usimamizi usiozidi lak 5 tena isipojua kubembeleza na kitu kidogo hupatiiii. Upuuzi mtupu
 
motisha zipi mkuu? Kikubwa ktk ualimu kumejaa fitna na majungu tena baadhi ya halmashauri izo nafasi za usimamizi mpk uhonge ndiyo utoke.... Mwaka mzima unpgania usimamizi usiozidi lak 5 tena isipojua kubembeleza na kitu kidogo hupatiiii. Upuuzi mtupu
Mkuu naelewa sana ni mwaka wa 7 sasa nimeacha ualimu
Sijawahi juta
Wee endelea kulalamika
 
Me pia nimeshatoka mwaka wa 2 huu pia nimewaacha mbali sn kimaendeleao wale nilioajiriwa nao Ualimu na bado wamebaki huko wkisubiria usimamizi na increment ya elf 15
Absolutely
Hongera mno
 
Bado, motisha hiyo uliyoiainisha ,wakati ukifika motisha hiyo haiwakuti wote.

Binafsi niliamini hivyo , lkn juzi nilimuuliza mwalimu mmoja Wa huko Tanga ,akaniambia waliosimamia mtihani wanasema mtihani ulikuwa rahisi.

Nikamuuliza kwani yy hakusimamia? Akajibu kaambiwa yy alisimamia mwaka Jana hivyo hii ni zamu ya wengine.

Niliudhika saana utadhani ni mm, sikupendezwa haswaa, ndo maana mamlaka za usimamizi zinapohimiza uwajibikaji huambatane na uwajibikaji Wa motisha unaosimamiwa na viongozi.
 
Back
Top Bottom