Hii ndo inaitwa "mwana ukome" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndo inaitwa "mwana ukome"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BigTime, Jan 19, 2011.

 1. BigTime

  BigTime Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 17, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah, wana JF wenzangu; kwa kweli hii hali ya maisha ya Mtized wa kawaida inazidi kuwa ngumu kama vile hatukupendelewa na Mwenyezi Mungu nchi yenye neema ya mali asilia na utulivu uliokuwepo toka mwanzo.. Mimi ni mtanzania wa hali ya kati kabisa, nisiyekuwepo katika chain wala sina damu ya kifisadi, lakini kiboko wanachonipiga serikali ya CCM kimeniingia. Nakuna kichwa na kujiuliza kama mimi ni hivi vipi wale wasio na uhakika wa kupata hata Sh 500 kwa siku.

  Jana nilikuwa nanunua baadhi ya vitu kwa matumizi ya nyumbani ndo nikakumbuka usemi wa marehemu shangazi yangu nilipokuwa mdogo hasa hasa nikijiumiza alikuwa akisema "Hiyo ndo Mwana Ukome" akimaanisha ningekuwa makini nisingeumia. Jamani bei ya vitu kwenye market zimeshoot vibaya mno. HAZIKAMATIKI na nimefanya research yangu ambayo si rasmi sana, kuna tofauti sana katika bei za NOV, DEC na sasa JAN....nimekuna kichwa kujiuliza nchii hii tunaelekea wapi nimeshindwa kuelewa ingawa kuna kila dalili za kufikia level ya TUNISIA (for real i see this coming)...nimenunua vitu very vital ambavyo ni muhimu na ni lazima niwe navyo nimeshtuka saaaana:

  Unga wa sembe per KG, TZS 1,700 (dec 2010 I bought for 1,400)

  Mchele TZS 2,500 (Mwezi Dec ilikuwa TZS 1,700)

  Cooking Gas (Oryx 6 litrs) TZS 35,000 (early Dec was 17,500.00)

  Petrol (Gapco, per Ltr) TZS 1910 (Dec was 1720)

  Sukari (per KG) TZS 2,500 (Dec was 2000)

  Mkate TZS 900 (Super Loaf kitaa walikuwa wanauza 700)

  Umeme ndo usiseme, nimetoa 10,000 nimepata units 32 za luku...(Haya ni masikhara)!

  Nk nk nk nk…huo ni mfano tu wa bei zilivyopanda

  Nikaja kugunduwa kuwa kila mtu siku hizi anapandisha bei kama anavyotaka na mamlaka zetu (ambazo zinataka ziheshimiwe na kutiiwa) zimekaa kimya/lala kama hazipo. Huko mtaani kuna kilio cha kusaga na meno, vitu havinunuliliki kbs, pesa yetu imeshuka thamani isivyo mfano...mfumuko wa bei ni mkubwa kama jinamizi gani sijuwi....wale majirani zangu waliokuwa wakivaa khanga na T-shirts za njano (nakaa Mwananyamala kwa Kopa) wakati wa kampeni ndo wamekuwa wa kwanza kulalama wakajisahau kuwa tukiweka uongozi mbovu, majanga na matatizo kama haya hayachagui mwana-CCM wala mwana-CHADEMA wala CUF, wote mnakumbwa nayo, ni kama mafua vile.....

  Nisiwachoshe, nilitaka kilio changu kisikike, mfumuko wa bei najuwa haumgusi mheshimiwa mkuu na vibosile wengine(najuwa wao ndo wenye mafwedha nnchini; purchasing power yao ni kubwa sana), ila nilikuwa nawauliza kama na wao wana mioyo ya NYAMA kama sie (FRESH HEARTS), na kama jibu ni ndio, wakumbuke binadamu wote ni sawa, hakuna asiyependa kula mara tatu kama wao, kuishi maisha mazuri kama wao, kuwa na imani ya moyo kama wao...........ama sivyo hili chozi na jasho la mnyonge itakuwa ni laana kubwa sana kwao na vizazi vyao, Mungu anaona.


   
 2. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  hawasikii kitu hao, ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, la maana ni kuingia mtaani tu ndio watatoka na taulo kuuliza kulikoni, jibu letu moja tu.... tunataka nchi yetu


  Amani yetu inatumiwa vibaya.
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Haya tuliyataka wenyewe acha tukome ndo macho yatafunguliwa. Kimsingi napenda maisha yendelee kuwa magumu ili maeno ya mwanafalsafa mmoja aliyesema kuwa "uongozi wowote ukiendelea kuyafanya maisha magu kwa wananchi wake, basi watafunguliwa macho na kusimama imara kuupinga uongozi huo.", yatimie!
   
Loading...