Kuna sherehe tatu za maisha katika uhai wa binadamu
1. Kuzaliwa
2. Ndoa
3. Kifo
Vyote hivyo hutokea maramoja tu katika maisha yetu (ukitoa baadhi ya imani za dini wanaoa zaidi ya mara moja ila bado ni ndoa tu)
Katika sherehe hizo tatu ni moja tu ambayo binadamu anaweza kujishughulikia mwenyewe nayo ni NDOA, katika namna ya kawaida tu hamna mtu duniani anayeweza kuacha kumbukumbu kuu ya maisha ya iwe ya hivihivi tu, lazima mtu kwa nafasi yako utafanya kitu kuifanya iwe ya pekee sana ili kupamba kumbukumbu zako kwa siku za usoni. Kwa maana hii ndio maana suala la ndoa sio la kawaida kwa Watanzania tu bali dunia nzima. Tuanze kwenye nchi za kaskzini, huko ndio mpaka kuna makampuni makubwa ya "wedding plan" wanaweza kukuandalia harusi hata mbinguni, kuna maharusi mengi ambayo sio ya kawaida yanafungwa na wazungu achilia mbali hii ya sasa inayoendelea kuleta gumzo ya familia ya kifalme huko uingireza, ninachotaka kuonyesha hapo ni kuwa harusi sio kitu cha kawaida sana.
Kwa mtu anayefuatilia matukio makubwa, harusi za kitanzania ni za kawaida kwa kweli tena ni za kawaida sana sababu nyingi zinamtiririko unaofanana nakubali zipo zinazokufuru ila ukija kuringanisha na za wenzetu kama Kenya au Nigeria..... siwezi kusema gharama sababu mimi si wedding planner ila mtu unaweza ukasema kwa matumizi na maandalizi, jaribu kuangalia CITIZEN tv, ya kenya siku ya jumapili saa moja kama sijakosea utaona kipindi cha wedding afu linganisha na Chereko cha TBC, linganisha hizo harusi!
Ni kweli ni muhimu kuzingatia matumizi kulingana na uwezo wako, na mahitaji ya baadae. Lakini vilevile ni muhimu kwa jamii kuendelea na moyo wa kuchangiana katika matukio ya kumbukumbu kuu za kimaisha na hata katika kupigania uhai wa wenzetu.
Familia yangu tumemuuguza Baba angu, alikuwa anasumbuliwa na figo zili-fail, hao watanzania unaowasema walijitokeza toka kila kona ya nchi hii kuchangia ili Mzee apelekwe japo India tu kubadilishwa hiyo figo... tulitengeneza kadi kama za michango ya harusi ila zilieleza ni mchango wa matibabu India na hela ilipatikana ila Mzee wangu alifariki akiwa bado yupo MUHIMBILI wakati tunasubiria urasimu wa serikali hii (simlaumu mtu).
Mi nadhani hapa mjadala uwekwe kwamba ni muhimu kuboresha kuchangiana kwenye masuala haya ya kijamii, ikiwa kila suala husika watu waonyeshwe uwazi wa hiyo michango na lengo la wazi na manufaa yake. Lakini si sahihi kwamba mabadiliko hayo yawe kwa gharama ya watu wasichangiane kwenye ndoa. Kila tukio lina nafasi yake katika maisha ya binadamu, na watanzania ni binadamu kama hao wengine tu.