Hii ndiyo Tanzania, zaidi ya ile unayoifahamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndiyo Tanzania, zaidi ya ile unayoifahamu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Consigliere, Apr 21, 2011.

 1. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,026
  Likes Received: 7,419
  Trophy Points: 280
  Harusi za kibongo, ni kivutio kingine cha utalii japo zinazidi kutufanya tubaki maskini wa akili na maendeleo.
  Hebu tufikirie kwa pamoja, kwa tukio la harusi tu unakusanya watu zaidi ya mia moja, na wote wanapatikana, koz hawana jambo la maana la kufanya (they have a lot of spare time), wanaandamana na maharusiui wanapokwenda kufunga ndoa, iwe nyumbani au kanisani.

  Then mnakwenda kupiga picha baharini, mkitoka hapo mnakwenda kupiga picha Mlimani City, munaendelea kutafuta kila eneo na jengo zuri lilopo mjini ili mpige nalo picha, mtawashawishi wazungu na waarabu mpige nao picha, then mnakwenda ukumbini, hapo maharusi munawekwa mbele kama vinyago vya mapambo au kombe siku ya fainali.


  Munatekeza millions of money per night achilia mbali zilizokatikia kwenye vikao vya maandalizi. Mbwembwe ni nyingi zinafanya Harusi zionekane ni za kifalme, hata wageni waingiao nchini hujikuta wakishangaa kwa kutojua nini kinatokea na waambiwapo kuwa ni sherehe za harusi, hujikuta wakisikitika sana kwa kudanganywa kuwa Tanzania ni maskini wakati wanachokishuhudia ni tofauti.

  Maisha yanaendelea na maharusi wanarudi mitaani au maofisini ambapo utamaduni wetu wa kupigana mizinga unaendelea kama kawaida, mmoja wa maharusi anapoumwa hakuna wa kujitokeza linabaki suala binafsi, Mungu anaibariki ndoa na watoto wanapatikana wakati wa kuwapeleka shule unapofika na uchumi kutokuwa mzuri hakuna mchangiaji anaejitokeza kusaidia wanasema kila mtu na abebe mzigo wake.

  Watoto wakifika muda wa kuoa au kuolewa hapo ni suala la ku-report kwenye kamatiza kudumu za harusi zilizoundwa.


  Hivi jamani kwa nini kamati hizi za kijamii zisingekuwa kwa ajili ya maendeleo ya kielimu ya vijana wetu, milioni 25 tunazoziteketeza kwa tukio la siku moja unadhani zingesomesha wanafunzi wangapi.


  Misaada tunayoipata kutoka kwa nchi wafadhili ieleweke kuwa ni matokeo ya raia wa nchi hizo kuamua kujibana na kubadili mfumo wao wa maisha kimatumizi ili waweze kutusaidia sisi katika mambo mbali mbali ya kijamii. Kwanini sisi tunashindwa kufanya hivyo kwa ajili yetu wenyewe.


  Kama kuna kitu kinaitwa kubana na kupunguza matumizi au matumizi yenye nindhamu basi na kianzie kwetu binafsi na ndani ya familia zetu, bila ya hivyo tabia hii itakua , kukomaa na kuwa sugu, na kujikuta na sisi bila ya kujijua tumejiandaa kwa muda mrefu kuwa aina fulani ya wafujaji ambao tunasubiri kugeuka kuwa mafisadi.


  Behaviors are only comfortable but behavior change is possible.

  Tujiulize na kufanya maamuzi ya busura tungali vijana kwa maendeleo yetu na vizazi vijavyo

  Hii ndiyo Tanzania, zaidi ya ile unayoifahamu.
   
 2. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Mawazo yako ni mazuri lakini nafikiri haikufaa kwenye Jukwaa la siasa, please mod pelekeni hii thread panapohusika
   
 3. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,807
  Likes Received: 1,142
  Trophy Points: 280
  aanze ****** kwanza kupunguza magari ya msafara wake kama mfano
   
 4. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  true 100% Aisee utamaduni (culture) ni kitu cha ajabu sana. Utashangaa jinsi wamasai wanavyohangaika na ng'ombe porini. Au wengine kuishi uchi huku wamevaa shanga za gold kilo nzima viunoni. Sijui Mungu anahusika? Manake duh
   
 5. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Najua matatizo ya ndoa za mkeka mkuu, pole kwa yaliokukuta.
   
 6. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kuna sherehe tatu za maisha katika uhai wa binadamu
  1. Kuzaliwa
  2. Ndoa
  3. Kifo

  Vyote hivyo hutokea maramoja tu katika maisha yetu (ukitoa baadhi ya imani za dini wanaoa zaidi ya mara moja ila bado ni ndoa tu)
  Katika sherehe hizo tatu ni moja tu ambayo binadamu anaweza kujishughulikia mwenyewe nayo ni NDOA, katika namna ya kawaida tu hamna mtu duniani anayeweza kuacha kumbukumbu kuu ya maisha ya iwe ya hivihivi tu, lazima mtu kwa nafasi yako utafanya kitu kuifanya iwe ya pekee sana ili kupamba kumbukumbu zako kwa siku za usoni. Kwa maana hii ndio maana suala la ndoa sio la kawaida kwa Watanzania tu bali dunia nzima. Tuanze kwenye nchi za kaskzini, huko ndio mpaka kuna makampuni makubwa ya "wedding plan" wanaweza kukuandalia harusi hata mbinguni, kuna maharusi mengi ambayo sio ya kawaida yanafungwa na wazungu achilia mbali hii ya sasa inayoendelea kuleta gumzo ya familia ya kifalme huko uingireza, ninachotaka kuonyesha hapo ni kuwa harusi sio kitu cha kawaida sana.
  Kwa mtu anayefuatilia matukio makubwa, harusi za kitanzania ni za kawaida kwa kweli tena ni za kawaida sana sababu nyingi zinamtiririko unaofanana nakubali zipo zinazokufuru ila ukija kuringanisha na za wenzetu kama Kenya au Nigeria..... siwezi kusema gharama sababu mimi si wedding planner ila mtu unaweza ukasema kwa matumizi na maandalizi, jaribu kuangalia CITIZEN tv, ya kenya siku ya jumapili saa moja kama sijakosea utaona kipindi cha wedding afu linganisha na Chereko cha TBC, linganisha hizo harusi!
  Ni kweli ni muhimu kuzingatia matumizi kulingana na uwezo wako, na mahitaji ya baadae. Lakini vilevile ni muhimu kwa jamii kuendelea na moyo wa kuchangiana katika matukio ya kumbukumbu kuu za kimaisha na hata katika kupigania uhai wa wenzetu.
  Familia yangu tumemuuguza Baba angu, alikuwa anasumbuliwa na figo zili-fail, hao watanzania unaowasema walijitokeza toka kila kona ya nchi hii kuchangia ili Mzee apelekwe japo India tu kubadilishwa hiyo figo... tulitengeneza kadi kama za michango ya harusi ila zilieleza ni mchango wa matibabu India na hela ilipatikana ila Mzee wangu alifariki akiwa bado yupo MUHIMBILI wakati tunasubiria urasimu wa serikali hii (simlaumu mtu).
  Mi nadhani hapa mjadala uwekwe kwamba ni muhimu kuboresha kuchangiana kwenye masuala haya ya kijamii, ikiwa kila suala husika watu waonyeshwe uwazi wa hiyo michango na lengo la wazi na manufaa yake. Lakini si sahihi kwamba mabadiliko hayo yawe kwa gharama ya watu wasichangiane kwenye ndoa. Kila tukio lina nafasi yake katika maisha ya binadamu, na watanzania ni binadamu kama hao wengine tu.
   
 7. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,026
  Likes Received: 7,419
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa pole kwa yote yaliyokupata ndugu yangu na Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema mzee wetu.
  Pili nawapongeza watu waliojitokeza kutoa michango ya ili kunusuru hali ya mzee, kwani wamefanya jambo ambalo limenigusa sana, jambo ambalo nadhani kwa kipindi hiki ndiyo tunalihitaji kwa nguvu zote.
  Nikirudi kwenye mada:-
  Uliyoyata ni mambo ya kiroho japo hukamilishwa na mwili, lakini unahitaji kuyapokea kwa msisimuko wa kiroho zaidi ili uweze kuishi maisha ya uadilifu kuweza kuilinda ndoa yako.
  Haikatazwi kufanya sherehe za harusi, tatizo ni tabia na mitazamo ambayo imekuwa ikijengeka katika sherehe hizi, kwani imekuwa ni fasheni zaidi, isiyo na mwitiko wa kiroho hata kwa maharusi wenyewe na huishia kusisimua akili zao, kitu kinachofanya dhamira yake isiwe tofauti na lengo la mtu kunywa mvinyo.
  Pia ni jambo sahihi kama mtu atalifanya kwa bajeti yake mwenyewe badala kuweka utegemezi kwenye michango ya watu, na nafasi ya michango hiyo ingechukuliwa kwa ajili ya activities nyingine katika jamii.
  Unaweza kulitazama katika mtazamo wako, sawa, lakini lakini tunahitaji sana mabadiliko for the better future.
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 9. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Sioni ubaya wa kufanya sherehe kulingana na uwezo wa watu waliotayari kuchanga kufanya hiyo harusi kwa sababu ni utamaduni tu ambao tayari naona umeanza kupungua kidogo sana. hivyo baada ya muda idadi ya watu wa kuchanga na kuhudhuria sherehe za harusi itapungua.

  Ila kibaya pengine ninachoona ni kwa baadhi ya watu kutaka kufanya sherehe kubwa wakati hana watu wanaomfahamu na wako tayari kutoa michangao mikubwa ya harusi hivyo wanaanza kulazimisha michango hata kwa watu wasio wafahamu maharusi tena wanadai utafikiri ni deni
   
 10. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #10
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehe
   
 11. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,026
  Likes Received: 7,419
  Trophy Points: 280
  Hapa ndiyo hata mimi panaponipasua kichwa, kwasababu mtazamo unaokuja kujengaka huko tuendako ni kuwa kama huna hela ya kuandaa sherehe kubwa za harusi basi bado huja-qualify kufunga ndoa au kuolewa.
  Wasi wasi wangu hali hii itawaathiri watu wengi na kuwaondoa katika soko la ndoa.
   
 12. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Mimi kusema kweli natamani sana kama hizi sherehe za arusi zingepigwa marufuku kabisaaa..! Maana naona ni uchezeaji wa hela bila sababu. Kwanza siku hizi kabla ya harusi kuna sherehe kama saba zinatangulia ambazo hazina maana yoyote kimsingi. Utasikia ooh ingejimenti, ooh kichen pati, oooh sendi ofu, ooh bachela pati, ooh sijui nini, bado baada ya harusi mara ooh kuvunja kamati... Na kila sherehe ni mamilioni ya hela yanateketea! Jamani! Baada ya sherehe maharusi wanabaki hawana hata kumi. Cha kusikitisha zaidi, hata michango iwe milioni mia, yoooote inaingizwa kwenye bajeti! Inaliwa yote siku hii... 1
  Hata kama una watu wa kukuchangia sawa, lakini hivi hizo hela hazina kazi nyingine? Huku maofisini watu tumeshachangia harusi mpaka karibu tutakosa hela ya kula.
  Halafu baada ya miezi sita ndoa imevunjika.
   
 13. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Ninachoona wenzetu wa nchi nyingine maarusi hutumia fedha zao wenyewe baada ya kujiandaa sio za kuchangishana (wakati mwingine hulazimisha) nadhani huu mfumo uendelee lakini kwa hela za wanandugu wa bwana harusi/bibi harusi, lakini siku hizi unaletewa kadi na watu hata huwafahamu, iko haja ya kubadilika.
  Tuchange mambo ya maendeleo, je unafahamu Shs. 10,000,000/= zinaweza kusomesha (Ada) yatima 500 ktk shule ya sekondari kwa mwaka? Au karibu watoto 120 toka form I mpaka IV kuliko kuzitafuna kwa siku moja?
  Mara nyingi harusi za kifahari hazidumu au zinakuwa na matatizo (sio zote)..
   
 14. m

  mkwega Member

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwel jamani
   
 15. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Michango kila siku hadi kadi kumi kwa mwezi!
  vikao kila wikiend utadhani hamna mapumziko wala mashamba...
  simu kibao za kukumbushana..tena mchango una kiwango cha chini! Duh
  mi nikioa nitwakaribisha tu
   
Loading...