Hii ndiyo Tanzania mpya chini ya Lowassa!

Hii ndiyo Tanzania mpya chini ya Lowassa!

Wanasema hata walipokuwa CCM walitaka mageuzi!

Hawasemi ni mageuzi gani waliyataka ndani ya CCM kwa sababu hatukuwahi kuwasikia wakitamka neno mageuzi au kuionya CCM kuhusu kupuuza ajenda zao.

Hata mageuzi wanayoyasema kwa sasa ni vague. Neno mageuzi linatumika kama justification ya kuomba kura.

Mawazo mapya wameyapata baada ya kuzeekea ndani ya CCM. This is fun!

Makongoro alitoboa siri kuwa, mageuzi waliyoyataka Lowassa na timu yake ndani ya CCM ilikuwa ni kumpindua JK anyang'anywe uenyekiti ili asiwazibie mambo yao.

Source: Hotuba ya Makongoro Nyerere ya kutangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM.
 
Ukawa ina majembe ya hatari,baada ya uchaguzi watanzania watakuwa wameanza kuonja raha na matunda ya amani na Uhuru wa nchi yao iliyojaa raslimali tele
Majembe ya hatari ndiyo nini?

Kwani kwa sasa watanzania hawaonji raha, matunda ya amani na uhuru? Au una maana gani unaposema raha, matunda ya amani na uhuru?
 
Mithali16:31" Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu km kikionekana kwenye njia ya haki". kwahyo hao wazee tuwape heshima yao.
Njia ya haki ni ipi katika mantiki ya andiko lako?
 
Haaa aibu sura za waliokuza Chadema wako wapi siku hizi?

Picha hiyo ni sura za wana ccm wanaoogopa Magufuli akiingia awatapata pa kula.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Jamani eeh!! Hizi propaganda tunazing'ang'ania hazina msingi wowote ule!! Kwani Sumaye, Kingunge na Mwapachu wanagombea majimbo gani?! Hao ni watu waliotoka tu CCM na wameamua kumsapoti Lowassa si kwa sababu wanataka kuchaguliwa kuwa viongozi endapo Lowassa atashinda uchaguzi huu.....kwahiyo leo hii mtu akitoka CCM basi hana haki ya kuchagua chama au mtu wa kumsapoti ktk kipndi hiki cha uchaguzi?!
Mtu makini tu ndio ataelewa nazungumzia nini hapa!
 
Wanasema hata walipokuwa CCM walitaka mageuzi!

Hawasemi ni mageuzi gani waliyataka ndani ya CCM kwa sababu hatukuwahi kuwasikia wakitamka neno mageuzi au kuionya CCM kuhusu kupuuza ajenda zao.

Hata mageuzi wanayoyasema kwa sasa ni vague. Neno mageuzi linatumika kama justification ya kuomba kura.

Mawazo mapya wameyapata baada ya kuzeekea ndani ya CCM. This is fun!

Hata Magufuli anahubiri mabadiliko ndio maana JK anahofia kuvunja baraza la mawaziri.
 
Haya ndiyo Mabadiliko Lowassa, Lowassa mabadiliko!

Hii ndiyo safu ya Tanzania mpya yenye fikra mpya!

Kuna wengine wamekuwa viongozi katika nafasi za juu kabisa za utendaji kabla hata nchi haijapata uhuru!

Hii ndiyo safu itakayowakimbiza Watanzania kimaendeleo kwa speed ya 120 Km/h!

Ninashindwa kuelewa kama ninaota au ninaishi kwenye ndoto!

There are no desperate situations, there are only desperate people-Heinz Guderian

What changes are we going to get from these senior citizen/pensioners?

Hayo ndiyo mabadiliko tunayoyataka?

Unreasonable haste is the direct road to error!

Tanzania iko mbioni kuingia kwenye Guinness World Records!

12109036_1511170319203725_7893429866689020787_n.jpg

c
Heh heh kweli hii ni CCM B Chadema wako wapi,halafu hawa wote wana fikra mgando,Chadema imeondoka na Dr Slaa
 
Shame wapi na ndiyo ukweli wenyewe?!!! Hao vikingwe ndiyo mabadiliko ?!! Tunatumia matatizo ya Watanzania kuwakejeli tu hapa...
Hawa jamaa mpaka wamekuwa pensioners ndani ya CCM na serikali yake eti leo wanasema watawakimbiza watanzania kiuchumi katika speed ya 120Km/h.

This is shaggy dog story!
 
Majembe ya hatari ndiyo nini?

Kwani kwa sasa watanzania hawaonji raha, matunda ya amani na uhuru? Au una maana gani unaposema raha, matunda ya amani na uhuru?

Hospitalini hakuna dawa,wamama wajawazito wanajifungua huku wakuwa wamelala watatu kitanda kimoja,shule hazina vifaa vya kutosha vya kujifunzia na kufundishia,wanafunzi wanakaa chini,mfumuko wa bei,halo mbaya ya kiuchumi,nk wenye akili wameelewa
 
Kweli mkuu hii ni safu mpya ya mchakamchaka, yenye kasi mpya 120mph na mtandao mpya wa walewale...hongereni

Hii safu ya pensioners inataka kuwakimbiza Watanzania kimaendeleo katika speed ya 120Km/h. Tanzania hatukosi maajabu!

Tuko mbioni kuingia kwenye vitabu vya maajabu!
 
Picha zao tu zinaonesha wote taabani.
Hawa ndiyo viongozi wakuu wa mabadiliko kutoka CHADEMA!

Wamezeeka na kuwa pensioners ndani ya CCM na serikali yake, kwa sasa eti wamepata maono ya mageuzi!

Kuna utani mwingine haufai hata kuusema!
 
Sisi hayo unayoyaangalia na kuyawaza sio kazi yetu kazi tuliyonayo kwa sasa na tunachotaka kwa sasa ni kuitoa ccm madarakani tu na sio vinginevyo awe na speed asiwenayo cc hatuangalii hilo
Wewe na nani?

Jisemee nafsi yako!

Ni haki yako kikatiba kuchagua kiongozi yoyote lakini haitaondoa ukweli katika msingi wa mada yangu.
 
Lumumba naona mmecharuka sana.kiasi kwamba umekosa cha kuandika.nenda ukauze ngadu kijana.
Lumumba ndiyo wapi?

Kama ningekuwa nimekosa cha kuandika usingepata cha kujibu.

Nani amekuambia mimi ni kijana?

Jibu hoja na kama unadhani hakuna hoja, unaweza kuachana na thread.
 
Ninachokiona ni wao kushindwa kwenye huu uchaguzi licha ya makelele yao mengi. Na baada ya hapo upinzani uliojengwa Tanzania kwa zaidi ya miongo miwili utakuwa umerudishwa nyuma kwa miaka mingi sana. Hapo ndipo CCM, baada ya kujishtukia na kujipanga upya, wataendelea kutawala nchi hii kwa kipindi kirefu kijacho.
Uchaguzi huu ni make or break kwa CHADEMA na hasa viongozi wake wakuu.

Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania.

ACT-Wazalendo wako mbioni kunufaika na matokeo ya uchaguzi kwa sababu CHADEMA iko mbioni kufuata nyayo za NCCR-Mageuzi.
 
Tukubali tu CCM hali ni Ngumu.Hao vigogo na walioko nyuma Yao si mchezo.Kweli huu mwaka wa upinzani.Kila dalili Inaonyesha hivyo. Wanao beza wanajiliwaza tu.
Unaodhani ni vigogo inawezekana ndani ya CCM siyo vigogo, kwa maana nyingine, political top gun wa CHADEMA kwa CCM ni lightweight/nobody.

Hoja ya msingi ni kukutana na hawa pensioners kwenye majukwaa wakiomba wapewe dola kwa sababu wanataka kuwakimbiza watanzania kimaendeleo katika speed ya 120Km/h. Really?
 
Hospitalini hakuna dawa,wamama wajawazito wanajifungua huku wakuwa wamelala watatu kitanda kimoja,shule hazina vifaa vya kutosha vya kujifunzia na kufundishia,wanafunzi wanakaa chini,mfumuko wa bei,halo mbaya ya kiuchumi,nk wenye akili wameelewa

Ndicho anachouliza mtoa hoja kwamba je hawa wastaafu walioshindwa kulifanya hilo wakiwa na nguvu zao ndio wataweza kulifanya wakiwa wamezeeka tena kwa speed ya 120km/hr?
 
  • Thanks
Reactions: snn

Similar Discussions

Back
Top Bottom