Hii ndiyo Ripoti iliyowang'oa mawaziri (Ripoti ya Lembeli)

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,216
Wakuu,

RIPOTI ILIYOWANG'OA MAWAZIRI HII HAPA;

Hongereni kwa kazi nzuri na nawapa pole wale wote waliopatwa na matatizo mbalimbali wakati wa hii operesheni. Mungu ibariki Tanzania na watu wake
 
Kwa ripoti hii,

Sio mawaziri tu7, wengi wanatakiwa wajiuzuru na wengine wafikishwe mbele ya sheria

Hii ndio tabu ya kukabidhi wanajeshi operesheni, hii kazi ilitakiwa ifanywe na polisi wanaojua sheria sio vita.

Ushabiki wa kisiasa pembeni, sheria na haki za binadamu zilikiukwa kwa kiasi kikubwa sana.

Naiomba serikali iwafikishe mbele ya sheria wale wote waliokiuuka haki za binadamu na kuvunja sheria za nchi
 
Kwa ripoti hii,

Sio mawaziri tu7, wengi wanatakiwa wajiuzuru na wengine wafikishwe mbele ya sheria

Hii ndio tabu ya kukabidhi wanajeshi operesheni, hii kazi ilitakiwa ifanywe na polisi wanaojua sheria sio vita.

Hii ndio taabu ya kukabidhi nchi kwa ukoo wa nyang'au ccm.... ni mawaziri wangapi watakaojiuzulu?
 
Hii ndio tabu ya kukabidhi wanajeshi operesheni, hii kazi ilitakiwa ifanywe na polisi wanaojua sheria sio vita.
Mkuu si umeona lakini hata wao wamepoteza watu kwa maana hiyo kutakuwa kulikuwa na resistance sehemu zingine, jeshi ndio lilistahili kutoa mwongozo kwenye ujangili wa wanyama pori lakini kwenye maswala ya ardhi kunahitajika hata mapolisi kweli, unless jamaa wanakaidi (bila ya kutetea uhalifu uliotendeka lakini wajameni wafugaji wameshaonywa sana kuingilia sehemu za hifadhi).

Kitu ambacho sielewi kwanini sasa hao mawaziri wafukuzwe kazi au kwanini yule mwengine kajiudhuru. Maana kwa jinsi nilivyosoma na kuelewa operesheni ilitekwa na jeshi na wengine wakawa hawana taarifa and we all know jeshi letu no nonsense na lenye kiburi. Unless kama walikubali ki hiari wao wenyewe kutotaka habari, lakini vinginevyo mtu wa kufukuzwa kazi hapa ni mkuu wa majeshi maana under his leadership ndio watu wame misbehave.

Na kwanini kamati aikumuhoji mkuu wa majeshi awape sababu zilizomfanya asiwe anawapa wenzie habari au kwanini hakuona umuhimu wa kushirikisha nguvu ngazi zilizopo locally, maana at the end of the day ni wao (jeshi) ndio walioiteka operation to me all the blame lie with them na si mawaziri waliobezwa unless labda mtu aseme makosa yapo wapi.
 
Tundu Lissu amelia na Amiri Jeshi wa JWTZ kwa kuamrisha Wanajeshi kwenda kwa Raia bila hata ya kutangaza hali ya hatari au lolote la muhimu. Amiri jeshi Mkuu, kwa maana hiyo, amevunja katiba. Hili linaweza kuja kuzuka tena baada ya mwaka 2015 mara akija Rais mwingine. Ilibidi hadi Mama Makinda amshangilie Lissu kuwa kaongea kama Mwanasheria.
 
Na ndivyo navyoona mimi hapa wakufukuzwa kazi ni mkuu wa majeshi, maana yeye ndie kawaponza wenzie, katika nchi ambayo siasa hazina mechanism zakueleweka people behave as they wish with power and authority. Na hapa kwangu wengine wameonewa tu.
 
Mbona sioni majina ya Wabunge na viongozi wa Vyama walitajwa na hii Ripoti kuwa wanahusika?

Hata Katibu mkuu wa Nishati na Madini na ile akaunti yake ya NMB 206010100044 inayotuhumiwa kutunika sijaona humo?

Vipi number za Mpesa za kupokelea rushwa sijaziona ?

Bado nauliza tena MKUCHIKA mkuu wa Usalama wa Taifa anakosekana kwenye hili kivipi?
 
Nafikiri Lissu atakuwa kasaidia sana na hasa watu wa Mtwara ambao waliletewa tu JWTZ na sijui kama wameshaondolewa. Unaleta tu wanajeshi na wanaanza kupiga watu, kisa Pinda amepinda.

Na ndivyo navyoona mimi hapa wakufukuzwa kazi ni mkuu wa majeshi, maana yeye ndie kawaponza wenzie, katika nchi ambayo siasa hazina mechanism zakueleweka people behave as they wish with power and authority. Na hapa kwangu wengine wameonewa tu.
 
Nafikiri Lissu atakuwa kasaidia sana na hasa watu wa Mtwara ambao waliletewa tu JWTZ na sijui kama wameshaondolewa. Unaleta tu wanajeshi na wanaanza kupiga watu, kisa Pinda amepinda.

Mkuu hila hao jamaa waliombwa sana watulie na madai yao, besides walianza uhalifu wa kuchoma mahakama, majengo ya serikali na nyumba za viongozi wa CCM wasio na majukumu kwenye sheria za gesi. It served them right in my opinion considering their provocation to the authority na vitisho vyao kwa serikali.
 
Kesho naamka nayo wacha nilale
ukiacha malengo walipangiwa wao walifuta na kuweka yafuatayo;
1. mauaji ya raia wasio na hatia -mama yetu wa Galapo
2. ubakaji
3.uporaji
4.unyang'anyi wa silaha za hali
5. kuwalinda na kutowapughudhi well placed individuals
6. kuonea wanyonge wasio na kinga
 
Mmmhhhh nahisi wewe ni mjeshi sio bure. Kwa hiyo wewe unaona hii iko poa tu
 
Hi nchi imechafuka kiasi hiki yaani kero tupu tunahitaji mabadiliko makubwa sio kila siku baraza jipya CCm imechoka waondoke wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…