Hii ndiyo Ripoti iliyowang'oa mawaziri (Ripoti ya Lembeli)

Umeona eeh
Japan kwenyewe waziri mkuu aliyedumu muda mrefu ni Koizumi; na ni miaka 4. Abe aliwahi kutawala less than a year.

Sasa nambie kama wangekuwa wanayumbishwa na sera za kisiasa wangekuwa hapo walipo?

Wanasiasa wanaua hii nchi...

Nakwambia South East Asian Countries zote wanajua kuwa maendeleo yao yameletwa na bureaucrats na wala si chama fulani wala mwanasiasa fulani. Na mtu akisema yeye ni bureaucrat ni heshima kuuubwa kwa wananchi wanaomzunguka.


Wanasiasa ubadilika kila muda, lakini civil service haibadiliki. Ingekuwa nao wanabadilika kwa mtindo wa wanasiasa nchi zisingekuwa endelevu na stable. Ebu fikiria Italy ambako walikuwa wakibadilisha Serikali kila miezi Sita au mwaka mmoja, hali. Ingekuwaje? Watu hawabainishi ama kwa kutokujua au vinginevyo kati ya civil service na political leaders. Ili ndilo tatizo lililopo sasa hapa nchini ukiwasikiliza viongozi wa Chama tawala kwa kauli na kuangalia matendo yao.
 
We kinachokusumbua ni uzumbukuku!!!!!!!! Bora hawa ccm nini? C ndo hawa wanafanya kampen huku wanatoka na wake za watu? tena bora unyamaze kabisa kama hujui siasa na ukome kutuletea umbeya hapa viongozi wa nchi siyo wa dini hatuchagui wanaoingia pepon ndo mana Mandela na ufuska wake anabaki kiongoz bora wa karne!
 
...Kitu ambacho sielewi kwanini sasa hao mawaziri wafukuzwe kazi au kwanini yule mwengine kajiudhuru. Maana kwa jinsi nilivyosoma na kuelewa operesheni ilitekwa na jeshi na wengine wakawa hawana taarifa and we all know jeshi letu no nonsense na lenye kiburi. Unless kama walikubali ki hiari wao wenyewe kutotaka habari, lakini vinginevyo mtu wa kufukuzwa kazi hapa ni mkuu wa majeshi maana under his leadership ndio watu wame misbehave.

Na kwanini kamati aikumuhoji mkuu wa majeshi awape sababu zilizomfanya asiwe anawapa wenzie habari au kwanini hakuona umuhimu wa kushirikisha nguvu ngazi zilizopo locally, maana at the end of the day ni wao (jeshi) ndio walioiteka operation to me all the blame lie with them na si mawaziri waliobezwa unless labda mtu aseme makosa yapo wapi.


Hawa waheshimiwa wamejiuzulu kwa sababu za kisiasa. Ukweli ni kwamba zoezi zima lilitungwa na kuratibiwa na wizara ya mali asili. Jeshi lilitumika katika utekelezaji tu! Katika mazingira ambapo hata ndani ya wizara yenyewe hakukuwa na mawasiliano mazuri, ni wazi kuwa hata jeshi lenyewe huenda hata halikupewa maelekezo (adidu rejea) za nini kunatakiwa kufanyika kwa masharti gani na katika mipaka ipi. Inaonyeka kana kwamba jeshi liliambiwa tu kuanza kazi - na wakaachiwa kufanya wanavyojua! Aidha hata kama walipewa adidu hizo - ni wazi hakukuwa na namna yoyote ya kuhakikisha maelekezo yanafuatwa.
Katika mazingira hayo waziri - ilibii tu aachie ngazi kwa kushindwa kudhibiti shughuli za wizara yake. Ndio maana hao jamaa 4 wakatoka... kwa kuwa ndizo wizara zilizohusika katika utekelezaji.
Pamoja na kusema hayo; ninaamini mfumo mzima wa utendaji katika wizara zetu unatakiw akutazamwa upya. Haiwezekani katika namna ya kawaida, katibu mkuu akajiamulia tu kufanya anavyofanya - tena bila kumuhusisha waziri na anabaki anapeta tu! Lazima kuna walakini. Na kwa juu juu; both waziri na katibu mkuu ni wateuliwa wa Raisi - Raisi ndio bosi wao! Tatizo, katibu mkuu ana ka-power zaidi kwani si tu ana uhakika zaidi wa kuendelea kuwepo kwenye system kuliko waziri; bali pia ana nguvu ya fedha (kama "warrant Officer"... waziri akitaka kusafiri - inambidi apate "go ahead" ya PS; la sivyo no "masurufu" - wapi umeona hiyo?
Kinachotakiwa hapa ni kuufanyia tathmini mfumu mzima wa utendaji wa serikali na kuubadilisha au kuurekebisha kwa kadri inavyostahili. La sivyo tutabadilisha mawaziri hadi mwisho wa dunia na bado uozo utaendelea kuwepo!

Cheers
 
Ukweli ni kwamba, hakuna dhamira ya dhati ktk hili; wakurupuka kutoka usingizini na ndiyo maana kasoro ni nyingi kuliko mafanikio. Mfano mzuri, boss wa JWTZ mbona wamemfumbia macho pamoja na askari walioshiriki kufaya maovu?!
 
siku zote shetani huwa ana lugha nzuri sana kukuvutia ili umuone kama yeye ndo Mungu. Tuliletewa lugha ya maisha bora kwa kila mtz, hizi ni lugha za kishetani. Hata mungu mwenyewe alipokuwa akiwatoa wana wa israel kwenye utumwa hakuwaahidi mema kiasi hiki. Kazi ya shetani ni kuua na kuharibu. hii ndo serikali ya kung'oa kucha, meno na kuua wananchi kwa risasi. Chadema au cuf nao wangekuwa kwenye serikali wangesema ni wao walioua. Namshangaa huyo chris glucos anayetamba huku mitandaoni kila kukicha kuwa ccm no chama kinachosikiliza wananchi. leo anakula mharo wake. aibu. Simama kwenye ukweli na siyo njaa zikutume kuukataa ukweli. Jehanamu inawangoja.
 
Ningependa kujipatia nakala ya ripoti ya Lembeli kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili ili nijiongezee maarifa na ufahamu.
 
Back
Top Bottom