Hii ndiyo rekodi ya uchapakazi wa Lowassa

This is how you cheapen and trivialise critical issues of integrity by associating them with the coming elections. If any of you has balls he shoud come forward with issues that will make sense and vindicate Lowassa. No body will feel intimidated and desist from airing his views merely because a section of people are so myopic as not to realise how dangerous Lowassa is to our plight as a Nation. Call us anything but let truth be told!
Mbopo

When did you come to realise that Lowassa is dangerous before or after the election, if so then who is myopic.

Lowassa for Chairman

images

Kuna mengi zaidi hayo..waliowahi kufanya naye kazi wanasema he is greedy, rude and selfish. Mtu wa namna hii hafai kabisa kuwa kiongozi. Kuna kampuni zinaitwa alfa...from what I here everything that starts with the word alfa has something to do with him kupitia kwa mgongo wa mtoto wake fred. Ana radio 5 FM na hivi karibuni atafungua ABC TV nchi nzima. Mtumishi wa serikali kapata wapi uwezo wa kuinvest to this extent? Hatufai hata kidogo.[/QUOTENakuunga mkono.Tatizo la Watanzania huwa hawaangalii mambo kwa undani zaidi.Kiongozi wa juu hapaswi kuwa na visasi, kufanya uwamuzi mgumu hata kwa mambo yanayohujumu uchumi wa nchi, kutumia uongozi vibaya kama kufukuza watumishi wa serikali kwenye mikutano ya hadhara na kutaka uongozi hatakama itagharimu maisha ya watu.Wanaoshabikia mtu wa aina hii ni wavivu wa kufikiri na kufanya utafiti.

KUWE NA UTAMADUNI WA KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA, MTOA MADA HAUNA MADA HAPO NI MAJUNGU MATUPU. weka mambo ubaoni watu waelewe, naona unamchukia EL bila hata kujua, usidandie train mbele. Huyu jamaa ni kiongozi unabisha? Halafu mtafute muadilifu kwa vigezo vyako umuweke jamvini kwa vigezo vyako tumchambue.

Napenda mabadiliko ya dhati sio fitna. Umeshawahi kumsikia Slaa akimchambua huyu jamaa kwa undani na ufisadi wake? Ana akili, tulia utajua tu.

Wana JF, kwa muda mrefu kumekuwa na maelezo yanayokinzana, hasa kuhusiana na uadilifu na uwezo wa uchapakazi wa Lowassa kwa kipindi cha utumishi wake kwa nchi hii, na hasa katika nafasi za uwaziri alizozishikilia. Kama namna nzuri ya kujaribu kutafakari utendaji wake, tujikumbushe kidogo alikopitia Lowassa.

1. Mwanzoni mwa miaka ya 90 Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulikia majanga, na itakumbukwa kwamba huu ndiyo wakati ambao mikoa ya kusini na hasa Mtwara walikumbwa na mafuriko yaliyoteketeza maisha ya watu pamoja na mali zao na baadhi ya athari hizo bado hazijarekebishwa. Akiwa ndiye mhusika mkuu, Lowassa aliratibu upatikanaji na utoaji wa misaada na inasemekana alijinufaisha yeye binafsi kutokana na janga hilo kwani mingi ya misaada haikuwafikia walengwa.

2. Baada ya kutoka hapo, Lowassa alipelekwa Wizara ya Ardhi na ni katika kipindi hiki ndipo tulishuhudia kilele cha migogoro ya ardhi (double allocations) maeneo ya Mbezi Beach, na hata kuporwa kwa maeneo ya wazi na kuyatolea hati, hasa maeneo ya Masaki, Msasani Peninsular na Oysterbay, katika mazingira ambayo yanaashiria kwamba kulikuwa na vichocheo vya rushwa. Ni katika kipindi hiki ndipo rushwa ilipokithiri wizarani na yeye mwenyewe kujilimbikizia viwanja, majumba na utajiri ambao ulikuja kuhojiwa na Mwalimu mwaka 1995 alipogombea nafasi ya kugombea urais. Ndicho kipindi cha kushamiri kwa wahindi kama Fida Hussein na Baghdad katika kupora viwanja na inasemekana Baghdad alikuwa na viwanja 100 Dar peke yake. Hadi leo serikali inahangaika kufanya revocation ya hati alizozitoa Lowassa katika mazingira ya utata.

3. Wizara ya Maji na Mifugo. Shida ya maji jijini Dar es Salaam iliongezeka na mtandao wa maji nchini uliendelea kuwa duni na kushindwa kusogea kwenye malengo ya serikali ya maji safi kwa kila mtanzania kufikia 2015. Ndicho kipindi cha utapeli wa Dawasco na wawekezaji wa Bi-Water baada ya kuona karibu atashtukiwa aliwafurusha na kuzua kesi iliyoigharimu serikali mabilioni katika kuiendesha. Alizunguka nchi nzima na kuhimiza wananchi wajenge wabanda ya ng'ombe, akiahidi kukopesha ng'ombe ili wananchi walipe ng'ombe. Mabanda haya sas yamegeuka maghala baada ya miaka inayokaribia 10 ya kusubiri. Hali ya soko la wanyama wetu ilibaki kuwa isiyo na ufumbuzi, licha ya yeye kutoka katika jamii ya wafugaji.

4. Ofisi ya Waziri Mkuu. Zaidi ya kututwisha mzigo wa Richmond, na kudandia hoja ya sekondari za kata iliyoasisiwa na utawala wa Mkapa, hakuna la kujivunia zaidi ya kukemea na kudhalilisha wafanyakazi wa chini yake. Aliendesha vikao vya kujadili bei za mazao na kuwaita wakuu wa mikoa na wilaya lakini hakuna ufumbuzi wa maana aliokuja nao kuhusu bei za mazao yetu kama pamba, korosho, kahawa, chai na pareto.

Mimi nawasilisha maoni kwamba utumishi wa Lowassa umegubikwa na kukosa uadilifu na kushindwa kuleta tija inayohitajika kwa watanzania. Hoja za kwamba alikuwa mchapakazi ni porojo tu za kudhani zitaficha maovu ya ufisadi wake.

"Hii ndiyo rekodi ya uchapakazi wa Lowassa"

Nakuomba ubadiri heading yako isomeke hivi "Maovu ya Lowassa" hapo nitakuona great thinker na hujatumwa na Nape lakini Ukisema hiyo ni record ya uchapakazi wake nitakuona ni mnafiki maana hakuna Waziri Mwenye record ya Mambo mazuri tuu au mabaya tuu.

wana jf, kwa muda mrefu kumekuwa na maelezo yanayokinzana, hasa kuhusiana na uadilifu na uwezo wa uchapakazi wa lowassa kwa kipindi cha utumishi wake kwa nchi hii, na hasa katika nafasi za uwaziri alizozishikilia. Kama namna nzuri ya kujaribu kutafakari utendaji wake, tujikumbushe kidogo alikopitia lowassa.

1. Mwanzoni mwa miaka ya 90 lowassa alikuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, akishughulikia majanga, na itakumbukwa kwamba huu ndiyo wakati ambao mikoa ya kusini na hasa mtwara walikumbwa na mafuriko yaliyoteketeza maisha ya watu pamoja na mali zao na baadhi ya athari hizo bado hazijarekebishwa. Akiwa ndiye mhusika mkuu, lowassa aliratibu upatikanaji na utoaji wa misaada na inasemekana alijinufaisha yeye binafsi kutokana na janga hilo kwani mingi ya misaada haikuwafikia walengwa.

2. Baada ya kutoka hapo, lowassa alipelekwa wizara ya ardhi na ni katika kipindi hiki ndipo tulishuhudia kilele cha migogoro ya ardhi (double allocations) maeneo ya mbezi beach, na hata kuporwa kwa maeneo ya wazi na kuyatolea hati, hasa maeneo ya masaki, msasani peninsular na oysterbay, katika mazingira ambayo yanaashiria kwamba kulikuwa na vichocheo vya rushwa. Ni katika kipindi hiki ndipo rushwa ilipokithiri wizarani na yeye mwenyewe kujilimbikizia viwanja, majumba na utajiri ambao ulikuja kuhojiwa na mwalimu mwaka 1995 alipogombea nafasi ya kugombea urais. Ndicho kipindi cha kushamiri kwa wahindi kama fida hussein na baghdad katika kupora viwanja na inasemekana baghdad alikuwa na viwanja 100 dar peke yake. Hadi leo serikali inahangaika kufanya revocation ya hati alizozitoa lowassa katika mazingira ya utata.

3. Wizara ya maji na mifugo. Shida ya maji jijini dar es salaam iliongezeka na mtandao wa maji nchini uliendelea kuwa duni na kushindwa kusogea kwenye malengo ya serikali ya maji safi kwa kila mtanzania kufikia 2015. Ndicho kipindi cha utapeli wa dawasco na wawekezaji wa bi-water baada ya kuona karibu atashtukiwa aliwafurusha na kuzua kesi iliyoigharimu serikali mabilioni katika kuiendesha. Alizunguka nchi nzima na kuhimiza wananchi wajenge wabanda ya ng'ombe, akiahidi kukopesha ng'ombe ili wananchi walipe ng'ombe. Mabanda haya sas yamegeuka maghala baada ya miaka inayokaribia 10 ya kusubiri. Hali ya soko la wanyama wetu ilibaki kuwa isiyo na ufumbuzi, licha ya yeye kutoka katika jamii ya wafugaji.

4. Ofisi ya waziri mkuu. Zaidi ya kututwisha mzigo wa richmond, na kudandia hoja ya sekondari za kata iliyoasisiwa na utawala wa mkapa, hakuna la kujivunia zaidi ya kukemea na kudhalilisha wafanyakazi wa chini yake. Aliendesha vikao vya kujadili bei za mazao na kuwaita wakuu wa mikoa na wilaya lakini hakuna ufumbuzi wa maana aliokuja nao kuhusu bei za mazao yetu kama pamba, korosho, kahawa, chai na pareto.

Mimi nawasilisha maoni kwamba utumishi wa lowassa umegubikwa na kukosa uadilifu na kushindwa kuleta tija inayohitajika kwa watanzania. Hoja za kwamba alikuwa mchapakazi ni porojo tu za kudhani zitaficha maovu ya ufisadi wake.

dowans,richmond,nam,bumako insurance,wakara wa meli,vodacom(wameingia mkataba na tra baada ya kuindoa kampuni ya umma ttcl kiusainii) etc

KUWE NA UTAMADUNI WA KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA, MTOA MADA HAUNA MADA HAPO NI MAJUNGU MATUPU. weka mambo ubaoni watu waelewe, naona unamchukia EL bila hata kujua, usidandie train mbele. Huyu jamaa ni kiongozi unabisha? Halafu mtafute muadilifu kwa vigezo vyako umuweke jamvini kwa vigezo vyako tumchambue. Napenda mabadiliko ya dhati sio fitna. Umeshawahi kumsikia Slaa akimchambua huyu jamaa kwa undani na ufisadi wake? Ana akili, tulia utajua tu.
Yuko kwenye orodha ya mafisadi wa Slaa, yupo kwenye kashfa ya richmond na walitumia fedha za EPA kumnadi JK 2005.Je hizo ni sifa za kiongozi mzuri hatakama mnakunywa nae kahawa?

SERIKALI INAYOKIKUMBATIA MATAJIRI,HAIWEZI KUWAKEMEA.
Na ukitaka kulijua hili tuangalie nani wa kumnyooshea kidole lowassa

Yaani mmejipanga kumpiga vijembe Lowassa mjue huyo ndiye rais wenu come 2015 ije mvua lije jua.
Hata aende Israeli mara1,000 Urais atausikia tuu.Kama anautaka Urais wa Tz amfufue Baba wa Taifa ili amsafishe, angekuwa msikivu angeachana na ndoto hizo kwani ameshalaanika.

Alilazimisha uwaziri mkuu yuko wapi, Ubunge wenyewe anaununua kwa Ndugu zetu Wamasai wenye elimum duni, Wamasai nao wanazidi kuelimika watajua tuu ukweli.

Kuna mengi zaidi hayo..waliowahi kufanya naye kazi wanasema he is greedy, rude and selfish. Mtu wa namna hii hafai kabisa kuwa kiongozi. Kuna kampuni zinaitwa alfa...from what I here everything that starts with the word alfa has something to do with him kupitia kwa mgongo wa mtoto wake fred. Ana radio 5 FM na hivi karibuni atafungua ABC TV nchi nzima. Mtumishi wa serikali kapata wapi uwezo wa kuinvest to this extent? Hatufai hata kidogo.

ni bora anayeinvest nymbani kuliko anayepeleka ugenini..

SERIKALI INAYOKIKUMBATIA MATAJIRI,HAIWEZI KUWAKEMEA.

Na ukitaka kulijua hili tuangalie nani wa kumnyooshea kidole lowassa

sio hilo tu mkuu na sasa hivi kuna members wanamsafisha EL ni balaa na hii thread ni moja ya watu wanaomsafisha huyu jamaa:cool:

Ni tajiri ambaye utajiri wake umetokana na nafasi alizowahi kushika serikalini
Ana bahati tu kwamba hakuna utawala wa sheria tz,badala ya kufikiria urais angekuwa anaendelea na mashitaka dhidi kujipatia mali kinyume na sheria

Huyu jamaa inaonekana hajui kabisa hicho alichokiandika!hivi wewe ni mkimbizi eeh?itakuwa umetokea Libya ivi majuzi ndo maana hujui mazuri aliyotenda huyo jamaa!Lowasa ni nondo anajua siasa pia ni mchapa kazi kwa maisha yake yakawaida na serikali ndo sababu ana pesa nyingi,we ng'aa macho utakufa na umasikini wako,jamaa elimu yake inambeba ana akili nyingi!usimsingizie mambo yako ya kinafiki!

Duh! Kumbe huu ndio uchapakazi ambao Sofia Simba alikuwa akimsemea Lowassa! Basi nimeamini kuwa uwezo na upeo wa Sofia Simba katika kutafakari na kuchanganua hoja, imenifanya niamini kuwa aliposema ''wanawake wawanyime ngono waume zao kama sio wafuasi wa ccm'' hakukosea bali ilikuwa mwisho wake wa kufikiri!

ukweli unabaki pale pale jamaa hafai tunakubali kuna mazuri kafanya lakini baya moja tu linauwezo wa kufuta mazuri yote ndio maana hata marehemu Baba wa taifa alisha muona anadosari.

Jamani kama kuchagua nani raisi kati ya JK na EL ningemchagua El seriously!

Unajua mashine kubwa ziko nyingi i.e Lister Peter. Robbin. Yanmar n.k. Ila ujue hata kuchukua wake za watu au wizi waweza kuwa mashine kubwa. Wewe ni Mtanzania kweli weye au ulitumwa kuleta vipuri vya mitambo ya Richmond? Au ndo Mangusutu buthelezi enzi za apartheid bondeni?

Back
Top Bottom