Hii ndiyo rekodi ya uchapakazi wa Lowassa

4 lowas?nani ampe?kizazi iki cha sasa au? mana sisi ni kizazi cha epaaaaaaaaaaaaaaaaaaaais 2015a no comment mbadhilifu mkubwa wa mali za uma eti anajiandaaa na urais hapati na asijekujiumbua<br>
 
Tanzania kwa ilivyo sasa inataka mchapakazi hata kama awe dikteta kwa miaka miwili tu akili itukae vizuri hatutaki PM bongo lala wa kulia lia kila kitu namsubiri rais aje wakati yeye ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za serikali.

Lowassa for Chairman
 
Bora lowasa kuliko pinda,i will vote 4 lowasa come 2015

Hakika hukatazwi kumpigia kura maana hiyo ndiyo hasa maana ya demokrasia. Swala hapa siyo kuchagulika kwake maana fedha zinaweza kununua watu wa aina yako. Suala hapa ni kama rekodi yake ya uchapakazi kama tulivyoonyeshwa ina taswira na tafsiri tuliyokuwa tunaambiwa kule nyuma.
 
Kinachonifurahisha ni kamba wale wanaomuunga mkono wamejikita zaidi katika kusema kwamba watamchagua kuwa rais hapo atakapogombea, au kujaribu kuwalinganisha na Pinda.

Suala hapa siyo ulinganifu maana kama ni hivyo kwa nini wasilinganishwe na mawaziri wakuu waliomtangulia kama Sokoine au Warioba ua hata Mzee Kawawa na Mwalimu?

Angalau leo kumejitokeza mtu wa kutusaidia kutukumbushe maeneo ya udhaifu wake ambayo yalifichwa au kujificha.
 
Tanzania kwa ilivyo sasa inataka mchapakazi hata kama awe dikteta kwa miaka miwili tu akili itukae vizuri hatutaki PM bongo lala wa kulia lia kila kitu namsubiri rais aje wakati yeye ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za serikali.

Nakubaliana na wewe kwamba anahitajika mtu mwenye kuthubutu kutenda mema kwa maslahi ya watanzania. Awe ni mtu ambaye wanaweza kumuamini kama msimamizi wa rasilimali na hazina zao. Kwa maelezo ya mtoa thread, Lowassa hana uthubutu wala uadilifu wa kutufanya tumfikirie kwa dhamana hiyo. Tunachokiona kwa watetezi wake ni kushindwa kwao kutueleza alifikaje hapo alipo kiutajiri maana hatujui kama alichukua mikopo kwenye mabenki na pengine wao ndo waturidhishe katika hilo. Lakini tunajua kwamba alihujumu mali za Taifa hili kupitia nafasi alizoshikilia katika uongozi wa nchi.
 
4 lowas?nani ampe?kizazi iki cha sasa au? mana sisi ni kizazi cha epaaaaaaaaaaaaaaaaaaaais 2015a no comment mbadhilifu mkubwa wa mali za uma eti anajiandaaa na urais hapati na asijekujiumbua<br>

Anao waumini wake wanaomsujudia na kumdanganya kwamba fedha zake zitanunua kila kitu ikiwemo heshima.

Ndo maana unaona akina Guninita, Mgeja, Mahanga, Serukamba na waumini wengine wa dhehebu hili wanahangaika kutaka kumpiga deki ilai auzike. Lakini wameshachelewa, jamaa ni kunguru, hafugiki.
 
Hilo mkuu naliunga mkono,mzee huyu ni mtata sana kwenye utendaji wake.

Kusema mtata ni understatement. Tuanishi na jambazi ambalo halistahili kuhusishwa nalo na nchi hii itageuka kichekesho hata kumfikiria tu kwa nafasi yoyote.
 
Haya unayoandika ni upumbavu tu na wivu...we unashinda internet kumtukana Lowassa wakati yeye na wanaye wanafanya kazi za kuzalisha na kuimarisha kipato cha familia yao,hamwezi kulingana...WANA AKILI KULIKO WEWE!

Mbona wewe unashinda kwenye keyboard kujipendekeza kwa familia ya Lowassa, unajuaje kama hao kina lowassa wana akili kuliko reformer, kwangu mimi mtu anayejipatia kipato kwa njia za kifisadi hana maana.
 
Wana JF, kwa muda mrefu kumekuwa na maelezo yanayokinzana, hasa kuhusiana na uadilifu na uwezo wa uchapakazi wa Lowassa kwa kipindi cha utumishi wake kwa nchi hii, na hasa katika nafasi za uwaziri alizozishikilia. Kama namna nzuri ya kujaribu kutafakari utendaji wake, tujikumbushe kidogo alikopitia Lowassa.

1. Mwanzoni mwa miaka ya 90 Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulikia majanga, na itakumbukwa kwamba huu ndiyo wakati ambao mikoa ya kusini na hasa Mtwara walikumbwa na mafuriko yaliyoteketeza maisha ya watu pamoja na mali zao na baadhi ya athari hizo bado hazijarekebishwa. Akiwa ndiye mhusika mkuu, Lowassa aliratibu upatikanaji na utoaji wa misaada na inasemekana alijinufaisha yeye binafsi kutokana na janga hilo kwani mingi ya misaada haikuwafikia walengwa.

2. Baada ya kutoka hapo, Lowassa alipelekwa Wizara ya Ardhi na ni katika kipindi hiki ndipo tulishuhudia kilele cha migogoro ya ardhi (double allocations) maeneo ya Mbezi Beach, na hata kuporwa kwa maeneo ya wazi na kuyatolea hati, hasa maeneo ya Masaki, Msasani Peninsular na Oysterbay, katika mazingira ambayo yanaashiria kwamba kulikuwa na vichocheo vya rushwa. Ni katika kipindi hiki ndipo rushwa ilipokithiri wizarani na yeye mwenyewe kujilimbikizia viwanja, majumba na utajiri ambao ulikuja kuhojiwa na Mwalimu mwaka 1995 alipogombea nafasi ya kugombea urais. Ndicho kipindi cha kushamiri kwa wahindi kama Fida Hussein na Baghdad katika kupora viwanja na inasemekana Baghdad alikuwa na viwanja 100 Dar peke yake. Hadi leo serikali inahangaika kufanya revocation ya hati alizozitoa Lowassa katika mazingira ya utata.

3. Wizara ya Maji na Mifugo. Shida ya maji jijini Dar es Salaam iliongezeka na mtandao wa maji nchini uliendelea kuwa duni na kushindwa kusogea kwenye malengo ya serikali ya maji safi kwa kila mtanzania kufikia 2015. Ndicho kipindi cha utapeli wa Dawasco na wawekezaji wa Bi-Water baada ya kuona karibu atashtukiwa aliwafurusha na kuzua kesi iliyoigharimu serikali mabilioni katika kuiendesha. Alizunguka nchi nzima na kuhimiza wananchi wajenge wabanda ya ng'ombe, akiahidi kukopesha ng'ombe ili wananchi walipe ng'ombe. Mabanda haya sas yamegeuka maghala baada ya miaka inayokaribia 10 ya kusubiri. Hali ya soko la wanyama wetu ilibaki kuwa isiyo na ufumbuzi, licha ya yeye kutoka katika jamii ya wafugaji.

4. Ofisi ya Waziri Mkuu. Zaidi ya kututwisha mzigo wa Richmond, na kudandia hoja ya sekondari za kata iliyoasisiwa na utawala wa Mkapa, hakuna la kujivunia zaidi ya kukemea na kudhalilisha wafanyakazi wa chini yake. Aliendesha vikao vya kujadili bei za mazao na kuwaita wakuu wa mikoa na wilaya lakini hakuna ufumbuzi wa maana aliokuja nao kuhusu bei za mazao yetu kama pamba, korosho, kahawa, chai na pareto.

Mimi nawasilisha maoni kwamba utumishi wa Lowassa umegubikwa na kukosa uadilifu na kushindwa kuleta tija inayohitajika kwa watanzania. Hoja za kwamba alikuwa mchapakazi ni porojo tu za kudhani zitaficha maovu ya ufisadi wake.

Tuseme nini zaidi ya ahsante kwa kutuwezesha watanzania kumjua vema mwizi wetu. Hivi bado kuna utata kuhusu kiumbe huyu na hatari yake kwa Taifa?

Labda uwe na kichwa kama cha Brother John Guninita ambaye tumbo lake limeunganishwa kwa mrija mpaka kwa Lowassa. Kwake yeye Lowassa ni Dripu!
 
Mbona wewe unashinda kwenye keyboard kujipendekeza kwa familia ya Lowassa, unajuaje kama hao kina lowassa wana akili kuliko Lowassa reformer, kwangu mimi mtu anayejipatia kipato kwa njia za kifisadi hana maana.

Tena kujipendekeza kwa kijinga mpaka anadiriki kusema wana akili, eti kwa sababu tu wame-perfect art ya kuiba na kudhulumu. Shame on him!
 
Tuseme nini zaidi ya ahsante kwa kutuwezesha watanzania kumjua vema mwizi wetu. Hivi bado kuna utata kuhusu kiumbe huyu na hatari yake kwa Taifa? Labda uwe na kichwa kama cha Brother John Guninita ambaye tumbo lake limeunganishwa kwa mrija mpaka kwa Lowassa. Kwake yeye Lowassa ni Dripu!
u

Hizi mbio za Uraisi 2015 zitatuumiza...yaani kama nilivootea nilijua tu Mbopo ataunga mkono hoja. Duuh! BM kweli nae hayuko nyuma, wapiganaji wake wako vitani.
 
Hakika hukatazwi kumpigia kura maana hiyo ndiyo hasa maana ya demokrasia. Swala hapa siyo kuchagulika kwake maana fedha zinaweza kununua watu wa aina yako. Suala hapa ni kama rekodi yake ya uchapakazi kama tulivyoonyeshwa ina taswira na tafsiri tuliyokuwa tunaambiwa kule nyuma.
Tupe wewe rekodi ya mchapakazi ndani ya CCM unayemfahamu zaidi ya Lowassa

Lowassa for Chairman
 
u

Hizi mbio za Uraisi 2015 zitatuumiza...yaani kama nilivootea nilijua tu Mbopo ataunga mkono hoja. Duuh! BM kweli nae hayuko nyuma, wapiganaji wake wako vitani.

This is how you cheapen and trivialise critical issues of integrity by associating them with the coming elections. If any of you has balls he shoud come forward with issues that will make sense and vindicate Lowassa.

No body will feel intimidated and desist from airing his views merely because a section of people are so myopic as not to realise how dangerous Lowassa is to our plight as a Nation. Call us anything but let truth be told!
 
Kinachonifurahisha ni kamba wale wanaomuunga mkono wamejikita zaidi katika kusema kwamba watamchagua kuwa rais hapo atakapogombea, au kujaribu kuwalinganisha na Pinda. Suala hapa siyo ulinganifu maana kama ni hivyo kwa nini wasilinganishwe na mawaziri wakuu waliomtangulia kama Sokoine au Warioba ua hata Mzee Kawawa na Mwalimu? Angalau leo kumejitokeza mtu wa kutusaidia kutukumbushe maeneo ya udhaifu wake ambayo yalifichwa au kujificha.
Kwani Sokoine anagombea nini? tunalinganisha watu walio kwenye uongozi kwa wakati huu you can't vote the dead.

Lowassa for Chairman
 
Tupe wewe rekodi ya mchapakazi ndani ya CCM unayemfahamu zaidi ya Lowassa

Lowassa for Chairman

No body is in the business of making comparisons. The thread has achieved the objective of letting us know what was not sufficiently put in perspective.
 
Nakubaliana na wewe kwamba anahitajika mtu mwenye kuthubutu kutenda mema kwa maslahi ya watanzania. Awe ni mtu ambaye wanaweza kumuamini kama msimamizi wa rasilimali na hazina zao. Kwa maelezo ya mtoa thread, Lowassa hana uthubutu wala uadilifu wa kutufanya tumfikirie kwa dhamana hiyo. Tunachokiona kwa watetezi wake ni kushindwa kwao kutueleza alifikaje hapo alipo kiutajiri maana hatujui kama alichukua mikopo kwenye mabenki na pengine wao ndo waturidhishe katika hilo. Lakini tunajua kwamba alihujumu mali za Taifa hili kupitia nafasi alizoshikilia katika uongozi wa nchi.
Kabla ya sisi kuwaambia aliupataje utajiri kwanza tuambieni kwa nini asiwe tajiri.

Lowassa for Chairman
 
Haya unayoandika ni upumbavu tu na wivu...we unashinda internet kumtukana Lowassa wakati yeye na wanaye wanafanya kazi za kuzalisha na kuimarisha kipato cha familia yao,hamwezi kulingana...WANA AKILI KULIKO WEWE!
<br />
<br />
naweza kukuunga mkono, wana akili kutuzidi ila ni akili za wizi, wanawaza dhuluma, kibaya zaidi wanafikiri tunawahitaji watuongoze!! ni heri wangekimbizana na mali, uongozi itawagharimu, kawaambie.
 
Tena kujipendekeza kwa kijinga mpaka anadiriki kusema wana akili, eti kwa sababu tu wame-perfect art ya kuiba na kudhulumu. Shame on him!

Ndo ushangae, CCM wenyewe wanataka avuke maana ni gamba lakini mshikaji amekufa ameoza haambiwi kitu kwa kina lowassa kazi tunayo
 
Back
Top Bottom