Hii ndiyo rekodi ya uchapakazi wa Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndiyo rekodi ya uchapakazi wa Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mudavadi, Aug 3, 2011.

 1. m

  mudavadi Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF, kwa muda mrefu kumekuwa na maelezo yanayokinzana, hasa kuhusiana na uadilifu na uwezo wa uchapakazi wa Lowassa kwa kipindi cha utumishi wake kwa nchi hii, na hasa katika nafasi za uwaziri alizozishikilia. Kama namna nzuri ya kujaribu kutafakari utendaji wake, tujikumbushe kidogo alikopitia Lowassa.

  1. Mwanzoni mwa miaka ya 90 Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulikia majanga, na itakumbukwa kwamba huu ndiyo wakati ambao mikoa ya kusini na hasa Mtwara walikumbwa na mafuriko yaliyoteketeza maisha ya watu pamoja na mali zao na baadhi ya athari hizo bado hazijarekebishwa. Akiwa ndiye mhusika mkuu, Lowassa aliratibu upatikanaji na utoaji wa misaada na inasemekana alijinufaisha yeye binafsi kutokana na janga hilo kwani mingi ya misaada haikuwafikia walengwa.

  2. Baada ya kutoka hapo, Lowassa alipelekwa Wizara ya Ardhi na ni katika kipindi hiki ndipo tulishuhudia kilele cha migogoro ya ardhi (double allocations) maeneo ya Mbezi Beach, na hata kuporwa kwa maeneo ya wazi na kuyatolea hati, hasa maeneo ya Masaki, Msasani Peninsular na Oysterbay, katika mazingira ambayo yanaashiria kwamba kulikuwa na vichocheo vya rushwa. Ni katika kipindi hiki ndipo rushwa ilipokithiri wizarani na yeye mwenyewe kujilimbikizia viwanja, majumba na utajiri ambao ulikuja kuhojiwa na Mwalimu mwaka 1995 alipogombea nafasi ya kugombea urais. Ndicho kipindi cha kushamiri kwa wahindi kama Fida Hussein na Baghdad katika kupora viwanja na inasemekana Baghdad alikuwa na viwanja 100 Dar peke yake. Hadi leo serikali inahangaika kufanya revocation ya hati alizozitoa Lowassa katika mazingira ya utata.

  3. Wizara ya Maji na Mifugo. Shida ya maji jijini Dar es Salaam iliongezeka na mtandao wa maji nchini uliendelea kuwa duni na kushindwa kusogea kwenye malengo ya serikali ya maji safi kwa kila mtanzania kufikia 2015. Ndicho kipindi cha utapeli wa Dawasco na wawekezaji wa Bi-Water baada ya kuona karibu atashtukiwa aliwafurusha na kuzua kesi iliyoigharimu serikali mabilioni katika kuiendesha. Alizunguka nchi nzima na kuhimiza wananchi wajenge wabanda ya ng'ombe, akiahidi kukopesha ng'ombe ili wananchi walipe ng'ombe. Mabanda haya sas yamegeuka maghala baada ya miaka inayokaribia 10 ya kusubiri. Hali ya soko la wanyama wetu ilibaki kuwa isiyo na ufumbuzi, licha ya yeye kutoka katika jamii ya wafugaji.

  4. Ofisi ya Waziri Mkuu. Zaidi ya kututwisha mzigo wa Richmond, na kudandia hoja ya sekondari za kata iliyoasisiwa na utawala wa Mkapa, hakuna la kujivunia zaidi ya kukemea na kudhalilisha wafanyakazi wa chini yake. Aliendesha vikao vya kujadili bei za mazao na kuwaita wakuu wa mikoa na wilaya lakini hakuna ufumbuzi wa maana aliokuja nao kuhusu bei za mazao yetu kama pamba, korosho, kahawa, chai na pareto.

  Mimi nawasilisha maoni kwamba utumishi wa Lowassa umegubikwa na kukosa uadilifu na kushindwa kuleta tija inayohitajika kwa watanzania. Hoja za kwamba alikuwa mchapakazi ni porojo tu za kudhani zitaficha maovu ya ufisadi wake.
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  Hilo mkuu naliunga mkono,mzee huyu ni mtata sana kwenye utendaji wake.
   
 3. k

  kibajaj Senior Member

  #3
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anaikopesha ccm huyu kwa wizi wake ndo mana wanaogopa kumfukuza
   
 4. r

  reformer JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna mengi zaidi hayo..waliowahi kufanya naye kazi wanasema he is greedy, rude and selfish. Mtu wa namna hii hafai kabisa kuwa kiongozi. Kuna kampuni zinaitwa alfa...from what I here everything that starts with the word alfa has something to do with him kupitia kwa mgongo wa mtoto wake fred. Ana radio 5 FM na hivi karibuni atafungua ABC TV nchi nzima. Mtumishi wa serikali kapata wapi uwezo wa kuinvest to this extent? Hatufai hata kidogo.
   
 5. g

  gingamtima New Member

  #5
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi natofautiana kabisa na wewe.Inaonekana uendaji mzuri wa huyu mzee umeudharau au hukuwa katika nchi hii wakati anafanya nazuri
   
 6. g

  gingamtima New Member

  #6
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ana mazuri mengi kuliko mabaya,inaonekana huyu bwana humjui kabisa!Kifupi,huyu mzee ni mashine kubwa.
   
 7. r

  reformer JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tueleze mazuri yake, na mabaya yake, sababu umekiri mwenyewe anayo yote. Acha kubwabwaja tu. Hatuwezi kuwa na viongozi who take too much and give us very little. Baya 1 linatosha kumhukumu mtu.
   
 8. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,315
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Wakati watu tunahangaika na njaa tupu, mwenzetu huyu juzi katoa sadaka ya Mil13 Bakwata. Tz ni zaidi ya uijuavyo bwana.
   
 9. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,680
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  @gingamtima, ni hakuna anayebisha kama unavielelezo kuhusu utendaji mzuri wa lowasa tupe mezani.
   
 10. m

  mwanza JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 508
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Ni mwonevu aliyetuingizia hasara ya shilingi billioni 8 kwa kuamuru kuvunjwa yale majengo karibu na seacliff akishirikiana na mama nagu
   
 11. G

  Ginila Nyeura Member

  #11
  Aug 3, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ninasema huyu bwana ni mwizi, kama vipi, kwenye marekebisho ya katiba tuondoe kinga ya viongazi kushtakiwa ili tuwe huru kudeal na viongozi wezi wote baada ya kipindi chao cha uongozi.
   
 12. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Yaani mmejipanga kumpiga vijembe Lowassa mjue huyo ndiye rais wenu come 2015 ije mvua lije jua.
   
 13. Ungana

  Ungana JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya unayoandika ni upumbavu tu na wivu...we unashinda internet kumtukana Lowassa wakati yeye na wanaye wanafanya kazi za kuzalisha na kuimarisha kipato cha familia yao,hamwezi kulingana...WANA AKILI KULIKO WEWE!
   
 14. M

  Mwana Mpole New Member

  #14
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoja na uchafu wote huo....yeye anabaki kuwa Bora kuliko Pinda.
   
 15. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Asante kwa taarifa, lakini mhhhh...
   
 16. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Bwana mukubwa uko sahihi.
  Wacha wale wezi wenziwe wampigie debe.
  Huyu hana historia ya uadilifu kama viongozi wengine, aidha utajiri wake umetokana na siasa hasa alipokuwa Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Rais-Kushughulikia Maafa. Hapo ndio alikomba pesa za maafa kwa kwenda mbele .Uliza mtu yeyote pale juu ya Maziwa ya maafa miaka ya El Nino.
  Tusishabikie mtu kwa maslahi binafsi, bali ya kitaifa-hata Mwalimu alinote hili kuwa huyu kijana alianza kazi hana kitu sasa hiivi anautajiri, kaupata wapi?
  Vile vile Wizara ya Ardhi alipora hadi viwanja vya makanisa-laana inayomwandama.
  Ni vyema akajiimarisha katika shughuli anayoipenda-kutengeneza noti , na si siasa.
  Historia itamhukumu.
   
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Agree with u, ana power ya uongozi.
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  So what........
   
 19. mjanja

  mjanja Member

  #19
  Aug 3, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  4 lowas?nani ampe?kizazi iki cha sasa au? mana sisi ni kizazi cha epaaaaaaaaaaaaaaaaaaaais 2015a no comment mbadhilifu mkubwa wa mali za uma eti anajiandaaa na urais hapati na asijekujiumbua
   
 20. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pinda je? and ukiwa compare bora nani?
   
Loading...