Mimi huwa nashangaa tunaposema kama kusingekuwa na wanunuzi hawa wanaojiuza wasingekuwepo. Unajua vice versa is true. Kama hakuna hao wanaojiuza pia kusingekuwa na wanunuzi. Unaweza kwenda kwenye banda la ng'ombe kununua mayai? Tatizo hapa tunaangaliana sisi wanadamu kwa wanadamu na kuhukumiana tukaacha kumwangalia shetani ambaye ndiye anayekamata watu na kuwafanya watumwa wake na hivyo kuwatumia kama apendavyo mwenyewe.
Naamini wengi tumetembea katika nchi mbalimbali na katika mitandao mbalimbali. Tuwe wakweli, suala la ukahaba, umalaya au jina lolote tunaloweza kuita, liko Tanzania tu kwa sababu ya umaskini? Je wanaotumia madawa ya kulevya wengi wao ni watoto wa maskini? Hakuna kundi la watu hawa katika nchi kama Marekani, Uingereza, Ufaransa nk? Mbona ni nchi zilizoendelea na kuwa na utajiri mkubwa tuuu!!!!!!!!!!!!! Tusikwepe wajibu kwa kusingizia mambo yanayobeba asilimia ndogo sana ya ukweli juu ya tatizo hili tukaacha ukweli wa tatizo lenyewe.
Sio kwamba nakataa ukweli kwamba umaskini unaweza kusababisha tatizo hili au matatizo katika ndoa, ninachosema adui yetu nambari one ni shetani kwani wako wasichana wengi sana wanaotoka katika familia duni sana inawezekana hata kushinda hao wanaojiuza lakini wanapambana na maisha mpaka wanavuka bila kuwa malaya. Lakini hao ambao wanapenda maisha rahisi kwa kisingizio cha maisha magumu ndio wanaofanya haya. Wako wasichana ambao ni wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanafanya ukahaba na unakuta wanatoka katika familia ambazo zina uwezo mzuri tu, na hawa tusemeje?
Kuna mahali wazazi wameshindwa kusimama katika nafasi zao kama wazazi na kufikiri kila jambo mtoto analotaka hata kama lina madhara kwa maisha yake ya baadaye ni lazima apewe na kwa sehemu kubwa utandawazi umehusika kwa kiasi kikubwa kuharibu watoto. Waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi akishakauka atavunjika. Ndio sababu ninasema kazi kubwa iliyoko sasa ni kumwomba Mungu aingilie kati.
Nawashauri wazazi tuwe karibu na watoto wetu, hata katika hali ngumu tuongee nao tushirikiane katika kutatua matatizo ya familia zetu, tuache ukali usio na sababu hasa hali ya uchumi inapokuwa ngumu; lakini kikubwa sana tuwafundishe watoto kumjua na kumpenda Mungu. Katika mazingira tulio nayo sasa na mitandao inayotuzunguka, bila Mungu hatuwezi.
Na sisi sote tusishabikie hawa mabinti kuharibika tuwaombee sana Mungu anaweza kuwabadilisha wakawa tena mabinti wazuri, tegemeo kwa familia na taifa letu. Mungu uwahurumie sana mabinti hawa.