MrFroasty
JF-Expert Member
- Jun 23, 2009
- 1,195
- 590
nb: Kwa kuweka katiba hii haina maana ninakiunga mkono chama hiki au kukubaliana nacho au kukipendekeza kwa wananchi kwa wakati huu. m.m
katiba
ya
chama cha jamii
(ccj)
utangulizi
- kwa kuwa mapambano ya kuleta uhuru wa nchi yetu yalikuwa na lengo kuu la kumwondoa mwananchi kutoka kwenye unyonge wa kunyonywa, kunyanyaswa na kudharauliwa na wakoloni, ambao ni ukombozi wa mwananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii; na
- kwa kuwa uhuru tulioupata ulitupa fursa ya kujenga nchi na taifa lenye kubeba matumaini ya wananchi wote kwa ujumla kwa kuweka misingi imara ya kuheshimu na kuzingatia usawa wa binadamu, utawala bora, utawala wa sheria, haki za binadamu, hifadhi na ustawi kwa wananchi wote na utaifa wetu; na
- kwa kuwa ukombozi kamili wa mwananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii unahitaji juhudi, maarifa, moyo wa kujituma na ujasiri wa kuthubutu kwa upande wa viongozi, vipaji ambavyo bado kuviona vikitumika nchini; na
- kwa kuwa nchi yetu imedhamiria kikatiba kuthamini na kuzingatia uhuru wa mahakama katika utoaji haki bila woga wala upendeleo, na uhuru wa bunge lenye madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake katika utekelezaji wa shughuli za umma; na
- kwa kuwa tanzania inao utajiri wa kutosha wa rasilimali unaoweza kuleta maendeleo ya haraka ya nchi kiuchumi na kuleta mabadiliko makubwa ya maisha kwa kila mwananchi ikiwa ombwe la uongozi litashughulikiwa; na
- kwa kuwa matumizi bora na endelevu ya utajiri wa rasilimali yanawezekana tu katika taifa ambalo lina uongozi wenye uchungu na nchi na unaozingatia maadili kama yalivyoainishwa na kusimamiwa kidete na baba wa taifa, mwalimu julius nyerere; taifa ambalo linawaandaa vijana wake vizuri kielimu na kimaadili; ambalo wanawake wana fursa sawa na wanaume; na ambalo mchango wa kila raia awe kijana, mzee, mlemavu n.k unatambuliwa na kuthaminiwa; na
- kwa kuwa elimu ni moja ya misingi ya maendeleo ya taifa lolote lile, msingi ambao baba wa taifa mwalimu j. K. Nyerere aliutumia kujenga taifa jipya lenye matumaini, nchi yetu haina budi kuendeleza utaratibu wa serikali kugharamia elimu ya wananchi wake; na
- kwa kuwa adui mkubwa wa haki na maendeleo ni ufisadi, yaani rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na uporaji wa rasilmali za taifa, adui ambaye hana budi kupigwa vita kwa nguvu zote na
kwa kuwa tanzania ni nchi iliyodhamiria kikatiba kufuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi; na
- kwa kuwa muungano wa tanzania bara na tanzania zanzibar nim ushahidi hai unabeba matumaini mahususi ya kuziunganisha nchi za kiafrika kuwa moja katika kukabiliana na changamoto za utandawazi; na
- kwa kuwa lengo kuu la mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ni kujenga na kuimarisha nguvu za umma na uwezo wa wananchi mmoja mmoja na kwa pamoja katika kubadilisha mazingira ya nchi yao na maisha wanayoishi; na
- kwa kuwa lengo hili kuu la kujenga na kuimarisha nguvu za umma na uwezo wa wananchi linawezekana tu ikiwa wananchi wataungana na kuongozwa na chama cha siasa imara kisichoyumba kwenye masuala ya msingi, chama chenye itikadi na sera za kimaendeleo, chama kinachoweka hai matarajio ya wananchi baada ya uhuru ya kiuchumi na kijamii, chama kinachopiga vita aina zote za ufisadi kwa kauli na vitendo na chenye msimamo thabiti wa kujali nchi na watu wake kwanza kabla ya maslahi mengine yoyote:
- hivyo basi, sisi wananchi wazalendo tuliokutana hii leo tarehe ... ... ... Jijini dar es salaam kutekeleza wajibu wetu kikatiba wa kuunganisha pamoja mawazo yetu na kuunda chama cha siasa kinachozingatia changamoto zote zinazoikabili nchi yetu tangu baada ya uhuru na kichachobeba matarajio ya wananchi ya leo na kesho, kwa jina la chama cha jamii, kwa kifupi ccj, ambacho lengo lake kuu ni kuleta mageuzi ya kitaifa ya kidemokrasia, kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa faida yetu sote sasa na ya vizazi vijavyo.
Suhala la kujiuliza... "kwa nini kianzishwe miezi michache kabla ya uchaguzi?
NL,UONGOZI 5.Awe na upeo mpana kiakili na kuwa tayari kujiendeleza yeye binafsi kielimu na kutumia elimu aliyoipata kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.
....sifa za kiongozi......naona na huku VIHIYO wanaruhusiwa kugombea.....sioni namna nzuri ya kumpima mtu kwa point namba 5!
Hapa Hakuna kitu kipya zaidi yale yale ya siku zote na wakati ukifika ndio tutaona matokeao yake. Kwanini wasijiunge na vyama vilivyopo??? hapa ndio kuna tatizo kubwaa
Hakuna kitu kipya hapa. Hapa Tanzania kuna utitiri wa vyama hii yote ni janja ya CCM ili kuwagawa watu na kuona hata kama kuanzisha chama kingine ila CCM watafanya ili kushinda na kusema kuwa JK ni Kiboko. Mimi naona ni bora kuingia kwa vyama hivi vilivyopo na kuwapa nguvu zao. Tanzania kuna kama vyama 20 hivi kwa sasa na pia hii ni mbaya sana kwa Taifa kama tanzania. Sijapendezwa na hali ya mambo ya divide na rule kama hiviLabda wameona kuwa vyama vilivyopo vina ubabaishaji/usanii mwingi so wameamua kuja na kitu kipya kukidhi mahitaji yao ya kidemokrasia(Hasa ukizingatia kwamba wanayo haki ya kuanzisha na kujiunga na chama chochote mradi tu wafuate sheria za nchi)
Hakuna kitu kipya hapa. Hapa Tanzania kuna utitiri wa vyama hii yote ni janja ya CCM ili kuwagawa watu na kuona hata kama kuanzisha chama kingine ila CCM watafanya ili kushinda na kusema kuwa JK ni Kiboko. Mimi naona ni bora kuingia kwa vyama hivi vilivyopo na kuwapa nguvu zao. Tanzania kuna kama vyama 20 hivi kwa sasa na pia hii ni mbaya sana kwa Taifa kama tanzania. Sijapendezwa na hali ya mambo ya divide na rule kama hivi