~!~ Hii ndiyo Katiba ya CCJ ~!~ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

~!~ Hii ndiyo Katiba ya CCJ ~!~

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 23, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  NB: kwa kuweka Katiba hii haina maana ninakiunga mkono chama hiki au kukubaliana nacho au kukipendekeza kwa wananchi kwa wakati huu. M.M


  KATIBA
  YA
  CHAMA CHA JAMII
  (CCj)
  Utangulizi


  • Kwa kuwa mapambano ya kuleta uhuru wa nchi yetu yalikuwa na lengo kuu la kumwondoa mwananchi kutoka kwenye unyonge wa kunyonywa, kunyanyaswa na kudharauliwa na wakoloni, ambao ni ukombozi wa mwananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii; na

  • KWA KUWA uhuru tulioupata ulitupa fursa ya kujenga Nchi na Taifa lenye kubeba matumaini ya wananchi wote kwa ujumla kwa kuweka misingi imara ya kuheshimu na kuzingatia usawa wa binadamu, utawala bora, utawala wa sheria, haki za binadamu, hifadhi na ustawi kwa wananchi wote na utaifa wetu; na

  • KWA KUWA ukombozi kamili wa mwananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii unahitaji juhudi, maarifa, moyo wa kujituma na ujasiri wa kuthubutu kwa upande wa viongozi, vipaji ambavyo bado kuviona vikitumika nchini; na

  • KWA KUWA nchi yetu imedhamiria Kikatiba kuthamini na kuzingatia Uhuru wa Mahakama katika utoaji haki bila woga wala upendeleo, na Uhuru wa Bunge lenye madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake katika utekelezaji wa shughuli za umma; na

  • Kwa kuwa Tanzania inao utajiri wa kutosha wa rasilimali unaoweza kuleta maendeleo ya haraka ya nchi kiuchumi na kuleta mabadiliko makubwa ya maisha kwa kila mwananchi ikiwa ombwe la uongozi litashughulikiwa; na

  • KWA KUWA matumizi bora na endelevu ya utajiri wa rasilimali yanawezekana tu katika Taifa ambalo lina uongozi wenye uchungu na nchi na unaozingatia maadili kama yalivyoainishwa na kusimamiwa kidete na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere; Taifa ambalo linawaandaa vijana wake vizuri kielimu na kimaadili; ambalo wanawake wana fursa sawa na wanaume; na ambalo mchango wa kila raia awe kijana, mzee, mlemavu n.k unatambuliwa na kuthaminiwa; na

  • KWA KUWA elimu ni moja ya misingi ya maendeleo ya taifa lolote lile, msingi ambao baba wa taifa mwalimu J. K. Nyerere aliutumia kujenga taifa jipya lenye matumaini, nchi yetu haina budi kuendeleza utaratibu wa serikali kugharamia elimu ya wananchi wake; na

  • Kwa kuwa adui mkubwa wa haki na maendeleo ni UFISADI, yaani rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na uporaji wa rasilmali za Taifa, adui ambaye hana budi kupigwa vita kwa nguvu zote na

  • KWA KUWA Muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar nim ushahidi hai unabeba matumaini mahususi ya kuziunganisha nchi za kiafrika kuwa moja katika kukabiliana na changamoto za utandawazi; na
  KWA KUWA Tanzania ni Nchi iliyodhamiria Kikatiba kufuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi; na

  • Kwa kuwa lengo kuu la mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ni kujenga na kuimarisha nguvu za umma na uwezo wa wananchi mmoja mmoja na kwa pamoja katika kubadilisha mazingira ya Nchi yao na maisha wanayoishi; na

  • Kwa kuwa lengo hili kuu la kujenga na kuimarisha nguvu za umma na uwezo wa wananchi linawezekana tu ikiwa wananchi wataungana na kuongozwa na chama cha siasa imara kisichoyumba kwenye masuala ya msingi, chama chenye itikadi na sera za kimaendeleo, chama kinachoweka hai matarajio ya wananchi baada ya uhuru ya kiuchumi na kijamii, chama kinachopiga vita aina zote za ufisadi kwa kauli na vitendo na chenye msimamo thabiti wa kujali Nchi na watu wake kwanza kabla ya maslahi mengine yoyote:

  • HIVYO BASI, SISI WANANCHI WAZALENDO tuliokutana hii leo tarehe ... ... ... jijini Dar es Salaam kutekeleza wajibu wetu Kikatiba wa kuunganisha pamoja mawazo yetu na kuunda chama cha siasa kinachozingatia changamoto zote zinazoikabili nchi yetu tangu baada ya uhuru na kichachobeba matarajio ya wananchi ya leo na kesho, kwa jina la CHAMA CHA JAMII, kwa kifupi CCJ, ambacho lengo lake kuu ni kuleta mageuzi ya kitaifa ya kidemokrasia, kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa faida yetu sote sasa na ya vizazi vijavyo.


   

  Attached Files:

 2. g

  geek Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukran Mwanakijiji,

  Katiba nzuri, je unaweza kutupatia lineup ya uongozi wa muda wa CCJ?
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mhhh kazi ipo hapa
   
 4. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,294
  Trophy Points: 280
  Thanks Mkuu

  Unayo hii in MS Word/PDF format? - ingekuwa nzuri zaidi na ingesomeka kwa uzuri zaidi.

  Wanakisajiri lini??
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kimeshasajiliwa.. kinasubiri usajili wa kudumu.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi najiandaa kuwa mjumbe wa shina wa chama hiki....mmmh rangi ya kijanai hiyo daaaah
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  I have no clue!
   
 8. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,294
  Trophy Points: 280
  The die is cast! - tusubiri tuone outcome
   
 9. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Je kuna uwezekano wa kumshinikiza msajiri (kisheria) kianze kwenye uchaguzi huu mkuu ujao(Oct 2010). Kama sio kwa nini wamechelewa ili hali wakijua kuwa msajili hatawaruhusu kwenye uchaguzi huu 2010?. Kama sio mbona wameanza kuchemka mapema kama yaliyomkuta Shitambala Mbeya vijijini. Ushauri wangu kama wanajua kuwa kisheria usajiri wa kudumu huchukua miezi sita wangekisajiri 2009 kwa malengo ya January 2010 kuanza kufanya kazi, lakini kwa sasa naamini msajiri atashinikizwa na chama tawala kisianze kutumika uchaguzi huu.
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Jan 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Na kwanini kianzishwe miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa kitaifa!?
   
 11. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,294
  Trophy Points: 280
  What do you think!? - labda kuna kigogo mmoja kutoka CCM anataka ajipenyeze huko na kugombea URAIS!

  Na labda ana kundi la wabunge ambao wanaona wana hali mbaya majimboni kwao au CCM kimewakalia vibaya kutokana na misimamo yao na kinaplan kuwamwaga kwenye kura zao za maoni

  At this stage kutakuwa na assumptions nyingi. Tuwe wavumilivu kidogo tu na muda si mrefu, tutawajua washika dau wenyewe
   
 12. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kwa nini kunakuwa na sajili mbili yani temp halafu ndio wa kudumu?
  kwa nini kusiwe na usajili wa kudumu moja kwa moja?
  je nchi nyingine zinafanyaje katika hili??
  je nia na madhumuni ya usajili wa temp ni nini??

  naomba msaada kwenye hili kama kuna mtu analielewa
   
 13. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  naona wanasisitizia kulipia uana chama, chama kinalipiwa au kinachangiwa na wenye uwezo wa kujitolea. Hila personally im liking all this saga.
   
 14. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hope some type of fisadinising mawazo ya watu is just coming soon
  lets b careful on it
   
 15. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #15
  Jan 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Huwezi kuona kuwa hii ni janja ya kutaka kuwatenganisha Watanzania?
   
 16. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haya ni mazingaombwe tu. Usanii juu ya usanii. Anyway katiba nyingi za vyama zinasomeka na huwa na maneno matamu sana, kazi ni utekelezaji na nia ya wenye vyama.

  Hawa si wa kweli na ni watu hatari sana wa demokrasia na maendeleo ya nchi.

  1. Kama wana nia ya kweli ya kumsaidia mtanzania, kwa nini wasubiri mpaka wapigwe chini na majambazi wenzao ndio wahamishie majina yao CCJ.

  2. Kwa nini wasitoke hadharani na kuweka bayana misimamo yao na nia zao.

  3. Kwa nini leo ndio wajifanyeji wanameguka baada ya kushindana kwenye migawo.

  4. Tanzania itaendelea kuliwa kwa sababu tunapenda siasa rahisi na kuoneana huruma.

  Vyama vya siasa ni vingi mno kuliko mahitaji ya nchi, kazi kubwa ni wanachama na viongozi kubadili siasa za mlipuko na kutimua viongozi vilaza na wasio na maamuzi yenye tija kwa taifa. Swala la kukimbia kila siku kwa nia ya kupewa madaraka au kulinda majimbo ya kisiasa hayasaidii.

  Wananchi wenye nia njema wavipe nguvu vyama ambavyo tayari vinaonyesha uhai, ili kuweza kuleta check and balance, hilo ndilo tunalolikosa Tanzania. Lazima tuwe na vyama viwili au vitatu vyenye nguvu sio vyama mia vyote vizaifu, halafu kimoja chenye nguvu.

  Kuanzishwa kwa hiki chama inaweza kuwa ni janja ya CCM kudhoofisha upinzani.

  Wait and watch eyes on the prize.
   
 17. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  With all due respect, sioni kama watanzani wameungana katika chama chochote cha upinzani,sasa kianzishwe chama ili kiwatatenganishe katika lipi?
   
 18. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Niliposoma katiba hiyo, nimekumbuka katiba ya TANU na CCM wakati huo tukilazimishwa kuzisoma miaka ya 70. Mh!
   
 19. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #19
  Jan 23, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Muundo wa Katiba ni kama wa CCM kabisa !!!!!!!!!!!!!!!!
   
 20. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #20
  Jan 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Suhala la kujiuliza... "kwa nini kianzishwe miezi michache kabla ya uchaguzi?
   
Loading...