hii ndiyo kampuni ya Abdulrahman Kinana

Wacha unafiki na umbea kijana.Source yenyewe hujaweka unapayuka tu mdomo.Na isitoshe pembe za ndovu zilizokamatwa huko zote zimetoka Congo.

na we tuwekee "source" yako inayoonesha hizo pembe zimetoka Congo. Mbona povu limekutoka haraka hivyo bila ya utafiti.
NI KWANINI HATUNA UCHUNGU NA NCHI YETU.????
 
hivi Ritz wakati mnampa kinana wadhifa wa kichama hamkujua uchafu alionao?
Au mliamua liwalo na liwe?
CCM wanadharau sana, wanajua wananchi ni mamburula na hata msipotaka, kwa nguvu ya pesa za kifisadi walitakalo litakuwa tu. Ni ngumu sana kufkiria JK alikuwa anawaza nnkurejesha wezi na mafisadi ktk CC. Ni maoni mangap yametolewa juu ya wezi hawa?? akaona lazma arejeshe hao hao. Je ni kweli hakuna wasafi ccm zaid ya hawa???

Ila mm nasema tumshkuru sana Mungu kwa CCM kufanya hii Grave Mistake na usikute leo kuu la JK ni kuiua CCM mana haiingii akilin kama JK alihusisha ubongo kwenye uteuzi wake. Hivi kwa haya utasema JK na CCM yake watatokomeza rushwa??? au Rushwa ndo itakuwa style ya maisha waliotuchagulia???Maana ya yote haya ni kwamba wananchi ndo wameachwa waimalize rushwa wenyewe kwa style ya wanayoijua wao.

Shime watanzania, tuungane kwa pamoja kuikataa Dharau hii pamoja na rushwa na hili tulionyeshe kwa vitendo katika sanduku la kura 2015. Kamwe tusikubali kuongozwa tena na genge la mafisadi na wahuni ambalo linatudharau siku hadi siku.
 
cdm kila mmoja ni mkuu wa propaganda...hahahahha kwa mtoto aliyezaliwa leo akijiunga na jf anaweza akajua ili uwe mtu safi dunian lazma ujiunge na JF.
Naona mzee kinana huu saa ndio wakati wake wa kuchafuliwa coz ndio ameshapata shavu.
 
na we tuwekee "source" yako inayoonesha hizo pembe zimetoka congo. Mbona povu limekutoka haraka hivyo bila ya utafiti.
Ni kwanini hatuna uchungu na nchi yetu.????


lakini ili tudiscuss mambo yanayoleta uchungu kama haya source ni muhimu mkuu
 
Hizi taarifa wanaozileta ni watu wa CCM, ambao baada ya Kinana kuchaguliwa sasa matumnbo yao joto, na ili kumvunja guts za kupamabana na mafisadi sasa wanasambaza habari hizi ili Kinana akose pa kuanzia.Surely Mungu anampa nguvu na maarifa ya kupambana na watu hao waovu.
 
Sasa wakala wa usafirishaji anasafirisha kontena au vilivyomo kwenye kontena> nenda kasome kuhusu usafirishaji utaelewa.

Wanakamatwa kila siku wauza madawa ya kulevya wakiwa wamyabeba kwenye ndege, hakamatwi mwenye ndege wala wakala aliyemuuzia tiketi anaekamatwa ni mwenye mali.

Kuwa na akili japo kidogo.
 
Wacha unafiki na umbea kijana.Source yenyewe hujaweka unapayuka tu mdomo.Na isitoshe pembe za ndovu zilizokamatwa huko zote zimetoka Congo.
You must be very close to either the investigation team or the smuggling Crüe cause the DNA traits of elephants in this region Congo and TZ is too close to make out your distinctive source of the tasks caught. It smells rats when you take Kinanas origin(being a Somalian), his association with Loliondo and Giraffee smuggling while he was deputy minister of defense and his wealth. I belive that if he will be put under "microscope" there will be theads linking him to the content of the container.
 
Wandugu naomba msome hii taarifa ndio mjue nchi yetu imeoza

KAMPUNI ya uwakala iliyosafirisha kontena lililokuwa na meno ya tembo ambayo yalikamatwa nchini Vietnam, inamilikiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, Abdulrahman Kinana, imefahamika.
Taarifa zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo inayoitwa Sharaf Shipping Company iliyosajiliwa Dar es Salaam.
Mshirika mwenzake katika kampuni hiyo, Rahma Hussen anamiliki hisa 2,500 zenye thamani ya shilingi 1,000 kila moja.
Kwamujibu wa taarifa za usajili, wamiliki wote wawili, Kinana na Rahma wanapatikana kwa S.L.P 10910, Kiwanja Na. 403 Mtaa wa Tosamaganga, Msasani Peninsular, Dar es Salaam.
Nyaraka zilizopo katika ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), zinaonyesha kuwa kampuni ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati Na. 47221.
Sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali zilizosafirishwa na kampuni ya Sharaf Shipping Agency liliibuliwa bungeni kwa mara ya kwanza na mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.
Hati ya kusafirisha makontena hayo mawili yaliyokuwa yamesheheni pembe za ndovu ilisainiwa na mfanyakazi mwenye asili ya India wa kampuni hiyo Samir Hemani.
Nyaraka zote zilionyesha kuwa kilichokuwa ndani ni plastiki zilizorudufiwa, wakati baada ya makontena kukamatwa, walikuta yamesheheni pembe za ndovu.
Taarifa zinasema kibali cha kusafirishwa kontena hilo kilisainiwa 13 Novemba 2008 na Meneja wa Fedha na Utawala wa Kampuni hiyo.
Wakati Hemani anasaini nyaraka hizo, kibali chake cha kuishi nchini tayari kilikuwa kimeshaisha. Kibali cha Hemani kiliisha 7 Mei 2008.
Makontena yalikamtwa nchini China yakisafirishwa kwenda Hong Kong.
Akichangia makadirio ya bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2009/2010, Kilango alisema utafiti wake umeonyesha kuwa makontena hayo yalipitia bandari ya Dar es Salaam na nyaraka zinaonyesha ndani kulikuwa na plastiki.
Kilango alisema nchi zinazoongoza kwa kupokea nyara kutoka Tanzania ni Phillipines, China, Singapore na Hong Kong.
Kutokana na kutopatikana kwa Kinana juzi kuzungumzia suala hilo, haikufahamika iwapo kampuni ya spika huyo wa zamani wa Afrika Mashariki au yeye mwenyewe, walijua kilichokuwamo katika makontena hayo.
Lakini afisa mwandamizi katika wizara ya Viwanda na Biashara alisema kazi ya kukagua kilichomo kwenye kontena linalosafirishwa si ya wakala wa meli kwani wenye mamlaka na idhini ya kufanya hivyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Alisema wanaowajibika kusitisha mzigo kusafirishwa pindi wanapoutilia mashaka ni TRA.
"TRA ndio wanakagua na baada ya kujiridhisha kama kilichomo ndani ndicho kilichotamkwa kwenye nyaraka na ni halali, ndipo wanaweka muhuri (seal) wa mwisho," alisema afisa huyo.
"Ukitamka kwa mfano, kuwa katika nyaraka ndani ya kontena kuna matairi 40 ya magari, lazima TRA wafungue na kukagua kuona kama kweli yako matairi 40 au kitu kingine. Baada ya hapo wanaweka seal; sasa kuna kila sababu ya kujenga mashaka,” alieleza.
Alisema, "Wakala wa meli kazi yake ni kusafirisha mzigo wa mteja wake. Hata mteja akija na kontena tupu na kusema anataka liende nchi fulani, kazi yake ni kulipeleka kunakohusika na si kuhoji kilichomo.”
Alifafanua kuwa watu muhimu wa kuhojiwa na ambao wanaweza kuwa wanajua mchezo wote, kama upo, ni wafanyakazi wa TRA.
Hadi juzi Jumatatu hakukuwa na taarifa zozote za maofisa wa TRA kuhojiwa kuhusiana na sakata hilo
 
ni hao ndi akina 99% ! uchafu+uchafu=? , alafu ni wapongeze ..? nitakua natenda zambi kwa mtanzania anae umizwa na 99%
 
Sasa wakala wa usafirishaji anasafirisha kontena au vilivyomo kwenye kontena> nenda kasome kuhusu usafirishaji utaelewa.

Wanakamatwa kila siku wauza madawa ya kulevya wakiwa wamyabeba kwenye ndege, hakamatwi mwenye ndege wala wakala aliyemuuzia tiketi anaekamatwa ni mwenye mali.

Kuwa na akili japo kidogo.

Mbele ya CHADEMA, hakuna jiwe litakaa juu ya lingine, na kila goti litapigwa.Dr.Slaa alishaanzisha mafisadi 11, sasa tunawaleta kwenu wengine, wananchi ongezeni sauti za radio na TV.................
 
Umejitahidi!! Source vp?

Anne Kilango akiongea bungeni manake maelezo yapo kwenye hansard na Nyaraka zilizopo katika ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), zinaonyesha kuwa kampuni ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati Na. 47221.
 
huyu jamaa wanamwamini saana kwa kucheza rafu ndo maana wamemuweka kwenye safu ya uongozi wa chama ili kuandaa majeshi ya 2015,
 
Back
Top Bottom