hii ndiyo kampuni ya Abdulrahman Kinana

aiseeeeeee mkuu wakati huyu jamaa anachaguliwa RITZ alifurai sana na kupiga vigeregere ona sasa umeuziwa mbuzi kwenye gunia
 
It does. Sio lazima hisa ziwe reflected kama working capital au business networth. Ndio maana kuna financial facilities kama bank overdraft, invoice credit, loans etc.
Acha kamba wewe. Unaelewa implications za shares kwenye working capital?
 
Kuna vitu huwa tunashindwa kuvifahamu tu lakini kamwe ukishakuwa na chama tawala ambacho institutionally kiko corrupt huwezi kutegemea kupata mtu msafi. Hata watakaojitokeza kupiga kelele na kutuhumu wenzao ni kwa kuwa wanakuwa wamekosa mianya tu lakini si kwamba ni wasafi. Wako wapi akina Sitta, Mwakyembe na kundi lao la mgambo wa ufisadi? Unawasikia wakipiga kelele tena?
 
hihihiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiihihihihiihihiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiihihihih:A S 100:
 
Bei ya hisa 1000 jumla ya hisa 10000 hivyo mtaji ni 10,000,000/=
Mzigo uliokamatwa ni 1.4bil
Does this sound?


kama nimemuelewa vizuri hisa ni za umiliki wa kampuni sio za mzigo uliokamatwa, ingawa hata kwenye umiliki wa kampuni nahisi kuna makosa, labda in USD's.
 
Mashine za kufua nguo za kisasa zilizo tolewa na wahisani kwenda M


ount.Meru hospt.zilienda wapi hadi leo
 
Hawa huwa hawaitiji Source labda ingekuwa habari inawahusu Chadema ndio watu wangeomba Source.

Kwani Riz unahitaji source gani kujua kwamba Kinana anamiliki kampuni ya kusafirisha mizigo. Nini ambacho hujui au unatetea tu kwa sababu ni mwana ccm mwenzako. Sometimes unajidhalilisha kusafisha kila mchafu hapa jf.
 
Wacha unafiki na umbea kijana.Source yenyewe hujaweka unapayuka tu mdomo.Na isitoshe pembe za ndovu zilizokamatwa huko zote zimetoka Congo.

kaoshe glass ulale, wacha wanaume tujadili, Kinana anamiliki kampuni ya kusafirisha mizigo. Na kwa kupeana kazi ndani ya Ccm yawezakana hata hizo Pembe ni za kigogo mwenzake ndani ya Ccm.
 
Kama huna ushahidi wa kutosha utaambiwa wakati yanakamatwa kampuni ilikuwa ilishauzwa kwa watu wengine!
kumiliki kampuni ya kusafirisha na mmiliki wa meno tembo kutumia kampuni yangu tatizo nini? costa imekudiwa kubeba maiti na maiti ipo lakini imepakiwa ndani yake madawa ya kulevya je hiyo inakaaje?
 
Yale yale ya TPI na Kina Madabida!

Wandugu naomba msome hii taarifa ndio mjue nchi yetu imeoza

KAMPUNI ya uwakala iliyosafirisha kontena lililokuwa na meno ya tembo ambayo yalikamatwa nchini Vietnam, inamilikiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM na ambaye sasa ndiyo katibu mkuu Abdulrahman Kinana, imefahamika.
Taarifa zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo inayoitwa Sharaf Shipping Company iliyosajiliwa Dar es Salaam.
Mshirika mwenzake katika kampuni hiyo, Rahma Hussen anamiliki hisa 2,500 zenye thamani ya shilingi 1,000 kila moja.
Kwamujibu wa taarifa za usajili, wamiliki wote wawili, Kinana na Rahma wanapatikana kwa S.L.P 10910, Kiwanja Na. 403 Mtaa wa Tosamaganga, Msasani Peninsular, Dar es Salaam.
Nyaraka zilizopo katika ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), zinaonyesha kuwa kampuni ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati Na. 47221.
Sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali zilizosafirishwa na kampuni ya Sharaf Shipping Agency liliibuliwa bungeni kwa mara ya kwanza na mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.
Hati ya kusafirisha makontena hayo mawili yaliyokuwa yamesheheni pembe za ndovu ilisainiwa na mfanyakazi mwenye asili ya India wa kampuni hiyo Samir Hemani.
Nyaraka zote zilionyesha kuwa kilichokuwa ndani ni plastiki zilizorudufiwa, wakati baada ya makontena kukamatwa, walikuta yamesheheni pembe za ndovu.
Taarifa zinasema kibali cha kusafirishwa kontena hilo kilisainiwa 13 Novemba 2008 na Meneja wa Fedha na Utawala wa Kampuni hiyo.
Wakati Hemani anasaini nyaraka hizo, kibali chake cha kuishi nchini tayari kilikuwa kimeshaisha. Kibali cha Hemani kiliisha 7 Mei 2008.
Makontena yalikamtwa nchini China yakisafirishwa kwenda Hong Kong.
Akichangia makadirio ya bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2009/2010, Kilango alisema utafiti wake umeonyesha kuwa makontena hayo yalipitia bandari ya Dar es Salaam na nyaraka zinaonyesha ndani kulikuwa na plastiki.
Kilango alisema nchi zinazoongoza kwa kupokea nyara kutoka Tanzania ni Phillipines, China, Singapore na Hong Kong.
Kutokana na kutopatikana kwa Kinana juzi kuzungumzia suala hilo, haikufahamika iwapo kampuni ya spika huyo wa zamani wa Afrika Mashariki au yeye mwenyewe, walijua kilichokuwamo katika makontena hayo.
Lakini afisa mwandamizi katika wizara ya Viwanda na Biashara alisema kazi ya kukagua kilichomo kwenye kontena linalosafirishwa si ya wakala wa meli kwani wenye mamlaka na idhini ya kufanya hivyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Alisema wanaowajibika kusitisha mzigo kusafirishwa pindi wanapoutilia mashaka ni TRA.
"TRA ndio wanakagua na baada ya kujiridhisha kama kilichomo ndani ndicho kilichotamkwa kwenye nyaraka na ni halali, ndipo wanaweka muhuri (seal) wa mwisho," alisema afisa huyo.
"Ukitamka kwa mfano, kuwa katika nyaraka ndani ya kontena kuna matairi 40 ya magari, lazima TRA wafungue na kukagua kuona kama kweli yako matairi 40 au kitu kingine. Baada ya hapo wanaweka seal; sasa kuna kila sababu ya kujenga mashaka,” alieleza.
Alisema, "Wakala wa meli kazi yake ni kusafirisha mzigo wa mteja wake. Hata mteja akija na kontena tupu na kusema anataka liende nchi fulani, kazi yake ni kulipeleka kunakohusika na si kuhoji kilichomo.”
Alifafanua kuwa watu muhimu wa kuhojiwa na ambao wanaweza kuwa wanajua mchezo wote, kama upo, ni wafanyakazi wa TRA.
Hadi juzi Jumatatu hakukuwa na taarifa zozote za maofisa wa TRA kuhojiwa kuhusiana na sakata hilo.
 
Back
Top Bottom