Hii ndiyo inayosika namba mbili duniani kwa umaarufu

Hii ndiyo inayosika namba mbili duniani kwa umaarufu

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,679
12189011_1037267402982338_6089291010254985034_n.jpg

Sikuwahi kuzipenda muvi za Kihindi ila baada ya kuona trela la muvi iitwayo I, nikaamua kuidownload, imeigizwa mwaka huu, nilitaka kuona inahusu nini. Kiukweli niliipenda mno, hebu ngoja nikuhadithie jinsi ilivyo.

Muvi inaanza siku ya harusi, msichana Diya alikuwa akijiandaa kuolewa. Mishemishe zilikuwa nyingi nyumbani hapo, alirembwa chumbani lakini akaonekana kuwa na mawazo sana, bila shaka kuna kitu akawa anakiwaza mno.

Baada ya dakika kadhaa huku akiwa chumbani, kamera inatuonyeshea upande mwingine, kuna mtu mmoja wa ajabu, anatembea huku akiwa ameinama, mgongoni ana kibiongo, ukiiangalia ngozi yake, ina majipu mengimengi, yaani kama mtu aliyekuwa na malengelenge.

Mtu huyo anaitwa Lingesan. Ni mtu mwenye kisasi moyoni, kipindi cha nyuma hakuwa hivyo, alikuwa kijana handsome ila kutokana na wabaya wake kumfanya vibaya, alitaka kulipa kisasi. Siku hiyo ambayo msichana wake aitwaye Diya alikuwa akiolewa na mwanaume mwingine, hivyo alikuwa hapo kwa ajili ya kumteka, na kweli akafanikiwa, akamchukua na kuondoka naye kwenda kumfungia, mama wa bibi harusi alivyoambiwa kwamba binti yake katekwa, akazimia na harusi kusitishwa.

Baada ya kuonyeshwa mwisho yaani kwa staili ya FLASHBACK, muvi inaanza rasmi. Anaonekana kijana Lingesan akiwa mazoezini, huyu jamaa ni mtunisha misuli, amejazia haswa. Nywele zake nyingi, mustachi mkubwa, ukimwangalia tu, unajua kwamba ni mtu asiyejiweza kifedha.

Katika maisha yake ya huko gym, alichukiwa na kila mtu, ila hakujali, kuna siku walipanga kumpiga, akawapiga wote na kwenye mashindano ya kutunisha misuli akawazidi wote.
Ukiachana na maisha yake, kuna msichana alikuwa akimpenda, huyu alikuwa Diya, msichana mrembo aliyekuwa mwanamitindo. Baada ya kiushinda tuzo, akapiga picha na msichana huyo kwa kutumia kamera ya simu ndogo ya Nokia, vile visimu vya sh 20000/=, kwake ilikuwa furaha tele.

Kwa upande mwingine, Diya alikuwa mwanamitindo mzuri sana, kulikuwa na jamaa aliitwa John, mshikaji alimpenda sana Diya, alitamani kuwa naye, kwa kuwa kulikuwa na ziara ya kwenda China kupiga picha, mshikaji akatumia njia hiyohiyo kumtaka kimapenzi.

Diya akakataa, jamaa akamwambia utaona. Wakati John akijiamini kwamba atakwenda China, msichana akapitia mlango wa nyuma, akamtoa John, akamtafuta mwanaume mwingine ili achukue nafasi ya John, mwanaume huyo akawa Lingisan.

Jamaa alipofuatwa na msichana huyo, hakuamini, kwanza alikuwa akimtaka sana ila hakujua angempata vipi. Alivyoambiwa kwamba ilibidi aingie kwenye uanamitindo, akakubaliana naye, akaenda, akanyolewa nywele na ndevu, akapewa jina la Lee na wakaelekea nchini China.

Huko, wakaanza kupiga picha. Ila tatizo likaja kwenye picha za romantic, jamaa kila akipiga na Diya, mpiga picha anamwambia wanakosea, jamaa alipoulizwa kwa nini hujiamini? Akasema anamheshimu sana Diya, hivyo hawezi kukaa kiromantic naye.

Direkta akamwambia Diya kwamba ni lazima amwambie Lingsan kwamba anampenda ili awe huru, japokuwa Diya alikataa sana, akakubaliana naye, hivyo akamwambia jamaa, akachanganyikiwa mno, kuanzia hapo, picha zikafana sana.

Pale kambini kuna demu ambaye alikuwa akimpamba Lingsan akatokea kumpenda, alitumia nguvu zote kumpata ila hakufanikiwa. Alipoona mwanaume huyo yupo beneti na Diya, akaamua kumwambia ukweli kwamba huyo Diya hakuwa akimpenda, alimfanyia hivyo kwa kuwa tu alitaka picha zifanane na ukweli, kama anabisha, akamuulize.

Jamaa akaondoka, akaenda kumwambia msichana. Swali lake la kwanza ‘Do you love me?” (Unanipenda?) Diya akasema ndiyo.
Alichomwambia kingine, akamwambia aape kwa kumshika kichwani, Diya akakataa, hivyo Lingsan akajua ukweli kwamba hakuwa akipendwa, aliumia sana moyoni, kuanzia siku hiyo akaanza kuwa na mawazo mno.

Upigaji picha uliendelea zaidi. Yule John, akawatuma Wachina wammwagie tindikali Lingsan usoni ili aharibike, kilichotokea, Wachina wakapigwa sana na Lingisen. Baada ya kukamilisha upigaji wa picha, wakarudi India, huko, wakaendelea upigaji wa picha wa matangazo mengi, wakawa maarufu sana, wakatengeneza fedha na hatimaye wakaweka mikakati ya kuoana.

Siku moja Lingisan akaenda mpaka kwa meneja wake na kumwambia kwamba asingeweza kutangaza kinywaji kimoja kwa kuwa kinywaji hicho kina sumu ndani yake, bosi akakasirika, akamwambia afanye tangazo, jamaa akamwambia kwa kuwa watu wengi wanafanya anachokifanya, hivyo hatoweza, meneja akammaindi sana.

Mwisho kukawa na watu wanne wasiompenda Lingisan. Wa kwanza alikuwa John (huyu ni kwa sababu alichukua nafasi yake na kuwa maarufu) wa pili akawa yule mrembaji (Huyu alikataliwa, hivyo akawa na kinyongo naye) wa tatu akawa meneja (huyu ni kwa sababu Lingisan alikataa kutangaza kinywaji ambacho kingempa sana fedha) wa nne alikuwa baba yake Diya (huyu alimmaindi kwa kuwa alitembea na binti yake) wa mwisho akawa mtunisha misuli (huyu alimmaindi kwa kuwa alikuwa mpinzani wake)

Watu hao wanne wakaweka kikao, ilikuwa ni lazima Lingisan afanyiwe jambo moja kubwa. Mtu wa kwanza akasema amwagiwe tindikali, John akasema kwamba alijaribu kuwatuma watu nchini China wafanye hivyo, wakashindwa. Baba yake Diya akaingilia na kusema ‘More Than That’

Wa pili akasema auawe, baba yake Diya akaingilia na kusema ‘More Than That. Mwingine akasema wampe kilema cha maisha, baba yake Diya akaingilia na kusema ‘More Than That’. Kila walichokisema baba mtu alisema More Than That, so akaulizwa je alikuwa na adhabu gani kwa Lingisa, yeye akasema ni lazima watumie I yaani Influenza Virus, hivyo wamchome sindano kwani ilishawahi kutumika nchini Urusi na kweli wakafanikiwa.

Walichokifanya ni kuwatuma watu, wakafanikiwa kumteka Lingsan, hivyo akachomwa sindano ile. Siku moja akiwa anakwenda kuchana nywele, akaona kitana kinatoka na nywele, akashangaa, ngozi yake ikaanza kubadilika.

Akaenda kwa daktari, akampa ukweli kwamba aliokuwa akiumwa haukuwa ugonjwa bali alichomwa sindano yenye Influenza Virus hivyo hata uti wake wa mgongo utapinda na kuwa na kibiongo. Alipoambiwa hivyo, akakumbuka kwamba kuna siku alikuwa akioga, akaona amechomwa sindano begani, akajua kwamba hicho ndicho kilichotokea.

Wakati anawaza hivyo, akamuona yule jamaa mtunisha misuli, alikuwa miongoni mwa watu waliomteka ila akawapiga, akaanza kumfuatilia mpaka nyumbani kwa kina Diya, ndipo alipowaona wabaya wake wote isipokuwa baba yake Diya.

Muda huo aliharibika sana, hakuwa na nguvu za kupigana, watu hao wakaanza kumcheka kwamba walimkomesha, baba Diya alipotokea akaanza kumwambia kwamba watu hao walishirikiana kumfanya hivyo, wao walienndelea kucheka na kumwambia kwamba huyo aliyekuwa akimshtakia ndiye aliyetoa wazo achomwe sindano, jamaa alilia sana, wakampiga ila alichosema ni kimoja tu kwamba ATALIPIZA KISASI kwa wote, wakamcheka na kumwambia baada ya harusi ya Diya, wangemuua, ila cha ajabu akawatoroke. Hiyo ndiyo sababu ya kwenda kumteka Diya ili asiolewe na mtu mwingine.
*****
Huko mwishoni baada ya Diya kutekwa chumbani kwake, akawa anamuuliza yule mwanaume ni nani, jamaa hakuwa akijibu, Diya alilia sana, hakujua kama alikuwa ndiye mpenzi wake ambaye kuna siku aliambiwa kwamba alikufa, jamaa alifake kifo chake.
Diya akaomba aende chooni, akafunguliwa mnyororo,
alipokwenda kule, akajining’iniza kama amejinyonga, Lingisan akachanganyikiwa, alipoingia ndani kwa lengo la kumuokoa, akapigwa na msichana huyo na kukimbia.

Milango ilifungwa, alichokifanya Diya ni kumrudia Lingisan na kuanza kumpekua ili achukue ufunguo. Huko, akakutana na simu ya mpenzi wake, tena ikiwa na picha zao, akamfunga mnyororo na kumwambia yeye ni nani na kwa nini alikuwa na simu ya mpenzi wake, alichokifanya Lingisan ni kumuhadithia kilichotokea, tangu mwanzo mpaka hapo, Diya hakuamini kama kweli mtu huyo wa ajabu alikuwa mpenzi wake, hapohapo akazimia kwa presha.

VISASI

Lingisan aliamua kulipiza kisasi kwa watu wote, visasi vilivyowafanya kuwa kwenye maumivu milele, visasi vilivyowaumiza mioyo yao.

Unataka kujua aliwalipizia vipi visasi na wakati alikuwa kwenye hali mbaya, hakuwa na nguvu hata za kupigana? Itafute muvi hiyo. Itakufurahisha, itakuliza, itakufanya ujue kweli watu wanapenda.

Na unataka kujua kama Lingisan alipona au aliendelea kuwa hivyohivyo? Itafute muvi hiyo, inaitwa I imeigizwa nchini India na China na imetoka mwaka huuhuu.

Ngoja nitazame nyingine kisha nitakuja na MOVIE REVIEW nyingine.
 
Hiyo muvi niliiona kupitia Startimes nikiwa Mbeya.

Mwaka Juzi.

I (film) - Wikipedia

Halafu wewe unasema imeingizwa mwaka huu??

Tutafika tu.
Daaah huyu mkuu leo kayumba kweli. Hii movie mie nmeiona mwaka jana mwezi wa sita afu anatuambia ya mwaka huu..

Ahhh labda imeingia mkoani mwake mwaka huu.

Ila kiukweli hio ni bonge la muvi yaan huwezi kuielewa kwa kuangalia nusunusu. Lazma uiangalie yote ndo uielewe. Alieandika script yake kajitahidi sana
 
Daaah huyu mkuu leo kayumba kweli. Hii movie mie nmeiona mwaka jana mwezi wa sita afu anatuambia ya mwaka huu..

Ahhh labda imeingia mkoani mwake mwaka huu.

Ila kiukweli hio ni bonge la muvi yaan huwezi kuielewa kwa kuangalia nusunusu. Lazma uiangalie yote ndo uielewe. Alieandika script yake kajitahidi sana
Tena sanaaaaaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom