ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,529
- 21,530
My people,
Haya yanayoendelea sasa ni kiporo cha mambo ya nyuma ila bahati mbaya kiporo hiki kinapashwa na ubwabwa wa leo,ndio maana tunaona huu msuguano ambao unaendelea hivi Sasa
Ukiangalia historia huko nyuma TEC imekuwa ikilaumiwa kama kizingiti cha baadhi ya mambo ya Waislamu au haki zao kupewa kipaumbele,mfano haki ya kupata Mahakama ya Kadhi,hii mahakama si jambo la kustaajabisha sana,ni kutokuwa na elimu tu ni namna gani inafanya kazi,lakini ni mahakama ambayo inadili na ndoa na mirathi,sitozungumzia sana hapa kwani lengo sio hilo.
Kumekuwa na hitajio la kujiunga na Umoja wa nchi za kiarabu kwa dhumuni la kupata misaada kwa Waislamu kusaidia kutoa huduma mbali mbali za kijamii,hili nalo TEC wamekuwa mwiba katika kufanikiwa kwake
Kumekuwa na Memorandum of Understanding kati ya Serikali na Kanisa ambapo Kanisa linapewa hela na Serikali ili kufanikisha huduma kwa jamii kama hospital na mashule,swali linakuja je Waislamu hawastahili haya?
Kwahiyo ukiangalia kwa mapana yake kuna mambo ambayo Kanisa limefaidika moja kwa moja kutoka Serikalini na wakati Kanisa hilo hilo limekuwa kikwazo kwa Waislamu kushindwa kufikiwa kwa matakwa yao
Na kuna shutuma kwamba TEC imekuwa inatoa matamko mengi sana pindi tu Raisi anapokuwa Muislamu,na kuna taarifa kwamba ile misamaha ya kodi kwa vifaa vya ambavyo vinaagizwa na taasisi za dini,imeondolewa baada ya kugundulika kwamba viongozi hao wanatumia mgongo huo kwa manufaa yao binafsi,sasa Mama Samia Kachomoa king'amuzi watu wanashindwa kuangalia television,ndio makelele hayo mnayosikia kila kukicha,lakini upande wa pili kuna agenda yao
Sasa ukiangalia kinachotokea leo ni kweli TEC wanapigania haki na malalamiko ambayo watanzania wengi tunayo,lakini upande wa pili wanaamsha dude ambalo lilikuwa limelala,ndio hayo unayosikia Kobazi nao wanaliamsha.
Kwahiyo sio kwamba Kobaz hawajielewi,au wanaropoka hovyo au hawajaenda shule kama baadhi yenu mlivyojawa na propaganda za zamani kwamba Waislamu hawana shule kichwani,acheni hizo fikra zenu hasi
Kwahiyo kuna kiini cha haya mambo ambayo bado hayajatafutiwa ufumbuzi kati ya Waislamu na Wakristo ambayo nayo inatakiwa itafutiwe Tume ya kujua Chanzo na Kujua suluhisho lake
Ila haya kwasasa yasubiri kwanza,tudili na lile kubwa ambalo lipo mbele yetu,kikubwa sisi wafuasi wa dini tusiingie kwenye uhasama wa dini zetu,tuendelee kuwa imara kupendana na kuvumiliana kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote
Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania
Ni hayo tu!