Hii ndiyo chanjo unayotakiwa kutumia

Hii ndiyo chanjo unayotakiwa kutumia

Mwenye Akili Ni yule ambaye angalau katengeneza chanjo lkn bado hazijawa perfect 100% huyu hata kutengeneza Panadol hawezi unamuita ana Akili?
Akili ingekuwa inapimwa Kama hivyo nafkiri hata familia yako wote mngekuwa wehu au machizi[emoji16]
 
Umesahau sifa moja;
~ inatakiwa ifanyiwe majaribia siyo chini ya miaka miwili mpaka miaka kumi. Hii hudhihirisha ubora, na ufanyakazi wake kulingana na watu tofauti tofauti kulingana na mtengenezaji atakavyochagua
Na jaribio la kwanza lazima lifanyike kwa mnyama tofauti na binadamu.
 
Usione wivu watu kufaidi kutokana na Akili zao.Waliotengeneza chanjo watapiga pesa.Hiyo Ni faida ya kuwa na Akili.Watapiga pesa yes.Na kwa vile sisi tupo vizuri kwenye uchambuzi wacha wajanja watumie vichwa vyao kutengeneza faida.
Sisi Kama hatutaki kutengeneza tiba wao watatengeneza.Wanatumia Akili na pesa nyingi,Akili zao na pesa zao Lazima tulipie.
Sawasawa brother
 
Na jaribio la kwanza lazima lifanyike kwa mnyama tofauti na binadamu.
You are right mkuu Kuna phase 1 ya trials ambayo wanyama wanaanza kutumika wadogowadogo then hatua nyingine zinafuata
 
Chanjo ni maandalizi ya kibaolojia yanayolenga kuchochea uwezo wa mwili kajitengenezea antibodies na immunity(kinga) zinazosaidia kukabiliana na ugonjwa husika bila yenyewe (chanjo) kusababisha ugonjwa.faida za chanjo Ni nyingi ukiacha yamuhimu kabisa ambayo nikuokoa maisha ya watu faida nyingine nikutengeneza pesa nyingi kwa watengenezaji na faida nyingine nyingi za kiuchumia na kijamii.

SIFA ZA CHANJO UNAYOTAKIWA KUTUMIA KISAYANSI ;
mwanasayansi msomi au mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na Mimi zifuatazo Ni sifa za chanjo watanzania waafrika au watu mahali popote duniani tunatakiwa kuzitumia kwafaida yetu kiafya.

1.USALAMA(chanjo yoyote inatakiwa kuwa salama kwamaana haitakiwi yenyewe iwe chanzo Cha magonjwa au kifo).

2.ULINZI DHIDI YA MAGONJWA HUSIKA.(chanjo yoyote ili iitwe chanjo lazima iwe na uwezo wakumlinda mtumiaji dhidi ya ugonjwa au magonjwa husika).

3.UWEZO WAKUFANYA KAZI MUDA MREFU; chanjo yoyote lazima iwe na uwezo wakumlinda mtumiaji kwa muda mrefu miaka 40, 50 au zaidi bila kumletea madhara kiafya yamuda mrefu au mfupi.

4.UWEZO WAKUSABABISHA AU KUCHOCHEA UTENGENEZAJI WA(T-cells); ambazo nimuhimu katika ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa.

5.ZISIWE na MASHARA KABISA KAMA KIFO N.K
Kama yatakuwepo basi ni madogomadogo na kwamuda mfupi.

6.GHARAMA STAHIMILIVU au ZAKAWAIDA (gharama zinategemeana na watengenezaji na sababu nyingine lakini chamuhimu zisiwe zakibiashara zaidi kuzidi lengo madhubuti lakuokoa maisha ya watu.

7.UWEZO WAKUSTAHIMILI MABADILIKO YA KIBAOLOJIA NA KIJIOGRAFIA.

Hizi ni baadhi ya sifa chache za muhimu ambazo chanjo yoyote salama inatakiwa iwe nazo.je chanjo ulizowahi kutumia zina sifa hizo?? Au Chanjo ya Covid19 ambayo ndiyo habari ya mjini inazo hizo sifa?? Kama inazo basi nashauri tuzitumie kwa usalama wa Afya zetu nakuacha kufuata mikumbo au mihemko.Asante[emoji1431].
Kwa hakika umeongea kama Mtanzania ninayemfahamu fika. Hivi unajua tuko karne gani hii? Je unakiri kuwa yapo mengi ambayo yasingewezekana karne zilizopita lakini hivi leo yanawezekana.

Je una habari katika karne ya 15 binadamu alitumia muda gani kuzunguka dunia? Je leo hii binadamu huyo huyo angechukua muda gani? Tatizo kubwa linalowakabili Watanzania walio wengi ni ujinga.

Hakuna binadamu wanaoogopa mabadiliko kama Watazania na hii ni katika nyanja zote za maisha yake na wewe bernard10 ni mfano halisi wa Mtanzania huyo. Hauko tayari kwenda na wakati, unaogopa.

Mabadiliko yoyote yawe ya kijamii, kiutamaduni, kielimu, kiuchumi, kisiasa, kisayansi, kiteknolojia n.k. kwa Mtanzania ni ya kuogopwa kama ukoma. Kwa hakika Watanzania tuko tofauti na binadamu wengine.

Sijui na sina hakika kama na wewe uko kwenye kundi linaloogopa hata Katiba mpya, ha ha haaa! Siku njema bernard10!

Kwa ukumbusho!: Wako Watanzania sina hakika ni wa dini ipi waliwahi kutinga na kupiga kambi Uwanja wa Ndege wakitaka kusafiri kwenda kueneza injili kwa mataifa ya mbali bila pasi, nauli wala visa. Waliamini Mungu atawawezesha tu kufanikisha safari yao. Ilibidi nguvu itumike kuwatimua Uwanja wa Ndege...Watanzania, loo nawavulia kofia!
 
Umesahau sifa moja;
~ inatakiwa ifanyiwe majaribia siyo chini ya miaka miwili mpaka miaka kumi. Hii hudhihirisha ubora, na ufanyakazi wake kulingana na watu tofauti tofauti kulingana na mtengenezaji atakavyochagua
Hii ni tunayotumia ni MWENDOKASI kuanzia tume iliyoundwa na RAIS hadi kuletwa CHANJO NCHINI.

Sijui kama ilifika mwezi kutoka majibu ya TUME na kuletwa CHANJO nchini.
 
Najitahidi kukuelewa lakin imekuwa shida kidogo alioandika uzi huu siyo watanzania Ni mtanzania mmoja usi waatack watanzania wote alafu ungejikita kwenye mada siyo mipasho yako na taarabu nyingi
 
Umesahau sifa moja;
~ inatakiwa ifanyiwe majaribia siyo chini ya miaka miwili mpaka miaka kumi. Hii hudhihirisha ubora, na ufanyakazi wake kulingana na watu tofauti tofauti kulingana na mtengenezaji atakavyochagua
Wakati majaribio yakiendalea kwa miaka 10, huo ugonjwa uliolipuka utadhibitiwa vipi? Vifo viendelee tu ili kusubiri majaribio yaishe?Kumbuka ugonjwa ni dharura, dharura haisubiri miaka 10. Haya ndiyo matatizo ya wasomi wa Tanzania, yanakaririgi tu nadharia, nje ya hapo vichwa havichanganui mambo!
 
Hii ni tunayotumia ni MWENDOKASI kuanzia tume iliyoundwa na RAIS hadi kuletwa CHANJO NCHINI.

Sijui kama ilifika mwezi kutoka majibu ya TUME na kuletwa CHANJO nchini.
Wanajaribu kuupiga mwingi kwenye maisha ya watu
 
KENYA: WATUMISHI WA UMMA WASIOPATA CHANJO YA CORONA KUADHIBIWA Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Utumishi wa Umma, Wafanyakazi wa Serikali wanapaswa kupata Chanjo kufikia Agosti 23 Mwamko mdogo wa Chanjo umeathiri utoaji wa huduma za Umma Soma > #COVID19 - Civil Servants who won’t take COVID-19 vaccine to face disciplinary action #UVIKO3
Siyo Kenya tu Marekani watu mbaka wanaachishwa kazi Ufaransa almost kila sehemu kila huduma lazima uonyeshe umechanjwa ndyo maana watu wanaandamana kupinga maamuzi hayo yakidharimu
 
Siyo Kenya tu Marekani watu mbaka wanaachishwa kazi Ufaransa almost kila sehemu kila huduma lazima uonyeshe umechanjwa ndyo maana watu wanaandamana kupinga maamuzi hayo yakidharimu
Usipochanja ni sana kufanya zinaa bila kondomu.Unataka kuuwa wenzioo.
 
Back
Top Bottom