ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
11/03/2013
Chanzo: Gajetek - Gajet na Teknolojia
Hii Ndio Samsung Galaxy S4?
Zikiwa zimebakia siku tatu/nne kabla ya uzinduzi rasmi wa Samsug Galaxy S4 huko New York, picha inayoaminika kuwa ni ya simu hiyo imeenea kwenye mitandao ya gajeti na teknolojia. Picha hizo zimenaswa kwenye foram ya 53Samsung. Simu hiyo ambayo wadau wengi wanaamini ni ya bandia lakini yenye umbile halisi ya Samsung Galaxy S4 inafafa zaidi ya Samsung Galaxy Note II kulioko Samsung Galaxy SIII.
Inapishana na Galaxy Note II kwenye suala la kamera. Wakati Galaxy Note II kamera yake ina flashi upande wa kulia wa simu, simu inayosemekana kuwa ni Galaxy S4 ina flashi kwa sehemu ya chini ya kamera. Pia sehemu iliyopo flashi haifanani na ilivyo ya Samsung Galaxy SIII.
Wengi kati ya wanateknolojia wanaamini kwamba S4 itakuwa kubwa zaidi na haitabadilika sana kimaumbile. Pia inatarajiwa kuwa na mambo mapya kadhaa kwa upande wa software. Samsung hujaribu kutoa software mpya kila mwaka kwanza kupitia kwenye familia ya Galaxy S tangu karibu miaka minne iliyopita Samsung walipoamua kuwa hii ndio itakuwa simu yao kuu (flagship device)
Ukweli utajulikana baada ya siku kadhaa kuhusu picha hii. Hata hivyo minon'gono na tetesi ni sehemu ya habari za gajeti na teknolojia kwa vile kampuni hujaribu kufanya usiri mkubwa wa gajeti zao kabla ya uzinduzi rasmi. Itakumbukwa kuwa blogi ya Gizmodo mwaka 2010 walikuwa wa kwanza kutoa picha za iPhone 4 miezi kadhaa kabla ya uzinduzi rasmi, baadae ilikuja kudhihiri kuwa picha ile ilikuwa ni ya kweli.
Apple wamewapiga marufuku Gizmodo kuhudhuria mikutano ya WWDC mpaka leo, pia walibumburushana nao mahakamani kwa kuipata simu hiyo kinyume cha sheria, Gizmodo waliwarudishia Apple simu yao ambayo ilisahauliwa Bar na mmoja kati ya maofisa wao wa ngazi za juu ambaye alikuwa anaitumia kwa majaribio, Inaaminika Gizmodo walinunua simu hiyo kwa kiasi cha dola 5,00 hadi10,000 kutoka kwa "aliyeiokota".