Hii ndio Miji 10 ya hatari zaidi duniani

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,225
Vitendo vya Ugaidi ni miongoni mwa stori zinazoshika na kuweka headlines kubwa sana duniani, na kwa sehemu nyingi za dunia vitendo hivi sio vya mchezo kabisa.

Kutokana na ukuaji mkubwa wa vitendo ya Ugaidi duniani, makosa kama uwizi kwa kutumia mitandao, uhalifu wa IT na migogoro baina ya mipaka ya nchi ni vitu vikubwa sana, unaweza kusema hakuna nchi iliyo salama kabisa.



Nimekutana na orodha moja iliyo orodhesha Miji 10 ya hatari duniani, Miji 4 ya Afrikaimetajwa, ungependa kuijuwa? Nimekusogezea picha zake hapa chini.

1. Afghanistan, Kabul



Hakuna idadi ya wanajeshi wa Kimarekani wanaoweza kuusaidia mji mkuu waAfghanistan, Kabul dhidi ya matukio ya Kiagaidi nchini humo. Na huu ndio mji wa hatari zaidi duniani. Matukio ya mabomu, kulipuliwa kwenye mahoteli na Ubalozini ni kitu cha kawaida.

2. Somalia, Mogadishu



Mpaka hivi karibuni, Mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ulikuwa moja kati ya miji hatari zaidi duniani. Umoja wa Mataifa walijiondoa kwenye ulinzi na usalama wa nchi hiyo baada ya Serikali tawala kuanguka mwaka 1991. Matukio ya Al Qaeda yalivuma mpaka mwaka jana ambapo wapiganaji wa Umoja wa Afrika waliingilia kati.

3. Iraq Baghdad



Iraq, Baghdad ni miongoni mwa miji ambayo sio salama pia na kwenye matukio mbalimbali ya Kigaidi hutokosa kulisikia jina lake. Lakini baada ya Marekani kuingilia kati matukio mengi yanayotokea mjini Baghdad hali kidogo imetulia. Miaka mingi ya matukio mbalimbali imeharibu miundo mbinu ya mji huo.

4. Ciudad Juarez,Mexico.



Mexico ni nchi inayofahamika kama bandari ya madawa ya kulevya duniani kupitia mji waCiudad Juarez. Wafanyabiashara wa madawa ya kulevya Mexico wanaogopwa na mapolisi wengi ni vijakazi wao wakubwa. Ciudad Juarez ni moja kati ya miji hatari zaidi duniani ukitoa maeneo yake ya vita.

5. Abidjan, Ivory Coast.



Abidjan ni mji uliopo Ivory Coast ambao kwa muda mrefu kulikuwa na matukio ya kialifu mengi sana yaliyoteka headlines mbalimbali duniani lakini baada ya kukamatwa kwa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo alievua majukumu yake kumpatia Rais aliyechaguliwa Alassane Outtara, Abidjan kidogo imetulia lakini bado unahesabika kama mji hatari.

6. Caracas, Venezuela.



Caracas mji mkuu wa Venezuela nao pia upo kwenye list ya miji hatari zaidi duniani na unahesabika pia kama bandari ya madawa ya kulevya. Makosa kama uwizi, kuporwa na makosa mengine madogo ni vitu vya kawaida sana kwao mapolisi hawana sauti wala nguvu ya kudhibiti vitendo hivi.

7. Sana’a, Yemen.



Mji mkuu wa Yemen, Sana’a umekuwa ukiingia kwenye headlines mbalimbali duniani kufuatia vita dhidi ya aliyekuwa Rais wa nchi Ali Abdullah Saleh. Mgogoro huo umefuatia na matukio kadhaa ya Kigaidi nchini humo na kuwekwa kwenye orodha ya miji hatari zaidi duniani.

8. Peshawar, Pakistan.



Pehsawar mji uliopo Pakistan ni miongoni mwa miji hatari duniani, mji huu sio salama kabisa kwa wageni matukio ya kutekwa na kulipuliwa na mabomu ni matukio ya kawaida sana kwao.

9. Nairobi, Kenya.



Matukio ya Al Shabaab nchini Kenya pamoja na matukio mengine ya kiualifu iliiwekaKenya kwenye headlines mbalimbali. Kutembea au kusafiri usiku nchini Kenya sio salama kabisa kwani kuibiwa na kuporwa ni matukio ya kawaida.

10. Cape Town, South Africa.



Cape Town mji uliopo South Africa ni maarufu sana kwa maeneo ya kitalii duniani, lakini ikifika usiku mji huu sio salama kabisa kwa matembezi haswa kwa wanawake. Matukio mengi ya uhalifu ni kutokana na ubaguzi wa matabaka kati ya matajiri na maskini.
 
Manzese na Tandika zimeshindwa kuibeba Dar... Basi wanaume wa Dar waliamua kuwadhibiti Watoto wa Mbwa dogo dogo centre
 
[quote uid=379621 name="sumu-ya-panya" post=17139385]ongeza na sinoni daraja mbili ololo karibu na stend[/QUOTE]<br />[quote uid=345823 name="adden" post=17139422]Hee ngarenaro,unga limited na matejoo hazipo hapo.huu utafiti feki[/QUOTE]<br />bado hatujafikia viwango hivyo jomba.. halafu muache kutuchoresha mazee! hatutaki usoro...

Kweli asee chalaa angu arifu moja ilinitokea na panga ina kutu kinyama asee ile mtaa haifai kabisa pale mtoni matejoo
 
Johannesburg, Aleppo, Mogadishu, Washington haipo , hata Nairobi mnawaonea
 
Johannesburg, Aleppo, Sirte, Washington haipo , hata Nairobi mnawaonea
 
Haahaaa Caracas nayo imo..utafiti wa Magharibi bhana yaani ukikataa kuwatii lazima wakuchafue
 
Back
Top Bottom