Hii ndio maana ya ndugu lawama

Hii ndio maana ya ndugu lawama

Unaonesha wewe ni mtu wa vinyongo sana. Yatazame maisha kwa upana wake utajifunza kupotezea baadhi ya mambo. Maana hata hao marafiki uliowamwagia maua si wote na mara zote wanakuwa waaminifu, wapo wengi wanafiki. Ni kuwajua binadamu na namna ya kuishi nao.
Ndugu usitukane mamba kabla haujavuka mto, yatakukuta hautaamini kuwa ni wewe uliandika hivi. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji ili maumivu ya kunyolewa kwa kitana cha wembe nywele zikiwa kavu yasikukute.

Hapa mimi sileti kinyongo naongea masibu ya maisha. Kuna vitu vinakukuta unajiuliza utazungumza na nani kama watu wa karibu ndio wanakufanyia. Shuhuda zipo uliza hata hapa ni vile watu hawapendi kuweka mambo yao personal mtandaoni au public ila aisee usichukulie poa mtu anapokuwa anasema ya moyoni.

Wengine wanafanyiwa matukio ya kisirani na wake na watoto wao wa kuwazaa kabisa. Atakwenda kumwambia nani unadhani? [emoji848]

Usiwe mtu wa kujudge ila hoji ndipo utajifunza.
 
sio kila mtu mwenye ajira anakuwa na hela sometimes mtu anaenda kazini kila siku lakini kipato chake kinamtosheleza kula na ada ya watoto

Sasa kwq mishahara yetu hii unakuta ndugu ameomba umsaidie milioni 1 au laki tano unaipata wapi mkuu

Mfano mimi mwezi uliopita kuna watu wameniomba
1.500,000
2.200,000
3.Na kuna dogo ananiomba ni mnunulie smartphone 300,000

Mimi binafsi nina plan ya kununua kiwanja niache mipango yangu nimejinyima karibu mwaka mzima uniletee mipango yako eti nipe hela nifungue buashara

Lakini kiuhalisia roho zetu zinatuuma kushindwa kusaidia ndugu zetu

Sasa kwa mtu ambaye hafanyi kazi au ndo anajitafuta akiomba msaada akianza kuzungushwa anazani watu wanambania

Mi binafsi mkuu nakuombea ufanikiwe ili uelewe hii situation

Inafika mwisho wa mwezi hadi wajomba kijijini wanakupigia wewe uwasaidie hela ya kula huo mzigo wote utauweza? na usipo saidia ni lawama kama hizi
Mimi sijasema naomba msaada wakati huu. Mimi nina maisha yangu na sina uhitaji wa msaada kwa sasa hiyo ni experience nimepitia ndani ya miaka kama 8 au 10 kwa sasa. Muda huu sipo huko tena.

Hapa kinachonifanya kuandika uzi huu ni baada ya kupata taarifa za namna ndugu wanatafuta access ya kunifikia kwa ukorofi wao halafu mimi ni mtu ambaye nimeamua kuwa kimya na sina tena habari za kufautiliana nao.

Nawapa tu sapoti ya mbali na kudeal na bi mkubwa direct maana ndie mwenye access na mimi. Nafanya hivi sababu nimewagundua si watu wenye dhamira nzuri nadhani ni sababu ya kukosa exposure ya maisha.

Kuna mtu anaweza kuwa na miaka 40 ila hajui maisha hata kidogo ila kuna dogo unakutana nae miaka 18 ila maisha na kanuni zake zimenyooka anaweza kuishi popote na yoyote.
 
Ndugu usitukane mamba kabla haujavuka mto, yatakukuta hautaamini kuwa ni wewe uliandika hivi. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji ili maumivu ya kunyolewa kwa kitana cha wembe nywele zikiwa kavu yasikukute.

Hapa mimi sileti kinyongo naongea masibu ya maisha. Kuna vitu vinakukuta unajiuliza utazungumza na nani kama watu wa karibu ndio wanakufanyia. Shuhuda zipo uliza hata hapa ni vile watu hawapendi kuweka mambo yao personal mtandaoni au public ila aisee usichukulie poa mtu anapokuwa anasema ya moyoni.

Wengine wanafanyiwa matukio ya kisirani na wake na watoto wao wa kuwazaa kabisa. Atakwenda kumwambia nani unadhani? [emoji848]

Usiwe mtu wa kujudge ila hoji ndipo utajifunza.
Katika umri wangu huu nimekutana na changamoto zote ulizozieleza. Lakini nimejifunza kuwa positive. Mwenye ubaya ana uzuri wake pia, hata kama ni kidogo. Bahati mbaya umechagua kuona ubaya wao.
Ukweli usioweza kuruka ni kwamba udugu ni hazina. Ndiyo maana ukifa, au ukaumwa na kulazwa muda mrefu hospital, umepata ajali huna fahamu nk, washikaji zako pamoja na yote mema watayokufanyia watakurudisha kwa ndugu zako. Na iwe kwa masingo au ukarimu ndugu watakupokea TU.

Hili la mwisho linadhihirisha kuwa nduguzo ni kama kivuli chako, huwezi kukikwepa. Jifunze namna ya kuishi na ubaya haulipwi kwa ubaya. Kufanya hivyo unakuwa sehemu ya ndugu wenye matatizo. Show the difference
 
sio kila mtu mwenye ajira anakuwa na hela sometimes mtu anaenda kazini kila siku lakini kipato chake kinamtosheleza kula na ada ya watoto

Sasa kwq mishahara yetu hii unakuta ndugu ameomba umsaidie milioni 1 au laki tano unaipata wapi mkuu

Mfano mimi mwezi uliopita kuna watu wameniomba
1.500,000
2.200,000
3.Na kuna dogo ananiomba ni mnunulie smartphone 300,000

Mimi binafsi nina plan ya kununua kiwanja niache mipango yangu nimejinyima karibu mwaka mzima uniletee mipango yako eti nipe hela nifungue buashara

Lakini kiuhalisia roho zetu zinatuuma kushindwa kusaidia ndugu zetu

Sasa kwa mtu ambaye hafanyi kazi au ndo anajitafuta akiomba msaada akianza kuzungushwa anazani watu wanambania

Mi binafsi mkuu nakuombea ufanikiwe ili uelewe hii situation

Inafika mwisho wa mwezi hadi wajomba kijijini wanakupigia wewe uwasaidie hela ya kula huo mzigo wote utauweza? na usipo saidia ni lawama kama hizi
Hakuna anaekupangia maisha ila hapa hatuzingumzii kuingiliana mipango tunazungumzia tabia ushirika kati ya ndugu especially wa familia moja katika kuboresha maisha yao na kupiga hatua.

Unaona sasa mfano wewe, mdogo wako anakuomba laki 3 akanunue simu wewe unataka kwenda kununua kiwanja ukajenge. Umejua huyo mdogo wako anataka kufanya nini na hiyo simu? [emoji848]

Hapo umeassume tu kuwa dogo anataka kupata simu ya kuchat chat na mademu au kupost video TikTok na kufuatilia umbea Instagram. But unasahau kuwa kuna fursa mitandaoni huko kuliko mitaani ambazo pengine wewe hauzijui na hautaweza zifanya ila dogo ataweza fanya na zikamuingizia hata 40,000 kila siku na akawa vema hata kukushinda.

Niffer unamuona yule binti, alianza mdogo mdogo anauza vitu mtandaoni mama yake alimsapoti hakumpuuza kumpa sapoti hata yeye huwa anasema, leo unaona alipo? Mama yake alijua binti yangu atakuwa anaenda china na dubai kufunga mzigo wa mamilioni na kuwanyima usingizi watu wa kariakoo kwa simu tu? [emoji848]

Hizi sasa ndizo mentality za kichawi. Wewe umepata access ya kazi au biashara inakupa kipato cha kumudu maisha hata ya kumiliki kiwanja,kumpatia dogo laki 3 unaona adhabu na upo radhi umpotezee ili wewe ununue kiwanja ambacho probably unaweza usimalize ujenzi wake ndani hata ya miaka 10.

Dogo anakwenda kwa marafiki zake wakamkopesha simu au kumsapoti akapata namna ya kupata simu akaanza kuchangamkia mishe mishe zake MUNGU akamkunia nazi akapata cha kumkeep busy na kumpa kipato.

Utashangaa wewe na hivyo viwanja vyako mpo tu hapo na dogo ndie anakuja kukupa sapoti ya mifuko ya cement na akaja kuwa na kipato cha kumudu ujenzi wa nyumba akamaliza kabla yako na akapata nyumba zaidi ya tatu. Wewe ukamaliza ujenzi na ukashindwa kumudu maisha ukawa na nyumba lakini huna chakula ndani halafu huyu dogo akawa ndie tumaini kwako ukajinyenyekesha kwake ili akusapoti kwa chochote kitu.

Sasa usije chukia na yeye akakwambia sina laki 3 ya kukusaidia kwenda kupata matibabu ya hospital ila unamuona akienda kitambaa cheupe na rafiki zake wakila maisha na anateketeza zaidi ya milioni kwa wiki. Wewe unabakia kumsema na kumfitini kwa ndugu waliosalia.
 
Kama Una pesa wasaidie ndugu zako.

Usiwe MTU wa visasi.
Haujanielewa mimi hapa nakemea pepo la roho ya kwann ngazi ya familia. Bora ukutane na watu au mtu uraiani akuletee fitina utasema huyu ni mtu hanijui so mimi ni wanini ila kitu mbaya ni mtu ambaye mnatoka familia au ukoo wako anakufanyia figisu au anakupuuza unakubali kuwa ndivyo alivyo halafu unajiweka mbali nae unaona anaanza kukuletea swaga za lawama na kukuletea maneno meusi kwa ndugu as if mnaukaribu au ulishawahi kumdhurumu kitu mahala popote.

Kama kusaidia nasaidiana na wale tunaoshirikiana hata kama hawajawahi kunipa hata mia yao.

Unakuta una ndugu yako aidha binamu, dada wa tumbo moja, shangazi, au mamdogo ana maisha ya chini sana na anaishi kwa kujitafuta sana. Lakini bado mtu huyu huyu wakati mambo yamekua magumu yeye anakuwa ana huruma na wewe kuanzia kwenye namna anakusikiliza, namna anazungumza na wewe na namna anashirikiana na wewe. Imagine anakwenda kukopa 1.5 milioni anakudhamini na ukimtazama sio mtu wa kuwa hata na 50,000 mfukoni akipata dharula. Na anamshikirisha mume wake nae anakudhamini sehemu 2 milioni sababu ya uaminifu wake watu wanampatia.

Hawa watu wewe unawaacha vipi katika haya maisha.

Ukiona haujanielewa then jitathimini sana kuhusu maisha haya unayaishi vipi au unayaelewaje.
 
Kuna muda washikaji tuliokutana nao maishani Ni Bora kuliko ndugu
Wanasema ndugu zako miaka hii hamtazaliwa pamoja mtakutana uraiani.

Ukishaanza maisha sasa ndio utajua mawe na mchele vipo wapi. Ndugu zako ambao wanakupenda hawatakuacha uwe pekee yako katika haya maisha watakuwa na wewe bega kwa bega hata pale wanapokuona unapoteza sana wao wao watakuwa dhamana yako bila kuchoka hata mara 70 mradi wakuone unasimama.

Halafu kuna wale wanataka ukosee au au uharibu ili waseme "Si niliwaambia" au waseme " huyu sio wa kuhangaika nae". Its like ndani ya nafsi wamejiwekea kuwa wao hawatakiwi kutoa bali kupokea na pia wanahofu kukuona unainuka na kuwa juu maana unaweza kuwa threat kwenye nafasi zao kwa familia au pengine wanakuwa na hofu ya kuonekana wao wamezembea maisha wewe umeonyesha uwezo na bidii kuwashinda wao na hivyo unawadhalilisha.

Wanakuwa hawapendi tu waone unapiga hatua wao wanataka udumae ndio maana wanashindana na wewe. Ukidumaa hawana cha kukupa sapoti ila watakugeuza kwua emotional punching bag ukianza kupiga hatua wanataka kukukata gwala ili wao ndio waonekane namba moja.
 
Dah noma sana , sasa usiombe yule mwenye ushawishi mkubwa ndio akuoneshe dharau na aanze kuwaambukiza madogo kuwa hufai huna msaada wowote , madogo wanalipokea haraka mno. Mpaka waje waelewe ukweli umesota sana
Ushawahi ona ile umemaliza chuo halafu umekula alosto sasa ule muda watu wengine huwa unakuwa mrefu sana unaweza sota hata miaka 5 hadi 8 maisha yamekukataa unaishia kufanya mishe tu za hapa na pale.

Unakutana na matukio unakichezea unasema ngoja nirudishe mpira kwa kipa kwanza nianze upya. Sasa hapo ndio unakichezea balaa. Badala ya wanandugu kukusitiri wanakujengea fensi wakunyooshe.

Mara wakuunganishe kazi kwenye ofisi za watu za kujitolea wewe akili yako haipo kwenye kuajiriwa unataka kufanya biashara ukomae mwenyewe, mitaji hamna ukitaka washirikisha wanakutema kuwa wewe ni mvivu, mzembe, mjuaji, haushauriki.

So hapo ndipo ukiomba hata pesa sapoti ya nauli ya kwenda sehemu ile tafu unajibiwa kama sijui umeomba milioni.

Mixer kukufuatilia, kuongea mambo ya dharau mbele ya madogo hadi wanawajaza ujinga madogo wanaanza kukudharau adabu zinashuka inauma kichizi.

Unakuwa mtu wa kutafuta faraja kwa marafiki badala ya familia. Siblings wako wanakuwa ni watu wa kushindana na kuleta upinzani usio na kichwa wala miguu. Sababu tu ni haujakaa sawa kiuchumi na wao wanakuona kama threat sasa sijui threat ya namna gani maana wewe hauwachukii wala hauna time na mapungufu yao.

Mwisho wa siku umejikusanya umesepa kimya kimetawala wanaanza kufosi ukaribu. Sio sikukuu wala weekend siendi tena home. Bi mkubwa nazungumza nae kwenye simu tu na ninamtumia ninachojiskia kutuma sitaki kupangiwa na mtu maana si niliambiwa asiyefanya kazi na asile mbona wao hawajafanya kazi why wanataka kula sasa, sheria si ni ile ile? [emoji848]
 
Katika umri wangu huu nimekutana na changamoto zote ulizozieleza. Lakini nimejifunza kuwa positive. Mwenye ubaya ana uzuri wake pia, hata kama ni kidogo. Bahati mbaya umechagua kuona ubaya wao.
Ukweli usioweza kuruka ni kwamba udugu ni hazina. Ndiyo maana ukifa, au ukaumwa na kulazwa muda mrefu hospital, umepata ajali huna fahamu nk, washikaji zako pamoja na yote mema watayokufanyia watakurudisha kwa ndugu zako. Na iwe kwa masingo au ukarimu ndugu watakupokea TU.

Hili la mwisho linadhihirisha kuwa nduguzo ni kama kivuli chako, huwezi kukikwepa. Jifunze namna ya kuishi na ubaya haulipwi kwa ubaya. Kufanya hivyo unakuwa sehemu ya ndugu wenye matatizo. Show the difference
Dah basi mzee kama umepitia kuna kipande cha somo haujakielewa au pengine uliwachukulia tofauti hawa ndugu zako kwa namna ambavyo ulipitia.

Nadhani kuna level ya maisha ukiwapo unajua kwamba hapa siwezi wategemea hawa ndugu zangu maana si watu wenye uwezo wa kunitoa au kunisapoti nilipo halafu kuna level unaona kabisa huyu hapa anaweza nisaidia hiki kipo ndani ya eneo lake na hashindwi ila kaamua kutochukulia serious issue yangu kwasababu zake personal aidha uoga wa maisha, hataki kukudhamini sababu haoni impact au matokeo ya kile anachotaka kufanya na kadhalika.

But unamuona anafanya jambo kama lile kwa watu wengine na hakuna uzito. Ntakupa mfano, una labda kaka yako mkubwa, unamuomba akusapoti kiasi cha laki 5 au milioni na ni pesa ambayo utarudishia sio kuichukua.

Halafu anakwambia mimi kwa sasa sina hiyo pesa. Halafu wewe unachat na mkewe anakupa story kuwa amemkatia tiketi ya ndege yeye na watoto wanakwenda Dubai vacation au kutembea Serengeti kwa muda wa wiki mbili kula bata. Ukipiga hesabu za haraka hiyo hapo ataspend si zaidi ya 3milion. Na hapo huyo shemeji yako anazungumza haya na wewe ni mieze labda miwili baade baada ya kumpelekea shida zako kaka yako na hajui chochote kuwa una hizi taarifa.

Unaamua kukubali kuwa kila mtu kwenye maisha ana mipango yake na pesa zake na halazimishwi kupangiwa matumizi.

Fast-forward miaka kadhaa mbele, kwanza unashangaa huyu kaka yako anakutafuta halafu anakuwa kama analaumu mbona haumtafuti siku hizi. Halafu unakuja kusikia analeta story za wewe hauhudhurii vikao au msiba wa ndugu (kumbuka kuna misiba mingi umeenda na yeye haukumuona na kama ipo uliyokosa ni ile ilikukuta upo safari labda au mbali na eneo la msiba).

Mara kutokee harusi yeye akutafute muende wote kwenye kikao au atengeneze mazingira ya kutaka mkutane pub mpate kinywaji.

Mara usikie kuwa anakusema kuwa unaharibu pesa (ambazo hajui wala hana taarifa nazo[emoji23][emoji23][emoji23] anahisi tu kuwa unazo sababu aidha picha anazoona au kukuona sehemu fulani).

Mara aseme tuanzishe michango ya familia tuwe kama na mfuko wa kuchangia. Sasa unamuuliza tuchangie mfuko wa kazi gani kwani hapa sisi ni watu Baki si ni familia wewe ukiwa na shida bi mkubwa si huyu hapa au si utumie akiba zako. Anaanza kulaumu na kusema wewe hauna umoja na wenzako. [emoji23][emoji23] Sasa unajiuliza umoja gani huo ambao mwanzo haujaona umuhimu wake ila saa hii unaufosi tena kwa nguvu. Mimi siutaki maana nilipouhitaji haukuwapo so kama mtaunda umoja pambaneni nao mimi simo mimi ninao umoja wangu huku nje na nimeridhika nao maana nimeshasota sana sikuona faida ya umoja huu wenye sifa kama za Umoja wa Africa.

Kimsingi mtu anakuwa kama anakutafuta maneno na ukorofi ila unaamua kukausha unakaa mbali sasa anateseka sana. Sasa huyu ni m'moja na kuna dogo wa kike yeye ana akili za kifeminist mwehu si kidogo na nisivyowapenda wale wadudu ndio dogo anazidi kunichefua.

But watoto wao nipo nao vizuri na ndugu wapo ambao tunaelewana na hawana itikadi za kikuda na tunaishi fresh tu tukikutana amani imetawala. Shida ni ile unashangaa hawa wafamilia moja halafu wanaleta mambo meusi hii imekaaje.
 
Dah noma sana , sasa usiombe yule mwenye ushawishi mkubwa ndio akuoneshe dharau na aanze kuwaambukiza madogo kuwa hufai huna msaada wowote , madogo wanalipokea haraka mno. Mpaka waje waelewe ukweli umesota sana
Eeeh sasa hii ndio ilinikuta mimi. Mtu anakujengea mapicha picha mzazi hakuamini, madogo wanakuona umeyaparanganya, na ndugu wengine waliobakia nao wanakuwekea ganzi na mabunzi masikioni yaani mikausho ya sayari moja umbali kutoka sayari ya sita.

Mzee unakuwa kama Osama Marekani ukitokea tu unazinguliwa. Nikaona hapa isiwe shida kwann iwe nongwa wakati nje huko kuna raia wa kuishi nao na mambo yataenda tu.

Sasa wanakuwa wabakia wanataka kujua unafanya nini unajishughulisha na nini yaani wanataka kujua una maisha gani hawaoni pa kupatia taarifa, nikija home ni ile kama mwanga wa radi fasta paap nimetoweka hadi mwezi au miezi ijayo.

Lengo ni kukaa mbali na kutoendeleza makelele ambayo hayana msingi wowote sababu kama watu mnashindwa kaa na mwenzenu vizuri basi kaeni nae mbali kwa amani why sasa mnakuwa mnamfuatilia mambo yake ambayo mwanzo hakumtaka kuyaunga mkono na mliona hayana faida.

Sasa najua ni swala la muda tu kitaitishwa kikao cha familia. Hiyo siku nitaenda na jopo la mawakili kama kumi na mbili. Ntakodi noa mbili zinisindikize msafara wangu na kikosi cha ndugu kama 30 wawe baraza la wazee au jury. Nitavaa suti yangu ya kitambaa cha uturuki ili heshima iwepo wakati wa kuongea. Na hoja zangu nitatoa copy ili kila ninachokisema kiwe kwenye maandishi.

Na hiyo siku ndipo tutazungumza yote na nitawavua nguo kwa tabia zao ambazo zimepelekea yote haya. Na nitaweka masharti mazito sana kwao ambayo kama hayatafwatwa basi kutakuwa na vikwazo vya kijamii watavipata kutoka kwangu.

Kwasababu huwa sipendi upuuzi hata kidogo kwenye maisha yangu. Kama mimi ni mkorofi mbona huku nje naishi na raia freshi tu tukigombana ni ile ya kawaida tunamalizana na tunarudi kuwa pamoja. Why wao iwe shida.
 
Unaenda kwa wanao mtaani unawapa ya moyoni na kutubu sana. Wana wanaingia na huruma wanakushika mkono na hizo hizo buku buku za mawazo mixer kuingia madeni kwa niaba yako.
Mungu awabariki sana Wana👊
Huu uzi umenizungumzia mimi kabisa mkuu. Nilifungiwa mshahara na sikuwa na mishe yyte ya kunipa hela ila Wana walikuwa wananilea hadi nimekuja kaa sawa.
 
Eeeh sasa hii ndio ilinikuta mimi. Mtu anakujengea mapicha picha mzazi hakuamini, madogo wanakuona umeyaparanganya, na ndugu wengine waliobakia nao wanakuwekea ganzi na mabunzi masikioni yaani mikausho ya sayari moja umbali kutoka sayari ya sita.

Mzee unakuwa kama Osama Marekani ukitokea tu unazinguliwa. Nikaona hapa isiwe shida kwann iwe nongwa wakati nje huko kuna raia wa kuishi nao na mambo yataenda tu.

Sasa wanakuwa wabakia wanataka kujua unafanya nini unajishughulisha na nini yaani wanataka kujua una maisha gani hawaoni pa kupatia taarifa, nikija home ni ile kama mwanga wa radi fasta paap nimetoweka hadi mwezi au miezi ijayo.

Lengo ni kukaa mbali na kutoendeleza makelele ambayo hayana msingi wowote sababu kama watu mnashindwa kaa na mwenzenu vizuri basi kaeni nae mbali kwa amani why sasa mnakuwa mnamfuatilia mambo yake ambayo mwanzo hakumtaka kuyaunga mkono na mliona hayana faida.

Sasa najua ni swala la muda tu kitaitishwa kikao cha familia. Hiyo siku nitaenda na jopo la mawakili kama kumi na mbili. Ntakodi noa mbili zinisindikize msafara wangu na kikosi cha ndugu kama 30 wawe baraza la wazee au jury. Nitavaa suti yangu ya kitambaa cha uturuki ili heshima iwepo wakati wa kuongea. Na hoja zangu nitatoa copy ili kila ninachokisema kiwe kwenye maandishi.

Na hiyo siku ndipo tutazungumza yote na nitawavua nguo kwa tabia zao ambazo zimepelekea yote haya. Na nitaweka masharti mazito sana kwao ambayo kama hayatafwatwa basi kutakuwa na vikwazo vya kijamii watavipata kutoka kwangu.

Kwasababu huwa sipendi upuuzi hata kidogo kwenye maisha yangu. Kama mimi ni mkorofi mbona huku nje naishi na raia freshi tu tukigombana ni ile ya kawaida tunamalizana na tunarudi kuwa pamoja. Why wao iwe shida.
Àaah 😆😆, mimi japo sijawahi kugombana na mtu ila huwa siendi home bila sababu na naweza enda mara 1 kwa miaka 2 , nikienda ni usiku mchana sipo.
 
Ukiwa alosto huna mia ya kutu wanakukwepa. Kipindi kile cha kujitafuta ukiwapiga kirungu cha buku ya nauli au bundle ili uweze kufanya mawasiliano wanakupa majibu ya kilokole.

Utasikia asiefanya kazi na asile. Au, wewe una mikono miwili na miguu miwili na macho mawili unaomba walemavu wafanyaje. Hapo umeomba haujamfosi. Na bado ataenda kukupiga majungu kwa ndugu wengine na pamoja watakuchukulia poa sana mixer dharau za wazi wazi. Utatumwa hadi mafuta ya kupikia dukani ili mradi wakuonyeshe wewe hauna maana sasa kwenye familia.

Unakubaliana na hali maana kama Yesu mwana wa MUNGU aliteswa na wanadamu sembuse mimi. Unapiga moyo konde unasema ngoja ufosi kupambana na mitaa na walimwengu kuliko kupambana na ndugu ambao wamekuonyesha kuwa kumbe si muda wote damu ni nzito kuliko maji.

Unaenda kwa wanao mtaani unawapa ya moyoni na kutubu sana. Wana wanaingia na huruma wanakushika mkono na hizo hizo buku buku za mawazo mixer kuingia madeni kwa niaba yako.

Unajikaza unaweka mitego sawa, uhakika wa elfu 10,30,50 80 na hata laki kwa wiki na mwezi unakuwepo. Unalipa madeni unajiimarisha kiuchumi. Muda wa shukrani nawatafuta wanangu maana siwezi watupa maana ndio walinishika mkono gizani. Tunakula kitimoto pamoja na hata kusaidiana shida ndogo ndogo bila husuda.

Ndugu wanaona post, simu zao zinapigwa wanasema unajiweka mbali na familia siku hizi. Umepata mafanikio unakula na marafiki siku ukianguka hao hawatakubeba wala kukuuguza ni sisi ndugu zako wa damu.

Hapo ndipo unajua si muda wote damu ni nzito kuliko maji. Unaamua kupiga kimya tu sms za kikuda kama hizo haujibu unaamua kuwa outcast maana sometimes familia ndizo chanzo cha watu kukosa uelekeo badala kuwa chanzo cha uelekeo.

Haya maisha haya.
Well said mkuu
 
Hakuna anaekupangia maisha ila hapa hatuzingumzii kuingiliana mipango tunazungumzia tabia ushirika kati ya ndugu especially wa familia moja katika kuboresha maisha yao na kupiga hatua.

Unaona sasa mfano wewe, mdogo wako anakuomba laki 3 akanunue simu wewe unataka kwenda kununua kiwanja ukajenge. Umejua huyo mdogo wako anataka kufanya nini na hiyo simu? [emoji848]

Hapo umeassume tu kuwa dogo anataka kupata simu ya kuchat chat na mademu au kupost video TikTok na kufuatilia umbea Instagram. But unasahau kuwa kuna fursa mitandaoni huko kuliko mitaani ambazo pengine wewe hauzijui na hautaweza zifanya ila dogo ataweza fanya na zikamuingizia hata 40,000 kila siku na akawa vema hata kukushinda.

Niffer unamuona yule binti, alianza mdogo mdogo anauza vitu mtandaoni mama yake alimsapoti hakumpuuza kumpa sapoti hata yeye huwa anasema, leo unaona alipo? Mama yake alijua binti yangu atakuwa anaenda china na dubai kufunga mzigo wa mamilioni na kuwanyima usingizi watu wa kariakoo kwa simu tu? [emoji848]

Hizi sasa ndizo mentality za kichawi. Wewe umepata access ya kazi au biashara inakupa kipato cha kumudu maisha hata ya kumiliki kiwanja,kumpatia dogo laki 3 unaona adhabu na upo radhi umpotezee ili wewe ununue kiwanja ambacho probably unaweza usimalize ujenzi wake ndani hata ya miaka 10.

Dogo anakwenda kwa marafiki zake wakamkopesha simu au kumsapoti akapata namna ya kupata simu akaanza kuchangamkia mishe mishe zake MUNGU akamkunia nazi akapata cha kumkeep busy na kumpa kipato.

Utashangaa wewe na hivyo viwanja vyako mpo tu hapo na dogo ndie anakuja kukupa sapoti ya mifuko ya cement na akaja kuwa na kipato cha kumudu ujenzi wa nyumba akamaliza kabla yako na akapata nyumba zaidi ya tatu. Wewe ukamaliza ujenzi na ukashindwa kumudu maisha ukawa na nyumba lakini huna chakula ndani halafu huyu dogo akawa ndie tumaini kwako ukajinyenyekesha kwake ili akusapoti kwa chochote kitu.

Sasa usije chukia na yeye akakwambia sina laki 3 ya kukusaidia kwenda kupata matibabu ya hospital ila unamuona akienda kitambaa cheupe na rafiki zake wakila maisha na anateketeza zaidi ya milioni kwa wiki. Wewe unabakia kumsema na kumfitini kwa ndugu waliosalia.
Wapi nimesema simu ya kuchat chat?

Kwahiyo ulikuwa unashauri nisinunue kiwanja nimpe dogo akanunue simu? Ni msaidie dogo jambo lake langu atanisaidia nani?

Wewe unamawazo ya kilalamishi na asilimia 90% ya watu wa aina yako hawafanikiwi kwenye maisha.

Akili yako inawaza jambo lako tu haiwazi huyo unayemlalamikia ana jambo gani.

Mtu kupata ajira sio issue maana huyo mtu pia anamipango mfano mimi ni na mtoto na mke kila siku najibana nakula maharage nyama mara mojamija ili nifanye jambo langu labda nijenge au nilipe ada ya mwanangu.

Maisha yangu hayajastabilize nianze kuangaika na yako hivi hiyo ipo kweli? Atleast kuna wale watu ambao maisha yao yametengamaa tayari ameshajenga anasomesha hawa kweli wako na nafasi ya kusaidi.
 
Ndugu atabaki kuwa ndugu tu haijalishi amekutenda vipi. Mwangalie Joseph jinsi alivyofanyiwa fitina na ndugu zake kwenye biblia lakini hakulipa ubaya. Ukiona mtu anakufanyia ubaya wewe samehe maana kuna kitu kikubwa unacho ndiyo maana anakuchukia. Maisha ni mafupi tuishi kwa kuchukuliana na kusamehe ili watu wajifunze kwako siku ukiwa haupo.
 
Back
Top Bottom