[emoji849]
Kibongo bongo familia za aina hizo ni chache sana.
Ndo maana wengine tumeamua kua na zero expectations kutoka kwa ndugu, hii inasaidia kutokuwachukia pale unapoona kama hawakujali ipasavyo.
True mzee. Familia za upendo na amani ni chache sana aisee. Kuna familia hiyo hawana kitu mzee wao akafariki, akabakia bi mkubwa na vijana wake na mabinti. Mzee alikuwa na shamba mbili na kiwanja pale kinyerezi.
Mtoto mkubwa wa kiume wakakubaliana na mama yake wauze shamba moja kwa milioni 37 then wafanye maendeleo.
Bi mkubwa alikuwa anaumwa kansa na ilishamfika hatua mbaya akaona akakae huko kijijini kwao Tanga kwa ndugu zake. So kijana akawa amebakia kama kiongozi wa familia na pesa zote mikononi mwake. Lakini kutokana na upendo na utulivu walionao sijawahi kuona wakikorofishana na ni kama wamekubaliana kuwa huyo kaka yao asimamie show zote yeye. Hizo pesa atajua atafanya nini hawajaleta makelele.
Sasa nikawaza itokee kwenye aina hii ya familia kwanza hawatakubali hizo pesa zikae kwa yoyote wasema hebu hizi akae nazo mama. Na hapo sasa ni majungu na uchawa kwa bi mkubwa ili mwenye sumu kali dhidi ya wenzake ndie atatengeneza mazingira yeye ndie azipate.
Sasa ukitazama ni zile tabia za ubinafsi na uchoyo plus roho ya kwann ndizo hufanya baadhi ya familia zisiwe na maendeleo hata kama wazazi walipambana na kuwajenga watoto wao.
Unaweza kuta wamesomeshwa na hata kuendelezwa kibiashara na wana uwezo ila sasa kukaa chini na kusema sasa tuunde umoja wa kifamilia ili tupige hatua hapo sasa ndipo utashuhudia matabia ya kibinafsi yanaonekana.
Unakuta mtu mzima ila analeta ligi za kitoto kwenye familia. Ukisema ngoja nibadilishe furniture za home nimnunulie bi mkubwa electronics mpya na kadhalika. Mtu anaumia kabisa yaani na ni mama yenu wote, utaona anaumia yaani si kitu cha kuficha anaumia. Sasa unakuwa unajiuliza huyu ni mzima kiakili kweli? [emoji848]
Ukinunua vitu vya ndani ukaleta home ukatafuta na beki tatu ukamuweka, na kumpa maelekezo ya bajeti ili uweke mambo sawa unakuta ndugu yako wa kike mara na yeye katoka wapi huko sijui na yeye kaleta chakula wakati kile cha home ni cha kutosha, okay sio vibaya kaleta mzigo wa ziada wa chakula. Anaanza kumletea vituko dada wa kazi. Dada amepika wali yeye anapika ugali halafu anawaambia watoto wale ugali na watoto wanapenda wali. Yaani anapika chakula wakati kingine kimeshapikwa ili iweje, halafu bi mkubwa hakemei hii kitu.
Dada ananipigia simu ananiambia haya. Napiga simu home nauliza shida nini, bi mkubwa unaona anauma uma maneno tu. Unashindwa kuelewa.