Hii ndio Kigoma halisi, ukisikia nyingine ujue photocopy

Angetwambia Na yeye anatokea mkoa gani,ila ki ukweli ametudhalilisha,eti kwenda shule kwetu sio lazima???Dr Mpango na Prof Ndalichako Na wengine wengi wangepatikanaje Kama shule sisi haipandi?
anachoongea ni kweli..kwa watu wa kigoma shule sio lazima ila wapo waliosoma
 
Ngojea nipige kazi nikipata pesa ya madafu niende hilo eneo linaloitwa KALINZI nitafute bae wa kihutsu
 
Mk
mabesemct: 17918058 said:
Mkuu ulifanikiwa kuhudhuria disco pale Lake view au Kibo hall Kgm Mjini?
Mkuu pale like view ijumaa ndio uwa kuna disco na huduma zote uwa zinatolewa na watoto wa kirundi kuanzia counter mpaka kwenye mishkaki
 
Kuna tofauti kati ya kujua na kufahamu. Ungelipata mwenyeji wa Kigoma huenda ungeliijua Kigoma, kuliko unavyojaribu kudanganya watu kwa kuunganisha vijitukio na baadhi ya maeneo.
 
Pale unapata sato wa kilo moja kwa sh 2000
Nilishangaa sana mkuu mpaka nikawa najiuliza labda kuna kitu wananitegea, nilipo zoea nikaambiwa hata hiyo bei wanayoniuzia ni kwa kuwa walijua mimi mgeni,maana yake ningeweza pata kwa bei ya chini zaidi.
 
Sijui mleta Uzi anatoka mkoa gani, ila mikoa mingi Tanzania inafanana kwa maana ya Huduma.

Kuna maendeleo yamefikiwa kwa kiasi fulani hasa Kigoma mjini. Barabara za mjini zimeboreshwa sasa hivi, nilifika kwa Mara ya kwanza Kgm mwaka 2000. hali ni tofauti sana na sasa.

Vyakula bei kuwa kubwa hasa kwa Kigoma mjini ni sababu ya uhitaji mkubwa wa chakula DRC mashariki ambako kwa muda mrefu wako kwenye mapigano.

Ni kati ya mikoa inayojitosheleza kwa chakula. Mpunga,michikichi,maharage,mahindi lakini pia wana Samaki na dagaa toka ziwani Tanganyika.

Hifadhi ya gombe ambayo ipo kaskazini mwa mjini wa Kgm (50km),ipo kando kando ya ziwa Tanganyika na hakuna njia ya kufika hapo kwa urahisi zaidi ya boat. Hivyo basi ni kweli taxi driver anaweza asipajue huko labda ungeenda kibirizi kwa wavuvi na wasafirishaji maboti. Vivyo hivyo kwa hifadhi ya mahale ipo upande wa kusini wa mji wa Kigoma na ni pembezoni mwa ziwa Tanganyika na kufika huko ni kwa njia ya mjini( boti au MV liemba)

Kama ilivyo mikoa yote ya pembezoni, muingiliano wa watu ni mkubwa. Iwe wamakonde,wajaruo nk, sababu makabila mengi ya mpakani yanakuwa pia upande wa pili wa nchi!!

Kuna Lake Tanganyika Beach Hotel na Hilltop hotel, hizi ni hotel kubwa tu pia kuna lodge nzuri!

Jiografia ya mji ,sijui mleta Uzi alitarajia ifanane na wapi. Kila mji Uko tofauti kijiografia!!
 
Wadau huu mwaka nimepata bahati ya kutembelea mikoa kadhaa hapa nchini. Mkoa ulioniacha mdomo wazi ni Kigoma. Kwanza nilianza kushangaa mto Malagarasi kabla hata sijafika Kasulu, una mamba hatari mpaka nikakumbuka ule wimbo wa Idd Amin ulioimbwa enzi za vita kuashiria watavyomfanya wakakamata.

Kigoma mji mdogo sana tena halafu ramani yake hata haieleweki kutokana na miinuko katika ya mji, kuna mbuga inaitwa Gombe ipo km 50 tu mjini lakini 90% ya wenyeji hawajui ilipo wakiongozwa na madereva tax.

Kigoma wana stand mpya ya kisasa ambayo pia haina hata dustbin sijui taka zinatupwa wapi. Kutokana na udogo wa mji bajaji ni ruksa kufanya biashara popote wanapoweza hivyo kurahisisha suala la usafiri uwapo Kigoma. Asilimia kubwa ya wakazi na wafanyabiashara hapa mjini wanatoka Congo na Burundi.

Lami ya Kigoma inaanzia sehemu moja inaitwa Kidawa halafu inaishia Manyovu, mpakani kwingine kote ni vumbi . Kigoma inaongoza kwa kuuza vitu bei ghali sana, mfano kadet ya alafu 30 wao wanauza 55 ila cha ajabu ukifika Kasulu ni rahisi. Watu wengi wanaofanya biashara mjini wamejenga ndani ya barabara na hakuna tatizo, mfano maduka na bar nyingi zipo mita 15 toka katika ya barabara.

Wahudumu wengi kwenye haya maduka wanatoka Burundi kwa hiyo usishangae ukaenda hotelini ukamkuta mhudumu ni Mtutsi just mute serikali ya Kigoma inaruhusu. Kuna sehemu inaitwa Ujiji japokuwa ni sehemu maarufu ila inaongoza kwa nyumba za nyasi na pia ndipo sehemu waganga wengi walipo. Kule kuna nyumba zinaogopwa kumilikiwa sababu kila anayemiliki huwa anakufa hivyo zinabaki ka gofu.

Kuna kitu wanaita KIDONO hii ni chanjo fulani ambayo mtu ukishachanjiwa hata ukatwe panga kali vipi haukatiki ila pia masharti usile nyama ya mbuzi. Kijijini nako hali sio shwari nyumba zao hata iwe ya kisasa vipi hazifungwi lenta/Bim. Kijijini suala la kuoa wanawake wengi ni utamaduni waliorithi, unaweza oa kadiri uwezavyo na ukishaoa unatulia nyumbani mwanamke ndie anaenda shamba kulima analeta mnakula. Ukiwa na wake wengi ndivyo na mazao yanavyotiririka nyumbani na wakati mwingine mwanaume anachukua anaenda kuuza kidogo ili apate pesa ya kunywa pombe inayoitwa Kayogo.

Kijijini hakuna mwanamke anayekubali uzazi wa mpango maana wanaogopa kutimuliwa, suala la kusoma pia sio muhimu kwao labda itokee Mek ama weo akomalie ndio wanaenda shule. Kijijini pia nao hawapo nyuma kuwatumikisha warundi, huwa wanawaita KUBOTA. Wanawapeleka shamba wanawalimia kwa bei rahisi hivyo kuona ni nafuu zaidi japo kiusalama ni soo.

Wilaya kama Buhigwe na Kasulu wanalimisha Warundi sijui wanapenyaje mpakani pale. Kuna eneo linaitwa Kalinzi kwa wale wenzangu wanaoenda Ambrose Sinza, Buruguni Kimboka ama kwa babu mkifika Kigoma msisahau kuvisit ili eneo wapo watoto wa kitusi ka umeoa unaweza sahau familia yako, anyway mkumbuke UKIMWI.

Baada ya ziara ya kuchosha nilimpitia Zitto Mwandiga nikachukua mawese nikarudi zangu maana kule ukizubaa unaweza pigwa na radi na usijue imeshukaje maana miti haipo na wala hawana moyo wa kupanda. Tukutane Kagera next month
 
kigoma ni home lakini sijawahi kufika, itabidi niende nikapige misele aisee

na hizi ndege za magufuly zitakuwa zinafika kweli? maana sipendagi safari za kulala njiani, safari ya canada tulilala njiani nikachoka mpaka homa kidogo nikatapika vitu vya kijanikijani
 
Kitu kingine (watu)wanawake wa Kigoma hawajui kupika aisee, kupata chakula kizuri ni changamoto.
Kitu cha bei rahisi sana kigoma ni chumvu, nadhani kwakua inapatikana uvinza, hivyo wao kuzidisha chumvi kwnye chakula ni jambo la kawaida.
Wanawake wa kigoma hawako polite kabisaa.halafu sio wasafi.
Nazungumzia uzoefu nimfanyakazi wilaya zote za mkoa wa Kigoma.
Mnh
 
SABABU YA WAKIMBIZI MKUU. UMEINGIA NYARUGUSU PALE????? KUNA NGOs nyingi sana pe sijapata kuona.

Pale ndo nilielewa kwanini vita haiishi. Wazungu wanachochea moto ili watu wao wapate kazi.
Umeongea ukweli aisee. Pia hali niliyoiona hapo Nyarugusu pia nilisema vita haitaisha kamwe..maana mkimbizi haruhusiwi kurudi kwao kabisa na wanapewa kila kitu. Jamaa wa UN wanakula maisha kwa kwenda mbele. Nilifika hadi Kigadye nikagundua kumbe vita ya Burundi wazungu wanaichochea ili waweze kuishi. Ila wakimbizi hawana raha kabisa hasa kipindi cha mvua ndio utaona jinsi wanavyohangaika na magonjwa ,vyoo nk
SABABU YA WAKIMBIZI MKUU. UMEINGIA NYARUGUSU PALE????? KUNA NGOs nyingi sana pe sijapata kuona.

Pale ndo nilielewa kwanini vita haiishi. Wazungu wanachochea moto ili watu wao wapate kazi.
 
Mimi huwa nawapa heko wana kigoma wote kwa jitihada wanazofanya kujikwamua na umasikini. Endapo wangebweteka na kusema liwalo na liwe kama ilivyo kwa wazaramo nahisi kigoma inayoonekana Leo isingetazamika. Nasema hivi kwa sababu tangu Uhuru wa Tanganyika serikali haijawahi kufanya wala kufikiria swala lolote la kimaendeleo kwa mkoa wa Kigoma.

Kwa mpita njia anaweza akaibeza kigoma lakini ni moja kati ya mikoa ambayo ina watu ambao ni work harders.

Fikiria ni wafanya biashara wangapi wenye asili ya kigoma walioko mikoa mingine na wanafanya vizuri tu.

Haipingiki kwamba mkoa wa kigoma uko nyuma kimaendeleo lakini nadhani serikali ni chanzo kikubwa cha kuufanya mkoa huu usiendelee.
 
Wadau huu mwaka nimepata bahati ya kutembelea mikoa kadhaa hapa nchini. Mkoa ulioniacha mdomo wazi ni Kigoma. Kwanza nilianza kushangaa mto Malagarasi kabla hata sijafika Kasulu, una mamba hatari mpaka nikakumbuka ule wimbo wa Idd Amin ulioimbwa enzi za vita kuashiria watavyomfanya wakakamata.

Kigoma mji mdogo sana tena halafu ramani yake hata haieleweki kutokana na miinuko katika ya mji, kuna mbuga inaitwa Gombe ipo km 50 tu mjini lakini 90% ya wenyeji hawajui ilipo wakiongozwa na madereva tax.

Kigoma wana stand mpya ya kisasa ambayo pia haina hata dustbin sijui taka zinatupwa wapi. Kutokana na udogo wa mji bajaji ni ruksa kufanya biashara popote wanapoweza hivyo kurahisisha suala la usafiri uwapo Kigoma. Asilimia kubwa ya wakazi na wafanyabiashara hapa mjini wanatoka Congo na Burundi.

Lami ya Kigoma inaanzia sehemu moja inaitwa Kidawa halafu inaishia Manyovu, mpakani kwingine kote ni vumbi . Kigoma inaongoza kwa kuuza vitu bei ghali sana, mfano kadet ya alafu 30 wao wanauza 55 ila cha ajabu ukifika Kasulu ni rahisi. Watu wengi wanaofanya biashara mjini wamejenga ndani ya barabara na hakuna tatizo, mfano maduka na bar nyingi zipo mita 15 toka katika ya barabara.

Wahudumu wengi kwenye haya maduka wanatoka Burundi kwa hiyo usishangae ukaenda hotelini ukamkuta mhudumu ni Mtutsi just mute serikali ya Kigoma inaruhusu. Kuna sehemu inaitwa Ujiji japokuwa ni sehemu maarufu ila inaongoza kwa nyumba za nyasi na pia ndipo sehemu waganga wengi walipo. Kule kuna nyumba zinaogopwa kumilikiwa sababu kila anayemiliki huwa anakufa hivyo zinabaki ka gofu.

Kuna kitu wanaita KIDONO hii ni chanjo fulani ambayo mtu ukishachanjiwa hata ukatwe panga kali vipi haukatiki ila pia masharti usile nyama ya mbuzi. Kijijini nako hali sio shwari nyumba zao hata iwe ya kisasa vipi hazifungwi lenta/Bim. Kijijini suala la kuoa wanawake wengi ni utamaduni waliorithi, unaweza oa kadiri uwezavyo na ukishaoa unatulia nyumbani mwanamke ndie anaenda shamba kulima analeta mnakula. Ukiwa na wake wengi ndivyo na mazao yanavyotiririka nyumbani na wakati mwingine mwanaume anachukua anaenda kuuza kidogo ili apate pesa ya kunywa pombe inayoitwa Kayogo.

Kijijini hakuna mwanamke anayekubali uzazi wa mpango maana wanaogopa kutimuliwa, suala la kusoma pia sio muhimu kwao labda itokee Mek ama weo akomalie ndio wanaenda shule. Kijijini pia nao hawapo nyuma kuwatumikisha warundi, huwa wanawaita KUBOTA. Wanawapeleka shamba wanawalimia kwa bei rahisi hivyo kuona ni nafuu zaidi japo kiusalama ni soo.

Wilaya kama Buhigwe na Kasulu wanalimisha Warundi sijui wanapenyaje mpakani pale. Kuna eneo linaitwa Kalinzi kwa wale wenzangu wanaoenda Ambrose Sinza, Buruguni Kimboka ama kwa babu mkifika Kigoma msisahau kuvisit ili eneo wapo watoto wa kitusi ka umeoa unaweza sahau familia yako, anyway mkumbuke UKIMWI.

Baada ya ziara ya kuchosha nilimpitia Zitto Mwandiga nikachukua mawese nikarudi zangu maana kule ukizubaa unaweza pigwa na radi na usijue imeshukaje maana miti haipo na wala hawana moyo wa kupanda. Tukutane Kagera next month

1-Ni mkoa pekee ULIOBEBA JINA LA
NCHII TANGANYIKA zamani kigoma ilijulikana kwa jina la tanganyika waulize babuzako watakwmbia.
2- Ni mkoa pekee baada ya kwisha mkutano wa kamati kuu ya chama cha TAA 1954 Dsm kubadili madhumuni ya chama kutoka katk social na kuingia ktk politics ikazaliwa TANU. wajumbe hawajatawanyika wanapokea habari KIGOMA tayari wamekwisha pata ofisi ya TANU na Uongozi wote wa mkoa.(hapo ndipo mtawala alipoizungushia KGM dura nyukundu kimaendeleo).
Watafute wazee wazamani wa Tanu kama akina .mzee Bilali waikela wakueleze
3- Mkoa pekee uliotao wana Kandanda wengi machachari na mahiri
4- mkoa pekee uliotoa wanasiasa wengi machachari na mahiri
5- mkoa pekee uliotoa wanamuziki wengi machachari na mahiri.
 
Ndio mkoa pekee ambao ukitoka kijiji au wilaya moja kwenda nyingine usisahau kuvaa bukta au pensi ndani maana kuimba mtaji wa maskini ni nguvu zake na kuchezea mambata ya mgongo baada ya kutekwa sio vya kuuliza ni vya kufikia tuu!!

Umeniacha hoi nikakumbuka poli la asante nyerere,na malagalasi,yaliwakuta watu
 
Back
Top Bottom