Hii ndio Kigoma halisi, ukisikia nyingine ujue photocopy

Wadau huu mwaka nimepata bahati ya kutembelea mikoa kadhaa hapa nchini. Mkoa ulioniacha mdomo wazi ni Kigoma. Kwanza nilianza kushangaa mto Malagarasi kabla hata sijafika Kasulu, una mamba hatari mpaka nikakumbuka ule wimbo wa Idd Amin ulioimbwa enzi za vita kuashiria watavyomfanya wakakamata.

Kigoma mji mdogo sana tena halafu ramani yake hata haieleweki kutokana na miinuko katika ya mji, kuna mbuga inaitwa Gombe ipo km 50 tu mjini lakini 90% ya wenyeji hawajui ilipo wakiongozwa na madereva tax.

Kigoma wana stand mpya ya kisasa ambayo pia haina hata dustbin sijui taka zinatupwa wapi. Kutokana na udogo wa mji bajaji ni ruksa kufanya biashara popote wanapoweza hivyo kurahisisha suala la usafiri uwapo Kigoma. Asilimia kubwa ya wakazi na wafanyabiashara hapa mjini wanatoka Congo na Burundi.

Lami ya Kigoma inaanzia sehemu moja inaitwa Kidawa halafu inaishia Manyovu, mpakani kwingine kote ni vumbi . Kigoma inaongoza kwa kuuza vitu bei ghali sana, mfano kadet ya alafu 30 wao wanauza 55 ila cha ajabu ukifika Kasulu ni rahisi. Watu wengi wanaofanya biashara mjini wamejenga ndani ya barabara na hakuna tatizo, mfano maduka na bar nyingi zipo mita 15 toka katika ya barabara.

Wahudumu wengi kwenye haya maduka wanatoka Burundi kwa hiyo usishangae ukaenda hotelini ukamkuta mhudumu ni Mtutsi just mute serikali ya Kigoma inaruhusu. Kuna sehemu inaitwa Ujiji japokuwa ni sehemu maarufu ila inaongoza kwa nyumba za nyasi na pia ndipo sehemu waganga wengi walipo. Kule kuna nyumba zinaogopwa kumilikiwa sababu kila anayemiliki huwa anakufa hivyo zinabaki ka gofu.

Kuna kitu wanaita KIDONO hii ni chanjo fulani ambayo mtu ukishachanjiwa hata ukatwe panga kali vipi haukatiki ila pia masharti usile nyama ya mbuzi. Kijijini nako hali sio shwari nyumba zao hata iwe ya kisasa vipi hazifungwi lenta/Bim. Kijijini suala la kuoa wanawake wengi ni utamaduni waliorithi, unaweza oa kadiri uwezavyo na ukishaoa unatulia nyumbani mwanamke ndie anaenda shamba kulima analeta mnakula. Ukiwa na wake wengi ndivyo na mazao yanavyotiririka nyumbani na wakati mwingine mwanaume anachukua anaenda kuuza kidogo ili apate pesa ya kunywa pombe inayoitwa Kayogo.

Kijijini hakuna mwanamke anayekubali uzazi wa mpango maana wanaogopa kutimuliwa, suala la kusoma pia sio muhimu kwao labda itokee Mek ama weo akomalie ndio wanaenda shule. Kijijini pia nao hawapo nyuma kuwatumikisha warundi, huwa wanawaita KUBOTA. Wanawapeleka shamba wanawalimia kwa bei rahisi hivyo kuona ni nafuu zaidi japo kiusalama ni soo.

Wilaya kama Buhigwe na Kasulu wanalimisha Warundi sijui wanapenyaje mpakani pale. Kuna eneo linaitwa Kalinzi kwa wale wenzangu wanaoenda Ambrose Sinza, Buruguni Kimboka ama kwa babu mkifika Kigoma msisahau kuvisit ili eneo wapo watoto wa kitusi ka umeoa unaweza sahau familia yako, anyway mkumbuke UKIMWI.

Baada ya ziara ya kuchosha nilimpitia Zitto Mwandiga nikachukua mawese nikarudi zangu maana kule ukizubaa unaweza pigwa na radi na usijue imeshukaje maana miti haipo na wala hawana moyo wa kupanda. Tukutane Kagera next month
Mkuu umesema vyema. Naomba nikurekebishe kwa machache.
Sehemu lami inapoanzia ukitokea kasulu panaitwa Kidhawe
Lami ipo mto malagarasi darajani kisha inakuja kuanzia tenauvinza ukiwa unatokea Tabora.
Mengine yote ulosema ni ukweli kabisa. Ila ungeweka kidono ni kizuri sana mkuu. Karibu Mwandiga
 
Iviligwa Kasulu Jamaa !
Ntore,Nzambagiza,Nswa,
Mitaa Sasa Kama Ulaya Murusi
Kwashayo,Mwilamvya,Kimobwa,Bogwe,Kumnyika,

Kikwete Bridge Mbele Pale Mulyabhibhi
 
Kuna center inaitwa Nguruka Samaki wake wako poa sana
Hahahahaha! Hapo aisee samaki ni wazuri ila kwa wezi Nguruka ni balaa siku za nyuma nakumbuka treni ikikaribia eneo hili mizigo ya karibu na dirisha abiria wanaitoa kuhofia wezi.
 
Yapo umeongea ni kweli mengine ni uongo uliokubuhu.

1. Siyo kweli kwamba wahudumu kwenye bar, hotel na maduka ni warundi. Ukweli ni watanzania, maana kuwa na mrundi kama ulivyosema ni soo. Lkn wapo waliopenya warundi na wazaire wapo mjini kigoma.

2. Pili, ndoa za mitara zipo kwa jamii za waislam, lkn ukija maeneo ya kasulu mitara siyo mingi.

3. Nyumba za mijini asilimia kubwa zina renta lkn za vijijini hazina. Sababu ni ujenzi wa tofari mbili na hazijawahi sababisha madhara.

4. Barabara ya lami ipo maeneo baadhi ya toka tabora kuja kigoma kupitia uvinza. Kidhwe kasulu hadi kibondo na nyakanazi ni vumbi tu. Tunamtegemea magufuri

5. Kasulu ni mji wa kibiashara, hivyo wafanyabiashara baadhi wa urambo, kaliuwa, kgm mjini, burundi na Kbondo, huchukulia bidhaa pale. Kgm mjini ni ghali sana.

6. Ramni ya kigoma iko wazi, hukuielewa sababu wewe sio geographer.

7. Ujenzi kwenye hifadhi ya barabara ni kwa sababu hapakuwahi kuwa na miradi ya ujenzi

8. Uzazi wa mpango upo, sijui umetembelea kijiji gani.

9. Miti siku za hivi karibuni wameanza kupanda. Zamani waliothamini walikuwa ni wenyeji wa heru na manyovu(buhigwe). Lkn baada ya kuvuna miti maeneo ya mashariki mwa mkoa, nao siku hizi wameamza upandaji wa miti ya mbao. Ukienda Kasulu pembeni ya mto bogwe utaona vitalu vya kutosha vya miti.
Penye ukweli tuseme ukweli mkubwa.
1. Wapo warundi wahudumu na wanaojiuza. Usibishe. Uhamiaji mara nyingi wanapambana nao.
2. Ndo za mitala zipo sana tu. Kasulu pia zipo tena hadi wazee wa kanisa hapo Mwilamvya na Haya ya mjini wana wake zaidi ya mmoja. Sema tu huyu mke wa puli na kuendelea anakuwa hatambuliki kikanisa ila yupo na watoto. Njoo hapa Mwandiga ndio balaa japo wengi ni waislm lakini hili jambo lipo.
3. Baadi ya nyumba za mjini hazina lents. Hasa hizi wanaojenga sasa hv ndio za kisasa ila majority ya nyumba za zamani hazina lenta
5. Namba tano upo sahihi kabisa.
6. Upo sahihi
7. Hiyo sio sababu. Kama Tanroads wapo wanahifadhi yao ya barabara.
8. Hili la uzazi wa mpango sijui nisemeje. Labda wewe utupe maana ya uzazi wa mpango unavyoelewa. Kuwa na watoto 12 waliopishana mwaka mmoja mmoja au wenye umri sawa kwa watoto wa bi mdogo na mkubwa ni kawaida. Kila mtoto anakuja na bahati yake bwana. Huku tunazaa hadi waishe. Hawatalala njaa watoto. Tumejaliwa ardhi yenye mazao.
9upo sahihi.
Tuseme ukweli kigoma yetu na utamaduni wetu. Nyie ndio mnaogopa kusema ni waha mkifika huko dar.
 
Mkuu najua unabisha ila mie nilienda kiutafiti zaidi, na nimefuata barabara inayotumika sana subiri nitapoleta report ya kila wilaya utaelewa kwanini vitu vingi nilificha. Unapotaja kote nimepasurvey na usibishe kuwa hakuna warundi wanaofanya kazi tena na kiswahili wanajua vizuri ila ukiongea half an hour utagundua, sasa nakupa sehemu mbili za kwenda kujihakikishia ili uhamini. Kuna wafanyabiashara wawili wa maduka ya jumla na ndio wanasambaza sukari mkoa mzima ukikosa kwao basi ujue hamna sukari. Wanaopanga sukari kwenye godown semi zikifika ni watu toka kwa nkurunziza. Nenda pale like view anzia kaunta kabisa alafu kwa wahudumu wa kawaida. Tukutane Kagera next month
Hiyo lake view ni ya mrundi. Sijafika kigoma bt
Rafiki yangu anamjua mmiliki, ila anaishi Tanzania huyo mrundi sasa

Mengine sijui kama raia tayar ama la
 
Mifano mengine haina mashiko,wazaramo hawajabweteka, wanatumia akili ndio maana mkoa wa Dar na Pwani ndio mikoa iliyotajwa kuwa tajiri na watu wenye kipato.Huwezi kumfananisha kimaisha mtu anayeishi huko kijijinii Kigoma na anayeishi Dar es salaaam, alafu hao unaowataja wana jitihada ya kujikwamua na umaskini ndio mkoa unaongoza kwa umaskini wa kutupwa.Tatizo watu wa mikoani mnadhani umaskini unaisha kwa kufanya kazi ngumu na kulima na ndio maana mnaishia kuwa maskini daima kwa sababu nguvu inatumika zaidi.Mkishakuja kutumikishwa kazi mjini mnaenda kusimulia wadar es salaam wavivu
Ûtajiri wa dar haujaletwa na wazaramo usituongopee, hao unaowaita wamikoani kama hao wakigoma ndio wafanyabiashara wakubwa,wachaga,wapare, wakinga,nenda kariakoo kuna wazaramo pale ?wengi ndio wanaotumikishwa
 
Back
Top Bottom