Hii ndio Kigoma halisi, ukisikia nyingine ujue photocopy

Ukitembelea soko la watumwa pale ujiji ni kituko kingine cha mji wa kigoma.huezi amini kua ndo lililokua soko la watumwa,watu wananya biashara hovyohovyo pale sokoni.nilikua huko miaka minne iliyopitaa
 
Kitu kingine kinachoshangaza gari za DFP na UNHCR ni nyingi kuliko magari ya kawaida kiasi kwamba unaweza kuhisi plate no. za Kigoma ni tofauti na sehemu nyingine
Mkuu, kwa uzoefu wako, Je wanaofanya kazi kwenye kambi za wakimbizi hali zao kiusalama,kiuchumi na kijamii zikoje? Ningependa kufanya kazi hizi japo kwa muda fulani wa maisha yangu yaliyosalia duniani..
 
mkuu sina uzoefu na hizo kazi. Nilienda Kigoma kwa issues nyingine. Natumaini wazoefu watakupa maoni stahiki.

Ila staff wa UNHCR nawaona wapo poa tu na kifedha wapo vizuri sana.
 
Wadau huu mwaka nimepata bahati ya kutembelea mikoa kadhaa hapa nchini. Mkoa ulioniacha mdomo wazi ni Kigoma. Kwanza nilianza kushangaa mto Malagarasi kabla hata sijafika Kasulu, una mamba hatari mpaka nikakumbuka ule wimbo wa Idd Amin ulioimbwa enzi za vita kuashiria watavyomfanya wakakamata.

Kigoma mji mdogo sana tena halafu ramani yake hata haieleweki kutokana na miinuko katika ya mji, kuna mbuga inaitwa Gombe ipo km 50 tu mjini lakini 90% ya wenyeji hawajui ilipo wakiongozwa na madereva tax.

Kigoma wana stand mpya ya kisasa ambayo pia haina hata dustbin sijui taka zinatupwa wapi. Kutokana na udogo wa mji bajaji ni ruksa kufanya biashara popote wanapoweza hivyo kurahisisha suala la usafiri uwapo Kigoma. Asilimia kubwa ya wakazi na wafanyabiashara hapa mjini wanatoka Congo na Burundi.

Lami ya Kigoma inaanzia sehemu moja inaitwa Kidawa halafu inaishia Manyovu, mpakani kwingine kote ni vumbi . Kigoma inaongoza kwa kuuza vitu bei ghali sana, mfano kadet ya alafu 30 wao wanauza 55 ila cha ajabu ukifika Kasulu ni rahisi. Watu wengi wanaofanya biashara mjini wamejenga ndani ya barabara na hakuna tatizo, mfano maduka na bar nyingi zipo mita 15 toka katika ya barabara.

Wahudumu wengi kwenye haya maduka wanatoka Burundi kwa hiyo usishangae ukaenda hotelini ukamkuta mhudumu ni Mtutsi just mute serikali ya Kigoma inaruhusu. Kuna sehemu inaitwa Ujiji japokuwa ni sehemu maarufu ila inaongoza kwa nyumba za nyasi na pia ndipo sehemu waganga wengi walipo. Kule kuna nyumba zinaogopwa kumilikiwa sababu kila anayemiliki huwa anakufa hivyo zinabaki ka gofu.

Kuna kitu wanaita KIDONO hii ni chanjo fulani ambayo mtu ukishachanjiwa hata ukatwe panga kali vipi haukatiki ila pia masharti usile nyama ya mbuzi. Kijijini nako hali sio shwari nyumba zao hata iwe ya kisasa vipi hazifungwi lenta/Bim. Kijijini suala la kuoa wanawake wengi ni utamaduni waliorithi, unaweza oa kadiri uwezavyo na ukishaoa unatulia nyumbani mwanamke ndie anaenda shamba kulima analeta mnakula. Ukiwa na wake wengi ndivyo na mazao yanavyotiririka nyumbani na wakati mwingine mwanaume anachukua anaenda kuuza kidogo ili apate pesa ya kunywa pombe inayoitwa Kayogo.

Kijijini hakuna mwanamke anayekubali uzazi wa mpango maana wanaogopa kutimuliwa, suala la kusoma pia sio muhimu kwao labda itokee Mek ama weo akomalie ndio wanaenda shule. Kijijini pia nao hawapo nyuma kuwatumikisha warundi, huwa wanawaita KUBOTA. Wanawapeleka shamba wanawalimia kwa bei rahisi hivyo kuona ni nafuu zaidi japo kiusalama ni soo.

Wilaya kama Buhigwe na Kasulu wanalimisha Warundi sijui wanapenyaje mpakani pale. Kuna eneo linaitwa Kalinzi kwa wale wenzangu wanaoenda Ambrose Sinza, Buruguni Kimboka ama kwa babu mkifika Kigoma msisahau kuvisit ili eneo wapo watoto wa kitusi ka umeoa unaweza sahau familia yako, anyway mkumbuke UKIMWI.

Baada ya ziara ya kuchosha nilimpitia Zitto Mwandiga nikachukua mawese nikarudi zangu maana kule ukizubaa unaweza pigwa na radi na usijue imeshukaje maana miti haipo na wala hawana moyo wa kupanda. Tukutane Kagera next month
Wewe kwenu wapi?
 
Mkuu ulifanikiwa kuhudhuria disco pale Lake view au Kibo hall Kgm Mjini?
 
Heee umegusia mkoa Wangu umeandika sana japo wewe umejikita kwenye
1. Ukabila
2. Ngono
3.Ubaya ila uzuri wake hujaandika
4.Dharau
Ngoja niache ila taja mkoa wako tukupe sifa nzuri na mbaya
 
Mkuu mr.loner hukubahatika kuchukua migebuka?. Nitakwenda Kigoma kuchukua dagaa na migebuka mwezi ujao.
 
mtoa mada ametukashfu waha na wnakigoma hakika kalaniwa tayari yaan cha msing alichoongea ni kua hamna maendeleo vtu bei ghali
 
Ndio maana mbunge mmoja aliitoa Kigoma Tz.Ila tueleze na mazuri yake ili tukatembelee.
 
Angetwambia Na yeye anatokea mkoa gani,ila ki ukweli ametudhalilisha,eti kwenda shule kwetu sio lazima???Dr Mpango na Prof Ndalichako Na wengine wengi wangepatikanaje Kama shule sisi haipandi?
 
Mkuu

Hizi za UN niliziona nyingi sana na hazisimamishwi na trafiki mpaka nikahisi ndio zinaingiza warundi kinyemela, cha ajabu pia mali za UN utakuta mtaani zinauzwa kiholela na hawachukuliwi hatua, mfano taa za sola, maturubali sufuria nk

SABABU YA WAKIMBIZI MKUU. UMEINGIA NYARUGUSU PALE????? KUNA NGOs nyingi sana pe sijapata kuona.

Pale ndo nilielewa kwanini vita haiishi. Wazungu wanachochea moto ili watu wao wapate kazi.
 
Mkuu umenikumbusha hapo kidawe kuna mishikaki inauzwa hapo na ugali umefungwa kwenye majani ya migomba sijui unaitwaje vile "maloya" kama sijakosea vile.
 
Kitu kingine (watu)wanawake wa Kigoma hawajui kupika aisee, kupata chakula kizuri ni changamoto.
Kitu cha bei rahisi sana kigoma ni chumvu, nadhani kwakua inapatikana uvinza, hivyo wao kuzidisha chumvi kwnye chakula ni jambo la kawaida.
Wanawake wa kigoma hawako polite kabisaa.halafu sio wasafi.
Nazungumzia uzoefu nimfanyakazi wilaya zote za mkoa wa Kigoma.
 
Hongera sana KWA kubahatisha kufika kigoma, ila umesahau kutuhabarisha kuhusu SAMAKI wa ziwa Tanganyika maana wapo wengi, mmoja wapo ana miiba mingi sana ila jina lake nimelisahau.
 
Kitu kingine (watu)wanawake wa Kigoma hawajui kupika aisee, kupata chakula kizuri ni changamoto.
Kitu cha bei rahisi sana kigoma ni chumvu, nadhani kwakua inapatikana uvinza, hivyo wao kuzidisha chumvi kwnye chakula ni jambo la kawaida.
Wanawake wa kigoma hawako polite kabisaa.halafu sio wasafi.
Nazungumzia uzoefu nimfanyakazi wilaya zote za mkoa wa Kigoma.
Wachafu pia wako mkoa wa mara
 
Back
Top Bottom