englibertm
JF-Expert Member
- May 1, 2009
- 9,252
- 6,208
Mpendwa Lei' za asubuhi? Wajua kuwa M/mungu hapendi dha'naa mbovu na tuhuma bila kuwa na uhakika.Hiki alichokuwa anakifanya Iddi Amin kilikuwa hakina faida wala hasara, hawa wazungu walioitwa Tanzania kama wawekezaji tumeshindwa kuwadhibiti wanatuibia rasilmali zetu mchana kweupee kiasi kwamba wanatuona kama mabwege.
Nina wasiwasi huenda kuna wazawa hasa viongozi ambao wananufaika binafsi na sio taifa na ndio maana wamekaa kimya, kama nawasingizia Mungu anisamehe lakini kama kuna ukweli basi kilio cha watanzania kitamfikia Mungu siku moja.