Hii ndio Iringa halisi na watu wake

Hii ndio Iringa halisi na watu wake

ULANZI (Bamboo wine) ni Pombe maarufu mkoani iringa,
Naweza sema ndio pombe inayopendwa zaidi na wenyeji wa mkoa wa iringa tangu enzi.
View attachment 465546View attachment 465547

Ulanzi hufanyika kwa kuchachusha (fermentation) utomvu (sap) unaotokana na mmea mchana wa Muanzi (young bamboo shoot)
View attachment 465545

Hapa namaanisha, kimiminika hiki ni chakula kizuri kwa vijidudu (bacteria) vya kuchachusha ambayo huifanya kuwa pombe baada ya Massa matano hadi 12 baada ya kugemwa,

Hususani Msimu wa mvua ambapo maji ni mengi zaidi ardhin, Mmea mchanga wa mwanzi hukatwa kwa juu (at the tip) kisha hufungwa taping container (tunaita MBETA), asubuhi na mapema mgema hufika shambani kwake kukusanya ulanzi kutoka kwenye hizi containers, husafisha ile tip kwa kisu kikali (KUPYATILA) na huzisafisha vizuri containers na kuzirudishia mahala pake kwa ajili ya siku inayofuata.
View attachment 465548View attachment 465549View attachment 465550
I have been using it since then. Try it, its a very nice local wine,
Trust me.
View attachment 465551
Dah... Na hili ndiyo Tatizo kuu la Iringa/Njombe...Pombe. Niliwahi kupata deiwaka Njombe ...hadi kufikia mchana nilikuwa nimewatimua wasaidizi wote 9 kwa sababu ya ulevi.... Cha kushangaza nilipoingia kiwandani nilimuona opereta mmoja akiendesha mtambo huku akiwa na galoni ya ulanzi tena mbele wasimamizi wake....nilipouliza nikajibiwa Ile ni "chai" imeruhusiwa.. Nikachoka kabisa...
 
Mh..IRINGA kuzuri aisee...ila naski baridi ndo KIBOKO yao
Usidanganywe na hizo picha, hizo picha ndio key areas. Maisha ya iringa yapo expensive sana, ni mkoa ambao hata huduma za kawaida bado ni changamoto. Labda hali ya ubaridi kwa baadhi ya miezi, otherwise ni aheri hata Moro kuliko iringa
 
Dah.... Alama pekee ya kumtambulisha mtoto wa Iringa ni Ile urembo pembeni ya macho... Wenyewe wanaita 11....kama huna basi wewe ni sawa mzaramo aliyekimbia joto la Dar na kuja kujificha Iringa
Zinaitwa chale. Aisee hizo mi nilifatilia maana nikaambiwa mbili. Moja mtoto akizaliwa ana makengeza anachanjwa na wembe pembeni ya macho na kuwekwa dawa, kadiri anavyokua makengeza hupotea .
2) urembo: wasichana wa zamani ambao wengi wao kwa sasa ni wamama watu wazima au wabibi, walikuwa wanachuma majani fulani na kubandika pembezoni mwa macho kwa namna ya pekee, sijajua walifanyaje fanyaje hadi alama za majani zikawa za kudumu katika maisha yao. Ila kwa sasa ni ngumu sana kumkuta binti wa kihehe akiwa na urembo huoo sana sana utamuona na chale za kutibu makengeza
 
Usidanganywe na hizo picha, hizo picha ndio key areas. Maisha ya iringa yapo expensive sana, ni mkoa ambao hata huduma za kawaida bado ni changamoto. Labda hali ya ubaridi kwa baadhi ya miezi, otherwise ni aheri hata Moro kuliko iringa
Acha wivu Mluguru wewe!
 
Iringa ina wilaya 3. Iringa, Kilolo na Mufindi. Vyuo ni Mkwawa, RUCU, KLERUU, IUCO, IREBUKO, CHUO CHA AFYA, USTAWI WA JAMII, N.K
 
Hata Dibo mwenyewe kapapenda nae pamempenda! Dar vurugu sana! Vipi uwanja wetu wa Nduli kuna traffic ya kutosha ya kujia ndege!
Huu uwanja wetu bado haujapewa kipaumbele, Mbunge Msigwa achukue hii changamoto.
We need to Market Ruaha National Park, ili taifa lipate pesa zaidi na wana iringa tunufaike na hifadhi yetu hii,
Hapa namaanisha tunahitaji kuboresha uwanja wa ndege wa nduli pamoja na hotels hapa iringa,
Nimeskia Barbara ya Iringa- ruaha national park inakuwa upgraded ila sijui ni Lini.

Kuna mbunge mwingine wa Kilolo anaitwa Venance Mwamoto, huyu jamaa bado yupo kwenye usingizi wa pono, hakuna kitu anaweza wasaidia watu wake.

At least tunahitaji proactive leaders, to push and get things done. Hongera kwako Msigwa. Do it More, we need Numbers!
 
Vipi mkuu habari za mlo WA mbwa... Au ni vijijjni tu... Nilikaa iringa wiki moja.. Nilitaraji kukutana na barid Kali lakini kumbe kawaida tu labda haikuwa msimu wake.
 
Nimeipenda sana.Ila mkuu Mkoa wa Iringa una wilaya tatu. Wilaya ya Iringa (Manispaa na iringa Vijijini Mkuu wa wilaya ni Kasesera). Wilaya ya Kilolo na Wilaya ya Mufundi( Mufundi na mafinga)
 
Iringa ina wilaya 3. Iringa, Kilolo na Mufindi. Vyuo ni Mkwawa, RUCU, KLERUU, IUCO, IREBUKO, CHUO CHA AFYA, USTAWI WA JAMII, N.K
IMG_20170221_195819_347.jpg
IMG_20170221_195934_815.jpg
 
Huu uwanja wetu bado haujapewa kipaumbele, Mbunge Msigwa achukue hii changamoto.
We need to Market Ruaha National Park, ili taifa lipate pesa zaidi na wana iringa tunufaike na hifadhi yetu hii,
Hapa namaanisha tunahitaji kuboresha uwanja wa ndege wa nduli pamoja na hotels hapa iringa,
Nimeskia Barbara ya Iringa- ruaha national park inakuwa upgraded ila sijui ni Lini.

Kuna mbunge mwingine wa Kilolo anaitwa Venance Mwamoto, huyu jamaa bado yupo kwenye usingizi wa pono, hakuna kitu anaweza wasaidia watu wake.

At least tunahitaji proactive leaders, to push and get things done. Hongera kwako Msigwa. Do it More, we need Numbers!
Huo uwanja kila kitu kipo tiyari, utakuwa na run way ya 3km, ni magufuli ndo anataka ujengwe na yeye ndo alikuwa anasubiriwa aje aweke jiwe la msingi, bahati mbaya ziara yake inahairishwa mara kwa mara
 
Habari njema sana hii mkuu, asante kwa update!
 
Back
Top Bottom