Hii ndio Dini Kongwe Duniani

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,064
Reaction score
2,590
Kwa mahesabu ya Biblia mpaka sasa Dunia ina miaka 6000. Kwa maana hiyo, tukianza na dini kongwe inaonyesha kuwa kuna miaka 1000 watu waliishi bila dini. Hawakuwa na hizi dini ila walimuabudu Mungu na shetani. Miaka 1000 baadaye hatimaye dini ya kwanza ikaanzishwa, hii ilianzishwa mwaka 5000 kabla ya Kristo, na dini hiyo ilikuwa Hinduism(wahindu) leo hii dini hii ina wafuasi wake bilioni 1.1 mwanzilishi hajulikani.
Judaism: Hii dini ilianzishwa na Ibrahim miaka 3000 kabla ya Kristo. Leo hii dini hii ina wafuasi wapatao milioni 14
Zoloastrianism: Hii dini ilianzishwa miaka 1500 kabla ya Kristo na mtu alieitwa Zarathustra. Leo hii dini hii ina wafuasi milioni 2.6
Jainism: Hii dini ilianzishwa na mtu alieitwa Rishabhadeva.Ilianzishwa miaka 900 kabla ya Kristo. Leo hii ina wafuasi milioni 4.2
Buddhism: Hii dini ilianzishwa miaka 500 kabla ya Kristo na mtu aliyeitwa Siddhartha Gautama. Leo hii ina wafuasi milioni 506
Confucianism: Hii dini ilianzishwa miaka 500 kabla ya Kristo na jamaa aliyeitwa Confucius na leo hii ina wafuasi milioni 6.1
Ukristo: Hii dini ilianzishwa miaka 30 baada ya Kristo. Leo hii ina wafuasi bilioni 2.3 Wa Kristo (Yaani watu waliofuata Kristo)
Uislamu: Hii dini ilianzishwa miaka 610 baada ya Kristo ilianzishwa na mtume Muhammad mwaka 610 baada ya Kristo. Leo hii ina wafuasi bilioni 1.9

NB: MUNGU HAJAWAHI KUANZISHA DINI, NA HANA DINI NA HAKUNA DINI ILIYOANZISHWA NA MUNGU NA NDIO MAANA ANAMJIBU KILA AMUOMBAYE KWA DINI YAKE.
 
Biblia ambacho ni kitabu cha wakristo umemtaja shetani.Ukriso ulianza pale shetani alipiasi
 
Ukristo: Hii dini ilianzishwa miaka 30 baada ya Kristo.
Naomba ufafanuzi kwanini ukristo umeanzishwa miaka 30 baadae na si wakati wa uhai wake?.
Hinduism(wahindu) leo hii dini hii ina wafuasi wake bilioni 1.1 mwanzilishi hajulikani.
Hapa pia nina swali kwanini muanzilishi hajulikani manake dini pekee hapa ulizo andika hii tu haina muanzilishi.
 
Atheist wameanza lini? na mwasisi ni nani? na wana wafuasi wangapi?
Yoda Kiranga kujeni mtoe mwongozo!
Ilikuwepo kwenye jamii zilizostaarabika kama ugiriki na india, kabla hata ya Yesu.

Kwenye Middle ages, udini ulikuwa mkali falsafa ikapotea. Ilikuja kurudi karne ya 18 kwenye kipindi cha enlightenment cha ulaya.

Kwa kuwa atheism sio imani, hakuna taasisi ya kuisimamia. Hivyo inakisiwa atheists tupo 200-500m, wengi wakiwa wachina.

Japo inasemekana wasiofungamana na dini wapo zaidi ya bilioni 1.
 
Tufanye umeanza alipoumbwa mwanadamu...
Binadamu wa kisasa wamekuwepo duniani kwa miaka 300,000 na dini wameanza kuwa nazo miaka 50,000 iliyopita, swali la msingi ni kwa nini binadamu alianza kuwa na imani au dini.
 
Naomba ufafanuzi kwanini ukristo umeanzishwa miaka 30 baadae na si wakati wa uhai wake?.

Hapa pia nina swali kwanini muanzilishi hajulikani manake dini pekee hapa ulizo andika hii tu haina muanzilishi.
Hinduism ni mkusanyiko wa Mila, Imani na falsafa mbalimbali za India kwahiyo haina muanzilishi mmoja kama hizo DINI nyingine ndo maana hajulikani.
 
Atheists ni default setting ya binadamu,
Binadamu wote huzaliwa wakiwa atheists halafu baadaye ndio wanakuwa brainwashed na dini za wazazi wao na jamii zao.
Ukiwa hujui chochote unakuwa atheist?
 
Atheists ni default setting ya binadamu,
Binadamu wote huzaliwa wakiwa atheists halafu baadaye ndio wanakuwa brainwashed na dini za wazazi wao na jamii zao.
Very good explanation
 
Binadamu wa kisasa wamekuwepo duniani kwa miaka 300,000 na dini wameanza kuwa nazo miaka 50,000 iliyopita, swali la msingi ni kwa nini binadamu alianza kuwa na imani au dini.
Hapa wanasayansi mnaniachaga hoi kwamba miaka 300k?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…