Kula matunda tu uone Kama yanakaa huko tumboni,kwanza minyoo tu unakuta wanaingia kwenye mgogoro wakimaliza kupigana wanakaa kikao wanazira kula hayo matunda wanaanza kula utumbo wako..😂
Hayo maisha ni mtu fulani uwe nazo halafu swala la maji Aisee kunywa tu lita tatu asubuhi si mchezo ati!,akili yote inahamia kukojoa serious unywe maji Lita tatu halafu ukakimbie hapo huna haja ya kuwa na muziki tumbo lako tu litakuwa linakuimbia kwa dharau chubwichubwi!.
Umeshauli vyema ila kuvifuata hivyo kwa hii life style tuliyonayo ni amsha mtu kazini saa moja kamili na lala yake saa tano usiku huko bado hujakuta simu ya mpenzi wako kenzy nimemuandikia "Nakupenda mke wangu mwenye kibebeo nyuma!"😂
Unakuta mtu anahela nyingii halafu unamwambia usinywe bia!,so anywe maji na juisi natural hapo ukute anatukanwa na rafiki zake anajaza nzi..🤣
Mkuu have you ever experienced this message "me & you it's over" hiyo message inaweza kukunywesha k vant nne ugali mbili kitimoto kilo mbili kachumbali saba sigara pakti saba machozi lita tatu huku ukisumbua watu warudie muziki wa kuachwa kuachwa au ule wa bia tamu..😁