Hii ndio Butiama ya Nyerere

Hii ndio Butiama ya Nyerere

Ndugu yangu, Butiama imeharibiwa na wananchi wenyewe. Mimi ni mzaliwa wa Butiama. Kijiji cha Butiama kilishapiga hatua kubwa sana kimaendeleo, pengine kuliko vijiji vingi vya Tanzania-chini ya Mwenyekiti mahiri, Joseph Kizurira Nyerere (Kumurungu Kwata Obhike).

Butiama unayoiona sasa ni magofu kutoka na wizi na ufisadi wa viongozi wajinga. Butiama ilishakuwa na kiwanda cha useremala cha kisasa, kiwanda cha kushona nguo za kila aina, benki za Posta na NBC, Posta na Simu, ilishakuwa na combine Harvester, matrekta zaidi ya 15 au 20, Fiat 110 na 682 na tela; planters, shamba la ng'ombe waliokamuliwa kwa mashine, petrol station, mashine za kusaga na kukoboa, wanafunzi walipewa maziwa mara mbili -tatu kwa wiki, wanafunzi walishonewa sare na kugawiwa mbili hadi tatu kwa kila mmoja, madawati yote yalikuwa mninga, ilikuwa na malori yasiyo na idadi, bulldozer, hospitali yenye hadhi ya wilaya, nyumba ya kulala wageni (mwitongo), jumba la maendeleo, duka la kijiji, maji ya bomba kutoka Mugango hadi nyumbani kwetu Muhunda; na kila kitu kilichostahili kwa maisha ya mwanadamu.

Baada ya Mzeed Joseph kung'atuka, wapuuzi wameuza kila kitu, hadi mataili na vyuma chakavu. Wameng'oa hadi nyaya za umeme katika ofisi za umma. Kwa hali hiyo utamshutumu Mwalimu? Butiama ilikuwa na misitu. Lero miti inakatwa mkaa kana kwamba haina maana wala umuhimu. NI wajibu wa wana Butiama sasa kufaidi matunda ya uhalibifu wao. Mimi nyumbani kwangu ni maji ya kisima kirefu. Wananchi wanateka maji bure. Ni maji safi na salama kabisa. Asiye na maji, anakaribishwa kwangu.
 
Ahsante mkuu kwa maelezo yako mazuri,kweli miafrika ndivyo tulivyo wala haujasingizia chochote.
Lakini kwa kuwa wewe ni mmoja wa wazaliwa wa butiama,ebu watafute wenzako wote waliopo nje ya butiama,muone mtakavyoweza kusaidia hasa kuleta huduma za jamii(maji,afya,elimu)zilizo bora katka kijiji cha butiama.
 
Tutafutane wapi? Huwezi kuamini, jana usiku nimeambiwa kulikuwa na harambee ya kuchangia maendeleo ya Butiama iliyofanyika Serena Hotel, Dar es Salaam. Utashangaa kwamba sisi ambao ndiyo wadau wakuu, tena wanahabari wa kuhamasisha, hatukupewa taarifa! Hapa ninachoona mimi ni kwenda kuungana na masikini wenzangu kuhakikisha wanapata huduma muhimu za kijamii. Haiwezekani watu makini wafanye shughuli muhimu kama hii bila kuwahusisha wengine. Hata kama hatuna fedha, lakini tuna sauti ya uhamasishaji!
 
Mi nilizani kwa kuwa uku ni kwao na mwlm nyerere kungekuwa na kautofauti kidogo,hasa huduma muhimu za kijamii.

Wewe ni mtu wa ajabu sana ndio maana hata kuandika kiswahili fasaha huwezi. Ulitaka mwalimu ajipendelee?
 
Hicho ndo kijiji cha mtu aloamini sera ya Kujitegemea akijisifu kutembea na kitabu cha Azimio la Arusha kila sehem ili akisome lakin akaenda kuomba msaada wa kujengewa Msikiti na Gadafi kijijini kwake.

"I'VE SAID IT ALREADY, I'AM CONVICED THAT THE WAY TO BUILD A NEW AND BETTER WORLD IS NOT CAPITALISM. CAPITALISM LEADS US STRAIGHT TO HELL."
Sio mimi ni moja wapo ya nukuu za hayati braza yetu Hugo Chaves. Aliamini ambacho na wewe huamini kwa utumwa wako wa fikra.
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana ndio maana hata kuandika kiswahili fasaha huwezi. Ulitaka mwalimu ajipendelee?

Watanzania wanafiki sana . Wanapenda kuficha ukweli. Issue sio kujipendelea au kutaka watu walingane au wawe sawa. Ukweli ni kwamba lazima tofauti iwepo au ionekane kati kati kiongozi na raia, tajiri na masikini,msomi na sio msomi, hivi nyumani au kwa rais kutafanana na nyumbani kwa raia. Tumia akili kufikiri
 
Yaaa. ukifiria unatumia akili kufiri kumbe...
 
Tutafutane wapi? Huwezi kuamini, jana usiku nimeambiwa kulikuwa na harambee ya kuchangia maendeleo ya Butiama iliyofanyika Serena Hotel, Dar es Salaam. Utashangaa kwamba sisi ambao ndiyo wadau wakuu, tena wanahabari wa kuhamasisha, hatukupewa taarifa! Hapa ninachoona mimi ni kwenda kuungana na masikini wenzangu kuhakikisha wanapata huduma muhimu za kijamii. Haiwezekani watu makini wafanye shughuli muhimu kama hii bila kuwahusisha wengine. Hata kama hatuna fedha, lakini tuna sauti ya uhamasishaji!

Ndugu yangu hakika wewe ni mtu muhimu sana kwa maendeleo ya Butiama,sauti ya uhamasishaji inatosha kabisa kuleta mabadiliko
Sina hakika kama hizo fedha za harambe zitafika Butiama kwa shughuli za kimaendeleo,yawezekana wajanja wakazitafuna zote.
 
Kwa akili kama zako..sijui Neo-colonialism utaisha lini?"We produce what we don't consume and we consume what we don't produce"..kweli Mr maendeleo hongera zako

The joke is on you jack.The lower end of wit is higher than the higher end of your wits.
 
mkono kwa mkono

ila naona mkono kwa mkono amejitaidi kwa upande wa shule za sekondari,ila kwa idara zingineka Maji,afya bado kuna changamoto nyingi.
 
naelewa sana ila wewe ndo hujaelewa aina ya Uandishi nilioutumia kufikisha ujumbe maalum kwa watu wote wenye uelewa. Piga chabo kwenye Comment ya saba Utaelewa what i meant!

wanataka watafuniwe kila ki2, bila shaka amekurupuka baada ya kuona umemtaja kikwete,
 
wana JF,nimefika Butiama kwa mara ya kwanza kweli sikuamini apa ndio kijiji alichozaliwa na kuzikwa mhasisi wa taifa ili JK Nyerere.
Yaani kupatikana kwa maji ni shida kweli,wananchi wanaangaika usiku na mchana kusaka maji,mbaya zaidi ata upatikanaji wa maji kwenye hospital ni taabu kweli.
Majengo ya shule ya msingi yamechakaa ile mbaya,nazani hayajawai kukarabatiwa tangu shule imejengwa,kwa upande wa hospitali nayo majengo hasa wodi za wagonjwa zimechakaa naambiwa wagonjwa wananyeshewa wakati wa mvua,na ipo siku majengo yatawaangukia.
Hv ulitaka hizo shida za huduma maji, shule, hosp etc uzikute kwenye kijj cha nan? au changu ndo ungeona sawa? au ulifikiri kuna kabajeti kadogo ndani ya bajeti kubwa kametengwa kwa ajili ya butiama2? huko kijjn kwenu mabomba yanatoa maziwa mpaka uickitikie butiama? tz ni moja mgawanyo wa utoaji wa huduma lazima uwe sawa sehem zote na ningeshangaa kama ungeeleza tofaut na ulichokieleza, ishu ya kudiscus ni jinc ya kuboresha huduma vjjn na c butiama!!
 
Nyerere angejijari yeye tu nchi yetu huenda isingekuwa hapa ilipo,kuna baadhi ya wasomi tulio nao wasingepata nafasi ya kusoma,embu ona vijana wanavohangaika kupata mikopo ya vyuo vikuu,mi nadhani alifikiri vizuri kwa wakati ule.
 
Hv ulitaka hizo shida za huduma maji, shule, hosp etc uzikute kwenye kijj cha nan? au changu ndo ungeona sawa? au ulifikiri kuna kabajeti kadogo ndani ya bajeti kubwa kametengwa kwa ajili ya butiama2? huko kijjn kwenu mabomba yanatoa maziwa mpaka uickitikie butiama? tz ni moja mgawanyo wa utoaji wa huduma lazima uwe sawa sehem zote na ningeshangaa kama ungeeleza tofaut na ulichokieleza, ishu ya kudiscus ni jinc ya kuboresha huduma vjjn na c butiama!!

usigombane kijana kuwa mpole,ningependa kuziona huduma za kijamii(maji,shule,afya) kwenye vijiji vyote vya tanzania.
lakini khali ya butiama kwangu imenisikitisha,yaani imezidiwa na vijiji vingi apa tz.
Kamwe mgawanyo wa utoaji huduma hauwezi kuwa sawa vijijini kwa sababu( economic,cultural,geographical and political factors)
kumbuka ata miji mikubwa apa tz inatofautiana,mbona Dar es salaam imeendelea kuliko maeneo mengine?mbona tunaambiwa mkoa wa kilimanjaro umeendelea kulinganisha na mikoa mingine?
Kijana umeongea vizuri kabisa sentensi ya mwisho ya kwamba cha muhimu ni jinsi ya kuboresha huduma vijijini na sio
butiama,upo sahihi kabisa, lakini tunayo haki ya kuhoji sababu ya kila kijiji kushindwa kupata maendeleo.
Kwa Butiama ni lazima tuoji sababu fursa zilikuwepo na bado zipo lakini huduma za kijamii bado zipo nyuma.
 
Kwani si ndio maisha yetu watanzania hayo? Mbona unashangaa Butiama hamna hivyo vitu umejiuliza kijijini kwenu? Kwanini unataka Butiama iwe tofauti na Tanzania nyingine?

Maisha yanapaswa kuwa sawa na nadhani itakuwa ni makosa kama nyumbani kwa viongozi kuwe kama Ulaya alafu sehemu zingine ziwe 'daraja la tatu'. Mgawanyo wa kiuchumi usiwe wa kitabaka kufuata wanapotoka viongozi.

Tatizo la maji ni nchi nzima, huna sababu ya kushangaa kwa nini Butiama hakuna.
Awamu ya tano kanyaga twende
 
Uliyoyaona Butiama ni karibia nchi nzima. ndo maana watu wanahoji kasi ya maendeleo yaliyofikiwa kwa nusu karne ya chama tawala. Tatizo la Maji hata Dar ni kubwa sana.

Kiongozi mzuri ni yule anayepitia changamoto za maisha ya mwananchi wa kawaida, kwani zinamfanya atafute solutions ambazo zitasolve hata tatizo lake kwani naye ni part and pacel ya jamii husika. so was Nyerere.
kweli kabisa
 
Back
Top Bottom