Hii ndio Butiama ya Nyerere

Hii ndio Butiama ya Nyerere

moesy

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
3,555
Reaction score
3,539
wana JF,nimefika Butiama kwa mara ya kwanza kweli sikuamini apa ndio kijiji alichozaliwa na kuzikwa mhasisi wa taifa ili JK Nyerere.
Yaani kupatikana kwa maji ni shida kweli,wananchi wanaangaika usiku na mchana kusaka maji,mbaya zaidi ata upatikanaji wa maji kwenye hospital ni taabu kweli.
Majengo ya shule ya msingi yamechakaa ile mbaya,nazani hayajawai kukarabatiwa tangu shule imejengwa,kwa upande wa hospitali nayo majengo hasa wodi za wagonjwa zimechakaa naambiwa wagonjwa wananyeshewa wakati wa mvua,na ipo siku majengo yatawaangukia.
 
Wakati wa Mwl hali ilikuaje? Jakaya kang'oa mabomba,kachuna rangi, katindua Lami Kahamisha vitanda hospitali?.Umaskini tuliaminishwa ndio sifa ya Uadilifu na haya ndo matokeo!
 
Mkuu, ulitegemea kuona kuna tofauti gani? Hizo ndio hali za wananchi wa kawaida hapa nchini.
 
Mkuu, ulitegemea kuona kuna tofauti gani? Hizo ndio hali za wananchi wa kawaida hapa nchini.
Mi nilizani kwa kuwa uku ni kwao na mwlm nyerere kungekuwa na kautofauti kidogo,hasa huduma muhimu za kijamii.
 
Wakati wa Mwl hali ilikuaje? Jakaya kang'oa mabomba,kachuna rangi, katindua Lami Kahamisha vitanda hospitali?.Umaskini tuliaminishwa ndio sifa ya Uadilifu na haya ndo matokeo!

Una uhakika unachokisema hapo?
 
Wakati wa Mwl hali ilikuaje? Jakaya kang'oa mabomba,kachuna rangi, katindua Lami Kahamisha vitanda hospitali?.Umaskini tuliaminishwa ndio sifa ya Uadilifu na haya ndo matokeo!
Yaani wa kulaumiwa ni Nyerere mwenyewe na wala sio Mkapa, Mwinyi au Kikwete
 
Una uhakika unachokisema hapo?

naelewa sana ila wewe ndo hujaelewa aina ya Uandishi nilioutumia kufikisha ujumbe maalum kwa watu wote wenye uelewa. Piga chabo kwenye Comment ya saba Utaelewa what i meant!
 
Kwani si ndio maisha yetu watanzania hayo? Mbona unashangaa Butiama hamna hivyo vitu umejiuliza kijijini kwenu? Kwanini unataka Butiama iwe tofauti na Tanzania nyingine?

Maisha yanapaswa kuwa sawa na nadhani itakuwa ni makosa kama nyumbani kwa viongozi kuwe kama Ulaya alafu sehemu zingine ziwe 'daraja la tatu'. Mgawanyo wa kiuchumi usiwe wa kitabaka kufuata wanapotoka viongozi.

Tatizo la maji ni nchi nzima, huna sababu ya kushangaa kwa nini Butiama hakuna.
 
Sisi wenyewe mbona tunaona raha tu na tushazoea? tuachieni Butiama yetu!
 
Hicho ndo kijiji cha mtu aloamini sera ya Kujitegemea akijisifu kutembea na kitabu cha Azimio la Arusha kila sehem ili akisome lakin akaenda kuomba msaada wa kujengewa Msikiti na Gadafi kijijini kwake.
 
Nchi nyingine pangetengenezwa pawe eneo la utalii na makumbusho lakini unamsikia kabisa Kikwete anaamini na kutangaza Kwamba Nyerere hakufanya kitu ,chuki yake na visasi vya kumwambia bado hajakua 1995 ameiweka wazi bila kufisha na kutuaminisha yale wasemayo wanaomfahamu akiwemo Mkewe aliyesema LIndi kuwa mumewe ana hasira na ni mkali legacy yake atakapoondoka 2015 ni kuhakikisha amempull down Nyerere na yeye kuwa ndio Baba wa Taifa
 
Mi nilizani kwa kuwa uku ni kwao na mwlm nyerere kungekuwa na kautofauti kidogo,hasa huduma muhimu za kijamii.

Lakini kumbuka kuwa Mwl. hakuwa fisadi. Kwa hiyo hakujilimbikizia huduma zote muhimu kijijini kwake. Na kwa taarifa yako hali uliyoikuta ni afadhali.
 
Kwani si ndio maisha yetu watanzania hayo? Mbona unashangaa Butiama hamna hivyo vitu umejiuliza kijijini kwenu? Kwanini unataka Butiama iwe tofauti na Tanzania nyingine?

Maisha yanapaswa kuwa sawa na nadhani itakuwa ni makosa kama nyumbani kwa viongozi kuwe kama Ulaya alafu sehemu zingine ziwe 'daraja la tatu'. Mgawanyo wa kiuchumi usiwe wa kitabaka kufuata wanapotoka viongozi.

Tatizo la maji ni nchi nzima, huna sababu ya kushangaa kwa nini Butiama hakuna.
upo sahihi mkuu,nilikuwa nafikiri tofauti ya kwamba kijiji cha rais lazima kiwe na maendeleo kwa kiasi fulani kulinganisha na vijiji vingine, kumbe vijiji vyote vipo sawa.
sina uhakika na vijiji vya akina Mkapa, Mwinyi, Museven, Kikwete, Kibaki, Moi, etc vikoje!
 
Hicho ndo kijiji cha mtu aloamini sera ya Kujitegemea akijisifu kutembea na kitabu cha Azimio la Arusha kila sehem ili akisome lakin akaenda kuomba msaada wa kujengewa Msikiti na Gadafi kijijini kwake.
alifanya hivyo kwa nia nzuri na alimwomba Gaddafi akiwa mkulima wa kawaida,labda angekuwa kama Jakaya aliyeuza mapande ya ardhi kwa waarabu,na madini kwa wazungu,gesi wachina,makaa ya mawe kawakabidhi wa afrika ya kusini na Tanzanite kumlikisha mwanawe angeweza kuweka maji kijijini kwao
 
Uliyoyaona Butiama ni karibia nchi nzima. ndo maana watu wanahoji kasi ya maendeleo yaliyofikiwa kwa nusu karne ya chama tawala. Tatizo la Maji hata Dar ni kubwa sana.

Kiongozi mzuri ni yule anayepitia changamoto za maisha ya mwananchi wa kawaida, kwani zinamfanya atafute solutions ambazo zitasolve hata tatizo lake kwani naye ni part and pacel ya jamii husika. so was Nyerere.
 
alifanya hivyo kwa nia nzuri na alimwomba Gaddafi akiwa mkulima wa kawaida,labda angekuwa kama Jakaya aliyeuza mapande ya ardhi kwa waarabu,na madini kwa wazungu,gesi wachina,makaa ya mawe kawakabidhi wa afrika ya kusini na Tanzanite kumlikisha mwanawe angeweza kuweka maji kijijini kwao

sina wasiwasi na Nia yake kuwa ilikuwa nzuri, tatizo ni maana ya kujitegemea alishindwa kui practice kama ilivyohubiriwa!
 
Back
Top Bottom