Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,802
- 71,229
Najaribu kuona Julius Malema anavyoruhusiwa kupambana bungeni tena mbele ya Rais na hoja zinabishaniwa kwa hoja napata raha sana.
Je, hali kama hii ingetokea katika Bunge la TZ au tuseme Bunge la Ndugai ingekuwaje? Uhuru huu wa mawazo ungeruhusiwa nchi yetu ingefika wapi kimaendeleo?
Tunakwama sana mambo mengi na sababu ni kuwa kuna miungu watu ambao hata wakiharibu hawahojiwi hata kusemwa tuu nayo ni hatari kwani DPP na polisi wanaweza kutumiwa kukupa mateso na wengine wakajikunyata.
2020 ndio nafasi pekee ya kubadili mambo na kutoa Uhuru mkubwa kwa Bunge baada ya kuhakikisha Tumehuru ya uchaguzi inaundwa na watu wakatumia haki yao na ikaheshimiwa.