Huu ndio upekee wa Serikali ya Dr Magufuli, huu ndio upekee wa Bunge la Ndugai

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Tunaendelea kupiga kazi kama kawaida na kadiri siku zinavyokwenda tunazidi kuona upekee wa mihimili yetu miwili ya Bunge na serikali. Leo ikiwa ni tarehe 17 Aprili, 2018 upekee wa mihimili unaonekana taswira YAKE HALISI.

Ni kweli kuna baadhi ya mambo yana sura ya kweli ya mageuzi na yanaweza kuashiria mafanikio huko mbele lakini takribani mambo mengi yanahitaji tafakuri na kujiuliza kulikoni.

Leo tuangalie huu upekee wa Serikali hii na Bunge letu.

UPEKEE WA SERIKALI HII.
Serikali hii imejidhihirisha kuwa ya kipekee kwa kutaka watu wote wawaunge mkono kwa yale wanayoyaamini na hawataki kukosolewa kwa lolote. Wanatumia nguvu nyingi kupingana na ukweli hata kama UKO WAZI NA UNAOONEKANA NA KILA MTU.


Kuna upekee wa watu wasiojulikana na serikali haitaki kuhojiwa wajibu wake kuwabaini watu hao na huishia kujitetea kuwa uchunguzi unaendelea bila kuonesha dhamira ya kweli. Huu upekee ni wa ajabu maana hatuoni jitihada za kushirikiana na taasisi zinazolalamika ili kukomesha hao wasiojulikana. Wako wapi watekaji wako wapi wauaji ? hakuna majibu na ukihoji unaitwa mchochezi.

Kuna upekee wa kushughulika na wapinzani na sasa ni bandika kesi na weka ndani. Wameacha ile misingi ya UVUMILIVU WA KISIASA ya vyama vingi, wamekuja na upekee wa kunyamazisha sauti za wapinzani wao na kutaka Serikali tu na maajenti wake ndio wasikike. Eti wanapambana na ile kauli kuwa" JK alikuwa Dhaifu" wanafikiri kinyume cha udhaifu ni nguvu na kuvunja sheria ?


Kuna upekee wa kulinda wavunja sheria wa wazi na kubebana wazi wazi tena kwa kutumika mbeleko ya rais kwa mambo ambayo hayana maslahi yoyote na Taifa ( rejea Makonda vs Ruge) na kuacha mambo makubwa ya kitaifa yakiendelea kuligawa Taifa la wavuja jasho.

Kuna UPEKEE WA VIONGOZI KUTOWAJIBIKA KISIASA na huishia kusafishwa na kutoa maneno ya kejeli badala ya maneno ya kujutia madhaifu yanayoibuka (Utashangaa leo Mh Mwigulu anadunda licha ya uoza uliopo kwenye wizara yake n.k)

Kuna upekee wa kukosa Ajenda yoyote ya kuliunganisha Taifa. Utashangaa pamoja na kuwa JK aliitwa dhaifu, alikuwa na ishu zinawaunganisha watu, akijishusha licha ya mamlaka aliyokuwa nayo na alikuwa ana uvumilivu wa kisiasa. Alijitahidi kutofautisha siasa na Uraisi.

Kuna UPEKEE WA KUTOTOFAITISHA URAIS na UCHAMA. Rais alipaswa kuwa wa wote na Uenyekiti wake wa CCM ni wa wanachama wa CCM pekee. Huu upekee wa kutumia mambo ya kiserikali kuwa ya kichama hautasahaulika. ( yaani shughuli ya kutunuku vyeo vya kijeshi wewe unapokea wapinzani )

UPEKEE WA BUNGE LA NDUGAI.

Huyu baba amekuwa ni alama ya Bunge letu la sasa.


Kuna upekee wa Bunge kuitetea serikali badala ya kuisimamia ipasavyo.

Kuna upekee wa Bunge kutumika kucheza siasa za kulinda serikali na kuzima hoja zenye maslahi ya Taifa kuliko mabunge yote ya awamu zilizopita.

Kuna upekee wa kuingilia uhuru wa wapinzani pale wanapofanya wajibu wao kwa serikali iliyopo madarakani na badala yake kushuhghulika wa wapinzani hao kwa kutumia "MADARAKA YA KITI CHA SUPIKA"



Tunasubiri upekee mpya utakaojitokeza na tunasubiri miujiza mipya kwa Maslahi ya Taifa.


Kishada.
 
Na huu ni upekee pia

tapatalk_1519073600276.jpeg
 
Mkuu umeainisha vzr sana..na kwa kweli kila kitu kinaendeshwa kwa matakwa ya mheshimiwa..na ukipinga unabambikiziwa uchochezi na kukosa uzalendo!kinachofuata unaanza kutafutwa na wasiojulikana au kuitwa uhamiaji kuulizwa uraia wako!
 
"Democracy should be used to counter authoritarian ideas".

-Bila bunge madhubuti la kuikosoa na kuishauri serikali.
-Bila kuruhusu upinzani kutekeleza majukumu yake na kutoa elimu ya uraia pamoja na kujuza yanayojiri juu ya serikali yao.
-Bila media yenye meno na uhuru.

Baada ya miaka 10 tutagundua madudu mengi kulikoni yaliyowahi kutokea nyuma kwa hawamu zote.Imagine CAG ndani ya mwaka wa kwanza wa MKULU huyu amegundua kutoeleweka wapi 1.5 Trn shillings zimekwenda kwani there are no records zinazoonyesha wapi zimetumika[Unaccounted for].Imagine,what next the report of CAG will unravel for the year 2018/2019.
 
Katikati ya jitihada za kupambana na ufisadi na kupiga kazi hafla unaambiwa 1.5 T hazionekani, Lakini media ambazo zilikuwa na uwezo wa kuhoji zimefungiwa na zengine zimepigwa FAINI. sI HAYO TU WABUNGE wa upinzani ambao wangehoji wanatatizwa mara wafanyakazi wao wamestaafu na zaidi ya miezi mitatu eti BUNGE limeshindwa kuwapa watumishi wengine? Halafu kuna MTU ana kuja na MISIFA.
 
Bunge hili la kulinda Maslahi ya CHAMA KWANZA KULIKO TAIFA. Eti leo unaambiwa Bunge ni kama Idara au jumuiya ya CCM iliyoekewa Kanuni zinazolindwa na SUPIKA ?

Masikini Tanzania
 
Dhana ya uzalendo wa bunge ni kusaidia kuisafisha serikali ambayo imeabainika zaidi ya miongo 3 haisafishiki. na wameacha uzalendo kwa taifa. Kwani hata yule bibi wa bunge isingetosha tu kusema Serikali iijibu PAC na LAAC si ingetosha.
 
Mjuwee serikali yoyote hukosea lakini makosa yasiwe ndio mazoea na maisha yote. Nyinyi viongozi pigeni kazi huku mkifuata sheria hapo tutawaelewa lkn kwa mwenendo huu mjuwe tunawadharau kwa niaba ya wengine.
 
Upekee wa Serikali kujibu hoja za CAG kupitia mawaziri tena Bungeni (mipasho)badala ya maafisa masuuli kuijibu PAC.
 
Siku hizi walau tumekosa yale maneno fulani fulani ya mkulu ambayo akiyasema Taifa linanungunika chini chini.
 
Back
Top Bottom