Bunge likiendelea na msimamo huu nchi hii itasonga mbele

don xxx

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,112
1,017
Habari wakuu,

Nimesikia michango ya wabunge wa CCM wakati wakichangia hotuba ya Waziri wa fedha ya mapendekezo ya Mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18 na mwelekeo wa Bajeti.Katika michango ya baadhi ya Wabunge wa CCM haswa Ndg.Hussein Bashe (Mb) na Ndg. Ahmed Salum (Mb) nimetiwa moyo na michango ya wabunge hawa na kuona kuwa sasa Bunge linakwenda kujirejeshea heshima ambayo ilijipotezea.

Ninasema haya kwa kuwa tumezoea kuwaona wabunge wa CCM wakikubali na kubariki kila jambo lililosemwa na Serikali hata kama wanajua suala hili si la kweli ama linakinzana na maslahi mapana ya wapiga kura wao/wananchi.Hali hii ilizoeleka sana hata kufikia kuwaambukiza makada wa chama hicho kikongwe kusini kwa jangwa la shahara wakawa wanshangilia kila jambo la serikali hata kama halipaswi kuungwa mkono.Tumekuwa tukiona hata hapa JF makada wa CCM wamekuwa wakipinga threads zinazokosoa mwenendo wa serikali hususani muelekeo wa kiuchumi wa nchi na kuja na majibu mepesi kama; matajiri wameficha Pesa ,mara wasiofanya kazi ndo wanaolalamika kuhusu uchumi, mara mlizoea vya kunyonga na maneno mengine kama hayo.

Sasa, hali iliyojitokeza Bungeni kwa Siku hizi mbili kwa wabunge wa CCM kuanza kusema ukweli na kuungana na wabunge wa vyama vya upinzani kukosoa au kuirekebisha Serikali kunatia moyo na kuona kuwa Bunge lenye nguvu na lenye kujua wajibu wake linakuja Tanzania.

Lakini pamoja na kufurahishwa na michango ya wabunge hao wa CCM ambao wamechangia kwa uchungu na kupendekeza nini kifanyike ili tusonge mbele kiuchumi huku wakishangiliwa na wabunge wa kambi zote hawakusita kuonesha kuwa hali ya uchumi ni mbaya hadi Bungeni.Hili linanifanya nihisi mambo yafuatayo :-

1.Labda wabunge hawa wa CCM wanasukumwa na ukata uliowagusa wao binafsi pale Bungeni ndio maana wameungana na sisi wanyonge. Kama ni kweli watakuwa wamesukumwa na ukata basi ni maombi yangu kwa hali ya kiuchumi iendelee kuwa mbaya zaidi huko Bungeni ili waungane nasi makabwera katika kuisimamia Serikali kwa maslahi mapana ya nchi na si matumbo yao pekee.

2. Kama watakuwa wanasukumwa na dhamira ya dhati basi Mungu awabariki na kuwapa ujasiri zaidi wa kulitetea Taifa la Tanzania.

Ni rai yangu kwa wabunge wote wajitafakari upya na kujikumbusha wajibu wa Mbunge ni upi.Kazi yao ni kutunga sheria na kuisimamia Serikali, wajue kuwa walikuwa wanatukwaza sana pale walipokuwa wanavaa nafasi ya kuitetea Serikali dhidi ya wananchi.

Mungu awatangulie wabunge wote muanze kuiona kweli na kusema ukweli ili tupate maendeleo tunayoyataka.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Wabunge wa CCM wameamua kufanya kazi zao ipasavyo. Tuliwaachia sana CHADEMA wakitamba. Sasa chadema wamekuwa watazamaji
 
In any community kinachounganisha......wapinzani na wenye nchi.....ni maslahi.

Hakuna mbunge WA ccm mwenye uchungu na taifa hili. Majority ni wezi na mafisadi tuu. Na hakuna mbunge WA ccm mwenye jeuri dhidi ya Magufuli. Wote wapo walipo kwa hisani.
 
Ninavyomfahamu Dk Tulia atawanyoosha na cha mtemakuni watakiona hivi tunavyojadili hapa majalada ya wabunge hawa wawili yamekwisha fika mezani pa "Msini-drive".
 
Bashe ndio anaefanya jambo kwa maslai bila kuangalia rangi ya kijana na ndo anae okoa wabunge wa kijana naona sasa wengine wanaanza kushika bendera ya uchumi very good bashe mzee umefanya research na kuongea ukwel acha wa ndio we fanya unaoona sahihi kwa taifa umejionyesha miaka mingi mpenda maendeleo ya kwel na haki
 
Rais alishasema hao wapinzani kuchukua majimbo ni sababu wabunge wa ccm wenyewe walikuwa wamelala..mwaka huu upinzani wanaenda kupungua
 
In any community kinachounganisha......wapinzani na wenye nchi.....ni maslahi.

Hakuna mbunge WA ccm mwenye uchungu na taifa hili. Majority ni wezi na mafisadi tuu. Na hakuna mbunge WA ccm mwenye jeuri dhidi ya Magufuli. Wote wapo walipo kwa hisani.
Kwa hiyo wakiboreshewa maslahi yao watatuacha njia panda ?
 
Huwajui vyema hao MAGAMBA.

Wait & see!

Utarudi mwenyewe kuwakana.
Kinachoendelea Bungeni kimenifanya nihisi mambo mawili tofauti na kushindwa kujua lipi ni sahihi.Ndio maana kwenye uzi huu nimejiuliza hawa wenzetu wameamua kuungana nasi kusema ukweli au ni kwa kuwa maslahi yao yameguswa ? Sikusema kuwa hawa watu wamebadilika kwa dhamira ya dhati lakini kama wamebadilika tutafika tunako taka kufikia.
 
Huyo Bashe ni tofauti na wenzake wazee wa "Ndiyoo." Subiria wakati wa "miswada" utajionea..!
 
Tuseme mara ngapi jamani kuwa KAMWE Usimwamini mwanasiasa hata kama ni babako mzazi? Hawa utashangaa nao wapo wanapigania maslahi yao; na upepo ukibadilika nao wanabadilika. Si ajabu ni mapandikizi ya Lowassa na wanajua wanachokifanya. Expect nothing from a politician and you will never be disappointed!
 
Mungu ameanza kuwafunulia wabunge wa CCM na wameamua kumwambia 'Mfalme' ukweli kuwa unatembea ukiwa uchi na usiwasikilize hao wapambe wako wanaokufagilia na kukudanganya kuwa umependeza sana na vazi lako lilotukuka......

Well done wabunge kwa kuwa mshaanza kuustukia mfumo wa ONE MAN SHOW wa yule Bwana..........
 
Back
Top Bottom