Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mtwara walihamasishwa wapinge gesi isitoke kuja Dar. Yalikuwa ni maafa, wanasiasa wakahusishwa katika kuwajengea watu fikra za kupinga matumizi ya gesi nje ya mkoa. Povu likawatoka watu, ugomvi ukawa mkubwa, kwa sababu watu waliaminishwa kwamba sio sahihi gesi itoke Mtwara ije kupangiwa matumizi jijini Dar. Wanasiasa wakatafuta umaarufu kupitia suala la gesi ya Mtwara, zikasikika dhana nyingi potofu, zikilenga katika kuwapa kiburi wananchi wa Mtwara, ili wasikubali gesi yao itoke Mtwara.
Jana vyombo vya habari vimetoa taarifa ya kugunduliwa kwa gesi mkoani Pwani, yenye ujazo wa futi trilioni 2.17. Sitegemei kuwasikia watu wa Pwani wakipinga gesi yao kutumika nje ya mkoa wao. Sitegemei kuwasikia wanasiasa wakitafuta kick kupitia hii habari ya ugunduzi wa gesi mkoani Pwani.
Naamini kuwa nchi hii ni tajiri sana, wale wazungu walioweka mipaka ya Tanganyika kule Berlin waliongozwa na Mungu moja kwa moja. Sisi ni matajiri wa rasilimali, yaani pamoja na mbuga zote tulizonazo, bado chini ya ardhi kuna mambo mengi ambayo mema. Tupambane katika kuimarisha utajiri wa vichwani ili tuweze kwenda sambamba na utajiri wa ardhini, ambao Mungu alitukirimia kwa neema zake.