Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,170
RC atangaza kusaka Wazungu wazururaji mitaani
na Neema Kishebuka, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Meja Jenerali (mstaafu) Said Kalembo, amesema ataingia mitaani akishirikiana na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, kuwasaka na kuwakamata raia watatu wa kigeni, wanaorandaranda mkoani hapa, bila shughuli maalum, baada ya Idara ya Uhamiaji mkoani hapa kushindwa kufanya hivyo kwa kile alichodai ‘kupewa kitu kidogo'.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, iliyofanya kikao chake wilayani hapa jana, Meja Jenerali Kalembo alisema analazimika kuchukua hatua hiyo, baada ya kuchoshwa na watumishi wa uhamiaji wanaoonekana kushindwa kutimiza wajibu ipasavyo.
Alisema amekuwa akipokea malalamiko mengi, kuwa idara hiyo imekuwa ikiwaachia raia wa kigeni kuishi bila vibali, huku wengine wakiishi na vibali ambavyo muda wake umekwisha.
Alisema ana taarifa kuwa kuna Wazungu ambao haijulikani ni raia wa nchi wa gani ambao wamekuwa wakizurura katika mitaa ya jiji hilo, kuchukua ovyo wanawake na kuzunguka nao kwa madai kuwa ni wawekezaji.
"Jamani hivi hawa Uhamiaji vipi, kuna siku nitaingia mitaani kuwakamata nitamuomba RPC niwe naye ili tuweze kuwakamata na kuwaweka ndani, Uhamiaji wapo lakini kila mtu anasema Msuya (Danny Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga), anakula rushwa...Sasa ukiona RC anaingia mitaani wakati wanaohusika wapo wanalipwa mshahara na serikali, basi kuna tatizo na haiwezekani, hebu watu wa uhamiaji kama wapo shughulikieni hili ni aibu hizo rushwa zitawatokea puani," alisema Kalembo.
Akizungumzia tuhuma hizo, Msuya ambaye hakuhudhuria kikao hicho alikiri kuwepo kwa Wazungu hao, lakini hata hivyo alikanusha kuhusika na rushwa akidai kwamba kama angekuwa akipokea rushwa, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), ingekuwa imemkamata muda mrefu tangu malalamiko hayo yalipoibuka.
Aliwataja Wazungu hao na kuainisha muda wa kwisha vibali vyao kuwa ni Luitren Zijistra (Uholazi), anayefanya shughuli kiwanda cha maziwa na kibali chake kinamalizika Aprili 24, 2012 na hana matatizo, mwingine aliyemtaja ni Zingaro Giussepe (Italia) ambaye kibali chake kimekwisha na Stephen Peter (Ujerumani) ambaye ana kibali cha Maendeleo ya Miundombinu ya Utalii.
My Take:Hawa wakuu ndiyo askari wa miamvuli wa JK, what a shame!!! Yaani hii inathibitisha hawa wakuu wa mikoa kukosa kazi.