Hii nayo ya RC Kalembo imekaaje?

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
RC atangaza kusaka Wazungu wazururaji mitaani

na Neema Kishebuka, Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Meja Jenerali (mstaafu) Said Kalembo, amesema ataingia mitaani akishirikiana na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, kuwasaka na kuwakamata raia watatu wa kigeni, wanaorandaranda mkoani hapa, bila shughuli maalum, baada ya Idara ya Uhamiaji mkoani hapa kushindwa kufanya hivyo kwa kile alichodai ‘kupewa kitu kidogo'.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, iliyofanya kikao chake wilayani hapa jana, Meja Jenerali Kalembo alisema analazimika kuchukua hatua hiyo, baada ya kuchoshwa na watumishi wa uhamiaji wanaoonekana kushindwa kutimiza wajibu ipasavyo.

Alisema amekuwa akipokea malalamiko mengi, kuwa idara hiyo imekuwa ikiwaachia raia wa kigeni kuishi bila vibali, huku wengine wakiishi na vibali ambavyo muda wake umekwisha.

Alisema ana taarifa kuwa kuna Wazungu ambao haijulikani ni raia wa nchi wa gani ambao wamekuwa wakizurura katika mitaa ya jiji hilo, kuchukua ovyo wanawake na kuzunguka nao kwa madai kuwa ni wawekezaji.

"Jamani hivi hawa Uhamiaji vipi, kuna siku nitaingia mitaani kuwakamata nitamuomba RPC niwe naye ili tuweze kuwakamata na kuwaweka ndani, Uhamiaji wapo lakini kila mtu anasema Msuya (Danny Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga), anakula rushwa...Sasa ukiona RC anaingia mitaani wakati wanaohusika wapo wanalipwa mshahara na serikali, basi kuna tatizo na haiwezekani, hebu watu wa uhamiaji kama wapo shughulikieni hili ni aibu hizo rushwa zitawatokea puani," alisema Kalembo.

Akizungumzia tuhuma hizo, Msuya ambaye hakuhudhuria kikao hicho alikiri kuwepo kwa Wazungu hao, lakini hata hivyo alikanusha kuhusika na rushwa akidai kwamba kama angekuwa akipokea rushwa, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), ingekuwa imemkamata muda mrefu tangu malalamiko hayo yalipoibuka.

Aliwataja Wazungu hao na kuainisha muda wa kwisha vibali vyao kuwa ni Luitren Zijistra (Uholazi), anayefanya shughuli kiwanda cha maziwa na kibali chake kinamalizika Aprili 24, 2012 na hana matatizo, mwingine aliyemtaja ni Zingaro Giussepe (Italia) ambaye kibali chake kimekwisha na Stephen Peter (Ujerumani) ambaye ana kibali cha Maendeleo ya Miundombinu ya Utalii.

My Take:Hawa wakuu ndiyo askari wa miamvuli wa JK, what a shame!!! Yaani hii inathibitisha hawa wakuu wa mikoa kukosa kazi.
 
Halafu eti tunajiuliza kwa nini nchi haiendeleai, wakati aina ya viongozi tulionao ndiyo kama huyu Kalembo!
 
Wazungu hao labda wamegonga 'Ikulu' (kula mahawara zao), maana bongo utendaji unaenda kwa njia ya visasi
 
Wazungu hao labda wamegonga 'Ikulu' (kula mahawara zao), maana bongo utendaji unaenda kwa njia ya visasi

Hahaha ahahaha, very likely mkuu maana, najaribu kufikiria hawa wazungu what is so special in them mpaka uwepo wao nchini, legally or illegally imuhusishe RC.
 
Kalembo unachemka ina maana huyo mkuu wa uhamiaji kikazi ni mkubwa kushinda ww????
Mbona una shikwa na kigugumizi toa agizo ka kiongozi au ndo mnaiga ya boss wenu jk??????
 
Hahaha ahahaha, very likely mkuu maana, najaribu kufikiria hawa wazungu what is so special in them mpaka uwepo wao nchini, legally or illegally imuhusishe RC.

Si ndo mi nashangaa..maana hawa wakuu last time I checked ni kwamba RC ni rais wa mkoa..Je ni kweli upeo wake ndipo ulipokomea kudili na vijizungu vizururaji? ( angalia maana pana ya uzururaji) .tena vitatu tu? .naona kashikwa pabaya huyu si bure.
 
RC atangaza kusaka Wazungu wazururaji mitaani

na Neema Kishebuka, Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Meja Jenerali (mstaafu) Said Kalembo, amesema ataingia mitaani akishirikiana na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, kuwasaka na kuwakamata raia watatu wa kigeni, wanaorandaranda mkoani hapa, bila shughuli maalum, baada ya Idara ya Uhamiaji mkoani hapa kushindwa kufanya hivyo kwa kile alichodai ‘kupewa kitu kidogo’.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, iliyofanya kikao chake wilayani hapa jana, Meja Jenerali Kalembo alisema analazimika kuchukua hatua hiyo, baada ya kuchoshwa na watumishi wa uhamiaji wanaoonekana kushindwa kutimiza wajibu ipasavyo.

Alisema amekuwa akipokea malalamiko mengi, kuwa idara hiyo imekuwa ikiwaachia raia wa kigeni kuishi bila vibali, huku wengine wakiishi na vibali ambavyo muda wake umekwisha.

Alisema ana taarifa kuwa kuna Wazungu ambao haijulikani ni raia wa nchi wa gani ambao wamekuwa wakizurura katika mitaa ya jiji hilo, kuchukua ovyo wanawake na kuzunguka nao kwa madai kuwa ni wawekezaji.

“Jamani hivi hawa Uhamiaji vipi, kuna siku nitaingia mitaani kuwakamata nitamuomba RPC niwe naye ili tuweze kuwakamata na kuwaweka ndani, Uhamiaji wapo lakini kila mtu anasema Msuya (Danny Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Tanga), anakula rushwa...Sasa ukiona RC anaingia mitaani wakati wanaohusika wapo wanalipwa mshahara na serikali, basi kuna tatizo na haiwezekani, hebu watu wa uhamiaji kama wapo shughulikieni hili ni aibu hizo rushwa zitawatokea puani,” alisema Kalembo.

Akizungumzia tuhuma hizo, Msuya ambaye hakuhudhuria kikao hicho alikiri kuwepo kwa Wazungu hao, lakini hata hivyo alikanusha kuhusika na rushwa akidai kwamba kama angekuwa akipokea rushwa, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), ingekuwa imemkamata muda mrefu tangu malalamiko hayo yalipoibuka.

Aliwataja Wazungu hao na kuainisha muda wa kwisha vibali vyao kuwa ni Luitren Zijistra (Uholazi), anayefanya shughuli kiwanda cha maziwa na kibali chake kinamalizika Aprili 24, 2012 na hana matatizo, mwingine aliyemtaja ni Zingaro Giussepe (Italia) ambaye kibali chake kimekwisha na Stephen Peter (Ujerumani) ambaye ana kibali cha Maendeleo ya Miundombinu ya Utalii.

Chanzo: T. Daima
 
Anatauta ubunge ama? Si akawakamte kama kazi yake ndio hiyo? Why telling us in the public rally while he knows them inside out. Upuuzi mtupu.
 
Huyu Rtd Gen bado ni mkuu wa mkoa? Huwa analala kwenye vikao! Mpenda chuchu nadhani ameingiliwa anga zake!
 
Huyu R.C kweli hamnazo ameacha kupambana na vibaka yeye anafanya mambo ya ajabu.

Ole wako uwakamate boss wako nae watamkamata huko anako tembeza bakuri nae si anadhurula
 
Back
Top Bottom