Hii naiona huku tu Tanzania. Maana yake nini?

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Sisi wengine wenye International driving licence tunakutana na changamoto mbalimbali sehemu nyingine.

Mimi nimekuwa nikiendesha gari UK, USA, Dubai, Egypt, SA, Canada, Sweden, Netherland, Denmark, Botswana, Kenya, Switz, Russia, China, Japan, Korea na nchi nyingine nimezisahau. Sijawahi endesha Train na Ndege tu.

But kwa Tanzania napata shida kidogo nadhani kuna sheria zinatofautiana.

Mfano:
Ni kwanini magari yakifika kwenye zebra crossing yanasimama na kuwasha hazard? Hii ni hatari maana kuna siku nilidhani gari limepata shida nika epuka kidogo ndo nakuta kuna mtu anavuka. Nikashangaa. Je, hii ni sheria kuwa gari likisimama zebra crossing liwashe hazard?

Kama mtu anapita kwenye junction ananyoosha pia mi huona wengine wakiwasha hazard. Hii nayo sijawahi ona nchi hizo nyingine. Nimejaribu kumuuliza mdogo wangu yeye anaishi Canada anasema hamna hicho kitu. Nikamuuliza mwingine mdogo wangu anayeishi USA naye kasema hapana huo utaratibu.

Mzee yeye ambaye niliwaambia ana nyumba ya maana kiasi kwamba mlinishangaza kusema Mengi Marehemu ana nyumba nzuri kuja kuangalia ya kawaiiiiidaa. Mzee wangu yeye ana majumba nchi mbalimbali za maana. Naye hajawahi ona jambo hilo la kuwasha washa hazard


Labda sasa niulize kwenu ambao mmekaa sana Tanzania: Je, hiyo ni kisheria au ni mbwembwe tu za madereva wenu?
 
Kama wewe ni Mtanzania na unashangaa pia, sasa sisi tufanye nini? Hata sisi ni Watanzania kama wewe pia, hivyo siyo sawa kutushangaa.
 
Hii kitu hata Mimi nashindwaga elewa. Iliwahi leta ubishi pahala tukamuuliza trafik polisi nae akawa Hana jibu la kueleweka.
 
Bangi zingine bhana, zingine mvute mlale mapema muwahi kuamka na sio kutuletea habari 'silali nakuota wewe'.
 
Back
Top Bottom