Hii muvi mpya ya Chama cha Walimu CWT?

Hii muvi mpya ya Chama cha Walimu CWT?

hhhhj

Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
41
Reaction score
68
Chama cha waalimu tanzania(CWT) ni chama cha waalimu cha muda mrefu sana sasa kwa tanzania......Chaajabu chama hiki kimekuwa chungu na mwiba mkubwa kwa waalimu wake kwa muda sasa.....

Maranyingi CWT wamekuwa wakifanya kazi kwa matukio na kutoa matamko yasiyotekelezeka....Baadhi ya maeneo au baadhi ya walimu husema CWT wametusaidia kwa kiasi fulani ila ukifuatilia utakuja gundua ni wachache sana

MUVI YAO INAITAJWE?
Siku chache nyuma CWT walikuwa na mkutano na vyombo vya habari na kutoa maelezo kadha ikiwemo "Endapo serikali haitolipa madeni na malimbikizo na kuongeza chochote ndani ya mshahara wa mwezi huu(october) basi tarehe 30/10/2016 watatoa tamko(yaani walitoa siku 15)"......

Hilo TAMKO ndiyo siku ya kutengeneza muvi na muvj yenye ninavyowafahamu inaweza ikawa mawili
1~tamko la kuitisha mgomo
2~au wakatulizwa msiwasikie tena

TAMKO LA MGOMO
Hii siyo muvi mpya kwa waalimu hata kama mkisema muibadilishe vipi kwani ilishawahi kutokea....

Katika muvi hii ya MGOMO ipo hivi.....
Wanaoambiwa wagome hawa waamini walio waambia na wanaosema gomeni hawaaminiki kwa walio waambia yaani kila mmoja hamuamini mwenzake....

Mwisho wa muvi hiyo stering anakufa adui anakufa muvi inaisha kiajabu ajabu na hapo ndipo mnunuzi(serikali) huleta jeuri sokoni kwa kusema "anayetaka achukue asiyetaka achukue"

HITIMISHO
CWT endeleeni na biashara zenu za MWALIMU BANK na TEACHER'S DEVELOPMENT COMPANY(TDCL) na kuendeleza vitega uchumi vyenu vya mashamba na majengo ambavyo vipo kila mkoa pia msisahau kukata asilimia mbili zao kila mwezi....kwani kwa sasa walimu wengi waoga ipo siku watazinduka na kudai haki zao...

Kwani asilimia 75 ya walimu hawana imani na nyinyi na hiyo ishirini na tano ni walimu wa shule za msingi kwa kuwa wengi waoga na wazee kwakuwa wanaamini wapokaribuni kustaafu na chama wametokanacho mbali hivyo watakosa mabati
 
Back
Top Bottom