Hii kwangu ni ndoa ya mwaka

Hii kwangu ni ndoa ya mwaka

Na tunawaombea maisha mema afya njema na upendo katika familia yao.
 
mie pia ndio nataka niirejeshe hio model.Nadhani itasaidia sana kuondoa tabia ya kuwa na vidampa nje wanaoharibu utukufu wa ndoa!
 
Mmhhh yahitaji mioyo ka mitatu ya ziada kufikia ujasiri wa hao wanawake!!!
 
Mnajua bado siamini? Nimesoma nimerudia tena nashindwa kuishawishi akili yangu kukubali kwamba huu ni ukweli!!!

Teh teh!! Mimi nilibisha mbele yao aliponitambulisha kuwa hawa ni wake zangu!! Baada ya siku kadhaa ndiyo nikaamini kuwa ni kweli, thus why nikasema kwangu hii ni ndoa ya mwaka....!!
 
haiwezekani hii kwa kweli,hao wanawake ni unique kwa kweli

I wish upate fursa ya kuwaona hawa watu, mie mwenyewe nilistaajabu sana!! Sikuwahi kudhani kama kuna ndoa ya wake wawili kwa rika la vijana ikawa peace namna ile!!
 
Of course mitala sio ugomvi.... haswa kama kuna jamaa pembeni anakusahaulisha yote......
 
mbona kawaida kwa dini ya kiislam ukienda nchi za kiarabu hiyo ni kawaida sana bongo hata waislam wanaleta usista duu ndio maana foleni ya kuolewa inazidi ya magari pale ubungo mataa,ila hapo kidume lazima uwe na nguvu kama unashindia chipsi na hawa makuku matahahira ndoa itakuwa chungu dozi zitakuua
 
Mi pia nilijionea maajabu Unguja, wake wenza wanapatana mpaka nguo wanashona sare.
 
Habari JF?

Katika pitapita za huku na kule kupambana na maisha yetu haya, nilijikuta nimekutana na familia moja ambayo daah!! Walinivutia sana lakini walinifanya nijifunze kitu ambacho nanyi kupitia JF mnaweza kujifunza au kutoa shuhuda kama zipo ndoa zingine za namna hii achilia zile za vijijini.

Jamaa ana wake wawili, mkubwa na mdogo ila hao wake zake wanavyoishi ni zaidi ya mtu na ndugu yake!! Wanapendana to the maximum. Wanaishi nyumba moja waliyoijenga pamoja kwa nguvu ya wote watatu yaani wake wawili na mume, master bed rooms mbili yaan ya mke mkubwa na mdogo na vyumba vingine vya watoto huku wakishea sebule yao nzuri!!

Kilichonishangaza zaidi ni vijana (mume ana 36 na mke mmoja 30 mwingine 28) wasomi wa bachelors wenye watoto watatu mke mkubwa wawili na mdogo mmoja huku jamaa akijitapa kuwa wanakula ujana watoto wametosha!!

Nilimuuliza jamaa mara kadhaa umewapa nini hawa mabinti mpaka kupendana hivi kiasi cha kukaa pamoja sebuleni wakichezea smart phones zao pamoja wakiwa na furaha tele? Jibu lake lilikuwa ni kuwaelewesha na kuwajali wote kwa namna moja!!

Niliwauliza wake wenyewe kama wako poa? (huku wamekaa kwenye love siti yao mume katikati) wakanijibu ni zaidi ya poa na wanafurahia maisha ya pamoja kiasi kwamba mchana kila mmoja anapokuwa kazini wanamisiana sanaaaa!!

Hamgombani? "Tugombanie nini sasa na mume ni wetu sote na zamu ya kulala inajulikana kwa kila mmoja, zaidi tuna amani ya moyo sana kwa maisha haya tunapika pamoja, kustorisha pamoja yaani ni bonge la kampani watu hawajui tu. Si unajua visirani vya wanaume? hata siku jamaa akija na visirani vyake sisi tunafarijiana kwa story kama hivi au mmoja wetu akisafiri basi anajua mume wake yupo kwenye mikono salama ya mke mwingine. Kikubwa ni kuepuka maneno ya watu tuu"

Mabinti wa siku hizi, wasomi wetu na mapenzi ya siku hizi yalivyo!! Ni mwanamke gani atakubali kuolewa mitala?? Tena wanaishi mjini kabisaaa na kila mmoja ana kazi yake

Yote tisa kumi kuishi nyumba moja mnashea miundombinu pamoja kwa wanawake wa kibongo ni ishu!

Salute kwa hii ndoa, wanawake kwa waume wa JF tujifunze kumbe MITALA si ugomvi. Sikujua hilo japo sina maana ya kuleta mabadiliko.....!!!

Hata mie nawezaaa...
 
Kushare uume ni big Noooo!! Mimi mtu nikijua anacheat tu ni kwaheri sitaki mjadala.
Nina kinyaa sana.
 
Back
Top Bottom