Hii kwangu ni ndoa ya mwaka

Hii kwangu ni ndoa ya mwaka

Hii niliikuta kule Hydom...sema jamaa alikuwa na wake wanne...wote ndugu (dada na wadogo zake 3)
 
Nimeweka bundle Ya mwezi leo mchana saa hizo eti imeisha after making a few local phone calls
Hamnipati tena

Duuh pole hawa jamaa mi nimeshawakataa muda tu nilikuwa nawaheshimu sana ukizingatia ni mtandao kongwe Tz
 
Aisee, mmoja tu kasheshe, siku wakimtibua wote atakiona cha moto
 
Kushare uume ni big Noooo!! Mimi mtu nikijua anacheat tu ni kwaheri sitaki mjadala.
Nina kinyaa sana.

Mmmmmmmh we mwanamke mbinafsi mnooo....

Kiukweli yakwako pekeyako haipo sayari hii....

Ukitaka hivyo kuna wenzako watakosa kabisaa...

Usiwe na kinyaa pls
 
wanawake wanafiki sana hapo hakuna upendo wowote ni suala la muda tu huyo jamaa atajutia maamuzi yake
 
hao wanawake hawakupewa roho ya kibinadamu, bali ya wanyama ambao ndo hawana wivu! Yawezekana hao huwa wanafanya threesome!
 
kwetu kijijini baba ana wake wawili,wanapika chngu kimoja,kila mmoja ana nyumba yake
kula wanakula pamoja.
nikienda likizo nawanunulia zawadi wote.
 
Ligogoma,

Dunia ya sasa ni ya ajabu. Miaka kama 9 hivi iliyopita niliwahi kushuhudia hili. Lakini pia niliwahi kuwaona wapangaji wangu wakiwa na hili. Yule "mzee" alikuwa na wake wawili, sasa 'worse' enough ni mtu na dada yake(Tumbo moja).

Hawa walisema waliishi nje kisha walirudi Tanzania(nyumbani), yaani Mume na wake zake(mtu na dada yake) na walikuwa na watoto wao wakubwa walikuwa wakiishi nyumba moja. Hili nimelishuhudia kwa macho yangu kwa miaka miwili waliyopanga.

Ulimwengu wa sasa si wa kawaida. 'Kila kitu kinawezekana'. Dunia ya sasa iliyojaa fantasies, ugumu wa maisha, makubaliano, uigaji wa kila namna ya tukio si ajabu kabisa. Sioni ajabu kwa hiyo "ndoa" uliyoiona tena wakiwa ni vijana. Kama jamaa alivyokwambia "wanaenjoy ujana" hilo ndilo lengo. Sisemi ndivyo ilivyo ila katika makubaliano chochote kinawezekana(mf. hao wadada wanaweza kufichiana siri, kila mtu ana mtu wake huko nje lakini hawamuelezi "mume wao", au ni matamanio ya kimahaba/kimapenzi ambayo kila mmoja wao anatamani n.k).

Cha msingi, ni kujua unataka nini na pengine kama utahitaji watoto wako wafanye hivyo au la!
 
Last edited by a moderator:
mleta mada,,, naweza kuwasiliana na hao wahusika.....nilishasikia,,, nataka kuamini...ninataka kufanya nao live interview,,, labda itaweza shawishi wengine katika kupambana na michepuko....ni muhimu....
 
muh, siyawez mwenzenu, nikijua tu mume kachepuka na fulani, nahisi roho inachomoka, presha inashuka leo mkemwenza!!
 
Ukiwa unahadithia movie uweke na jina lake at least na wanajamii wengine tuione starring wamecheza nani na nani, i mean main characters ni kina nani,,Inaitwaje hiyo movie?
 
kwa wale vijana wa chipsimayai, baga sijuii ....hivi vitu hawataweza..
hiyo nguvu itatoka wapi?
 
Back
Top Bottom