Hii kwangu ni ndoa ya mwaka

Hii kwangu ni ndoa ya mwaka

Mh,kama ni kweli basi hao wanawake hawajaumbiwa moyo nlionao mimi.Hii kitu siwezi sitaweza sitamani hata chembe ya moyo wa ivo, kwa hili niwe tu mbinafsi wangu ni wangu jamani.
 
Hongera zao.....mmoja wapo akikosa ajira kazi itaanzia hapo lakini kama wameridhiana kwa Upendo wa agape ni safi
 
Hii niliikuta kule Hydom...sema jamaa alikuwa na wake wanne...wote ndugu (dada na wadogo zake 3)

Naomba ufafanuzi kidogo kaka, huyo jamaa alioa dada mpaka wadogo zake watatu na akakubaliwa??
 
Naomba ufafanuzi kidogo kaka, huyo jamaa alioa dada mpaka wadogo zake watatu na akakubaliwa??

Kaolewa dada mtu (bila vigelegele)

baba kamtuma mdogo mtu kamwangalie dada yako - akabakia huko huko

akamtuma mdogo wa mdogo mtu - akabakia huko huko

akamtuma mdogo wa mdogo wa mdogo mtu - akabakia huko huko

...and they lived happily ever after!!!

- na hii ni kweli -
 
Habari JF?

Katika pitapita za huku na kule kupambana na maisha yetu haya, nilijikuta nimekutana na familia moja ambayo daah!! Walinivutia sana lakini walinifanya nijifunze kitu ambacho nanyi kupitia JF mnaweza kujifunza au kutoa shuhuda kama zipo ndoa zingine za namna hii achilia zile za vijijini.

Jamaa ana wake wawili, mkubwa na mdogo ila hao wake zake wanavyoishi ni zaidi ya mtu na ndugu yake!! Wanapendana to the maximum. Wanaishi nyumba moja waliyoijenga pamoja kwa nguvu ya wote watatu yaani wake wawili na mume, master bed rooms mbili yaan ya mke mkubwa na mdogo na vyumba vingine vya watoto huku wakishea sebule yao nzuri!!

Kilichonishangaza zaidi ni vijana (mume ana 36 na mke mmoja 30 mwingine 28) wasomi wa bachelors wenye watoto watatu mke mkubwa wawili na mdogo mmoja huku jamaa akijitapa kuwa wanakula ujana watoto wametosha!!

Nilimuuliza jamaa mara kadhaa umewapa nini hawa mabinti mpaka kupendana hivi kiasi cha kukaa pamoja sebuleni wakichezea smart phones zao pamoja wakiwa na furaha tele? Jibu lake lilikuwa ni kuwaelewesha na kuwajali wote kwa namna moja!!

Niliwauliza wake wenyewe kama wako poa? (huku wamekaa kwenye love siti yao mume katikati) wakanijibu ni zaidi ya poa na wanafurahia maisha ya pamoja kiasi kwamba mchana kila mmoja anapokuwa kazini wanamisiana sanaaaa!!

Hamgombani? "Tugombanie nini sasa na mume ni wetu sote na zamu ya kulala inajulikana kwa kila mmoja, zaidi tuna amani ya moyo sana kwa maisha haya tunapika pamoja, kustorisha pamoja yaani ni bonge la kampani watu hawajui tu. Si unajua visirani vya wanaume? hata siku jamaa akija na visirani vyake sisi tunafarijiana kwa story kama hivi au mmoja wetu akisafiri basi anajua mume wake yupo kwenye mikono salama ya mke mwingine. Kikubwa ni kuepuka maneno ya watu tuu"

Mabinti wa siku hizi, wasomi wetu na mapenzi ya siku hizi yalivyo!! Ni mwanamke gani atakubali kuolewa mitala?? Tena wanaishi mjini kabisaaa na kila mmoja ana kazi yake

Yote tisa kumi kuishi nyumba moja mnashea miundombinu pamoja kwa wanawake wa kibongo ni ishu!

Salute kwa hii ndoa, wanawake kwa waume wa JF tujifunze kumbe MITALA si ugomvi. Sikujua hilo japo sina maana ya kuleta mabadiliko.....!!!

kuna kitu amekuficha kaka huku kwetu mambo hayo wala si ya kuuliza ni kawaida kabisa sayansi ya mwafrika imetumika hapo kiongozi, watu wamepumbazwa akili hawajitambui
 
kuna kitu amekuficha kaka huku kwetu mambo hayo wala si ya kuuliza ni kawaida kabisa sayansi ya mwafrika imetumika hapo kiongozi, watu wamepumbazwa akili hawajitambui

Aisee.....!! Basi sawa
 
Back
Top Bottom