Hii kampuni ya mabati ya Alaf wanajielewa?

Hii kampuni ya mabati ya Alaf wanajielewa?

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Posts
13,976
Reaction score
22,418
Habari wandugu,
Hivi karibuni nimekuwa nikitaka kuwasiliana na hii kampuni ya altaf inayotengeneza haya mabati tunayoyaita "Msauz", kwa kweli wamenichusha na hawajielewi hata kidogo.

Hawa mameneja wa hii kampuni nina mashaka na utendaji kazi wao, hivi katika dunia ya leo inakuwaje wafanya biashara wanakuwa hivi?

Niliwaandikia email kupitia kwenye website yao. Email address yao ni sales.alaf@safalgroup.com

Nimewapigia simu tangu jana around 04:55 pm hazikupokelewa hata land lines zao na nikapiga na namba ya voda pia ipo kwenye website yao haikupokelewa nkahisi labda muda wa kazi umekwisha, nimewapigia sasa hivi simu hazipokelewi hawa jamaa maku.... nini?

Namba zao za simu nilizopiga ni 022-2860010, 022-2860011, 022-2860012, 022-2860013, 022-2860014 na ya voda ni 0768- 555560

Acheni ujinga ALAF
 
Naona umemaliza kwa kuwa tusi Teh Teh

Ova
 
*KWAKO MTEJA*
Sasa mkuu pengine hawataki kuwasiliana na wewe. Si ubadilishe bidhaa tu as long as ulikua haujaanza kuwasiliana nao toka mwanzo na haujachukua mzigo wowote kutoka kwao.
..
*KWA KAMPUNI*
Hapa ndipo mzungu anapotushinda. Poor restlessness customer care. Wangejua lawama kutoka kwa mteja ni jinsi gani zinairudisha nyuma kampuni na kutengeneza image mbovu.

Pole mkuu.!!
 
shughuli za uuzwaji mabati ya Alaf hufanywa na ma-Agents zaidi kuliko Alafu wenyewe na huo ndiyo mfumo wao hivyo tafuta agent yoyote aliye karibu yako
 
Hawana njaa kwa mteja ambae anatakiwa kuwacliana na AGENTS WAO.
 
Alaf hawana njaa wako vizuri. ili upate huduma zao nenda Tazara na vipimo vyako vya idadi ya bati utapewa invoice ukalipie bank then leta slip upangiwe siku ya kuja kuchukua mzigo wako.
Walishanipigia na tumefanya biashara vizuri tu. huu uzi ulisaidia mkuu
 
shughuli za uuzwaji mabati ya Alaf hufanywa na ma-Agents zaidi kuliko Alafu wenyewe na huo ndiyo mfumo wao hivyo tafuta agent yoyote aliye karibu yako

Bora avumilie tu aende kiwandani kwao direct. Agent wanakula dili na wachina utaenda pigwa kanyaboya utakuja jutia baada ya miaka miwili
 
Wana wateja wao wakubwa wakubwa. Hawawezi hangaika na 'kinyangalikoko' anayetaka mabati mawili...
 
Alaf hawana njaa wako vizuri. ili upate huduma zao nenda Tazara na vipimo vyako vya idadi ya bati utapewa invoice ukalipie bank then leta slip upangiwe siku ya kuja kuchukua mzigo wako.
Kwa hiyo jamaa wamesharidhika na wateja walionao
 
Naona umemaliza kwa kuwa tusi Teh Teh

Ova
Wanastahili, kwa zama hizi za ushindani unafanyaje biashara utadhani unagawa misaada so inabidi watu wakuombe? Kuna kampuni moja ya vifaa vya ujenzi ipo maeneo ya Mwananchi kabla sijawafahamu nilipata taatifa zao nikapiga simu kikapokea kidada kina nyodo na kauli chafu hicho. Sasa sijui kilifikiri mshahara kinaopata unatoka kwa Boss aliyemuhonga papuchi akampa kazi na si wateja wanaonunua bidhaa! Waajiri wawe makini sana na waajiriwa wao, sisi watu weusi hatuna utamaduni wa kuthamini KAZI na kufanya kazi bila supervision ya hali ya juu sana.
 
Back
Top Bottom