Kama unajiuliza kampuni za betting wanapata wapi namba zako, hizi ndio baadhi ya njia wanazozitumia

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
1,149
3,088
Najua sitakuwa mwenyewe kwenye hili, nina uhakika kwenye simu yako lazima utakuwa umeshawahi kutumiwa message na kampuni za betting, kampuni ambazo hata hujawahi kutumia huduma zao na baadhi ya kampuni unakuta ni mpya.

Soma pia:

Binafsi nimekuwa nikipokea message nyingi kutoka kampuni tofauti tofauti ilhali sijawahi kubet tangu nizaliwe. Kiukweli messages hizi zinakera na kukwaza na inanipa maswali mengi je hizi kampuni za betting zinapata wapi taarifa zetu?

Sasa juzi nilikuwa nazungumza na rafiki yangu mmoja ambaye anajishughulisha na masuala ya betting na akanipa mbinu tofauti tofauti zinazotumika kupata taarifa za wateja ikiwemo emails na namba za simu.

Hizi ni baadhi ya hizo njia:

1. Kuuziana Data

Jamaa akawa ananiambia kwamba moja ya njia inayotumika ni kuuziana data. Kwamba hawa maCEOs wa betting wanajuana na hubadilishana taarifa za wateja.

Hali huwa mbaya zaidi pale kampuni moja inapokufa.

Kwa mfano juzi hapa kuna kampuni ya Winning Princess ilifungwa na kuacha kufanya kazi Tanzania, jamaa akawa ananiambia kuwa kama wewe ulikuwa ni mteja wa kampuni hiyo, kuna uwezekano mkubwa data zako kama namba ya simu na emails ziliuzwa kwa kampuni nyingine ya betting.

CEOs data.png

2. Kubadilisha Namba

Pia kuna wale watu ambao wamesajili namba ambazo zilishawahi kutumika na mtu mwengine zamani. Kwa hiyo, kama mtu ambaye alikuwa anatumia namba yako ya sasa hivi, alikuwa anabeti na namba ambayo unatumia ilikuwa kwenye mfumo basi utatumiwa sana message kwani database yao bado ina hiyo namba.

Messages.png


3. Kuuzwa kwa kampuni

Kama kampuni ikiuzwa pia mara nyingi na data zako zinaenda. Kwa mfano, kama ulikuwa unabeti kampuni X na hiyo kampuni ikauzwa na ikabdilisha jina kwenda Y maana yake ni kwamba taarifa zako kama emails, namba yako ya simu na michezo unayopendelea kucheza pia zitaenda kwa mmiliki mpya.

Compani.png


4. Kubonyeza links za mitandaoni

Kuna muda unakuta kama unaperuzi kwenye website mbalimbali na kuna kama tangazo linakuja na kukushawishi ubonyeze hiyo link. Kwa asilimia kubwa kama utabonyeza link za aina hiyo taarifa zako za muhimu kama email pia zinaweza kuchukuliwa na kutumika kukutumia message.

Nadhani kuna umuhimu wa serikali kuingilia kati suala zima la taarifa binafsi. Mambo ya kwamba taarifa zetu sisi wananchi wa kawaida zinauzwa na kukusanywa bila ridhaa yetu sisi wananchi, sio poa na ni linahatarisha privacy zetu


5. Mitandao ya simu kuuza taarifa zako

Suala la kampuni za simu kuuza taarifa zetu ni suala ambalo liko wazi na ndio maana wakati zoezi la uandikishwaji linaendelea, TAMISEMI walikuwa wanatutumia messages. TAMISEMI namba zetu za simu wanazipata wapi?

Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa hizi kampuni za simu zinazipa hizi kampuni za betting namba zetu ili zitutumie messages.
 
Back
Top Bottom