HII Itawezekana BONGO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HII Itawezekana BONGO

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Magulumangu, Sep 28, 2010.

 1. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemani Kova
  Polisi kwa kushirikiana na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam, wameanzisha mchakato wenye lengo la kuyafanya maduka yaliyopo Kariakoo yafanye kazi hadi saa sita usiku.
  Kwa mujibu wa utaratibu uliopo sasa, maduka hayo yanafungwa ifikapo saa 12:00 jioni.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemani Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa, jeshi hilo linawasiliana na wafanya biashara wa eneo hilo, ili kuanza majadiliano.
  Alisema hatua ya maduka hayo kufunguliwa hadi saa sita usiku itasaidia kuongeza kipato cha wafanyabiashara, kukuza uchumi na kupunguza msongamano wa watu.
  Kwa mujibu wa Kova, masuala ya msingi yatakayopewa kipaumbe katika mchakato huo ni yanayohusu ulinzi na usalama.
  Kova alisema majadiliano hayo yamelenga kuimarisha ulinzi wa kutosha katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu ya kuweka taa kubwa na kufunga kamera za kuwabaini wahalifu.
  Pia alisema mchakato huo utajumuisha kuanzishwa njia za simu ambazo zitatumika kwa haraka katika kutoa taarifa za uhalifu.
  "Hatua hii itawasaidia hata watu wanaotoka kazini jioni, kwenda madukani kununua bidhaa pasipo uharaka wala msongamano,” alisema.
  Alisema jambo la muhimu kwa wafanyabiashara hao ni kuzingatia masharti yanayohusu ulinzi.
  Wakati huo huo jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu 11 wanaosadikiwa kuwa majambazi sugu, wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali jijini hapa.
  Miongoni mwa makosa hayo ni ujambazi wa kutumia silaha, wizi wa televisheni, pikipiki za miguu mitatu bhangi na gongo.
  Kova alisema kuwa bado wanaendelea na operesheni ya kuwasaka majambazi sugu kwa lengo la kuondoa uhalifu jijini humo...

  UCHUKUO WANGU..

  Ujambazi unakua kwa kasi ya ajabu tz hata mchana je wakianzisha hii maduka mpaka usiku kutakalika kweli Kariakoo jamani?KOVA ATAWEZA KWA HILI
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ndiyo ina wezekana. Kukiwa na watu watakao jitokeza huo usiku na usalama toka kwa jeshi la polisi hata uhalifu utakua adimu. Na kama huo muongezeko wa muda una maanisha kipato zaidi kwa hayo maduka, basi wamiliki wa maduka kadhaa zinazo fuatana au wa mtaa mmoja wana weza kukusanya nguvu kugharamia ulinzi wa ziada toka kwa private security firms. Ni kitu kina wezekana ni planning tu na implementation. Tatizo Tanzania tuna sema hatufanyi.
   
 3. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hiyo kufanya shopping mchana tuu unaenda roho juu ndo iwe ucku!!?? hapo hawanipati kabisa.
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Polisi wanashughulika na usalama wa wenye maduka. Sawa. Lakini jee usalama wa watakaonunua vitu usiku nao unashughulikiwa vipi?
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kila kitu kinawezekana lakini suala la msingi la kuangalia ni usalama MUUZAJI na MNUNUAJI
   
 6. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nairobi insifika kwa kuwa na wimbi kubwa la ujambazi....lakini Nairobi hailali...biashara 24/7!!
  wasiwasi wangu... wazo jema ila limlenga kuwanufaisha wafanya biasha... sie ma-kapuku tunaonuna bidhaa na kurudi kwetu si ndo tunaviziwa vuri na vibaka!!?! Tunahakikishiwaje usalama?1:confused2:
   
 7. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hapa wana mpango wa kuharibu gesti za watu wanaolala kariakoo kwa kukosa sehemu za kulala na huamua kulala pembezoni mwa majengo kwa kutandika maboksi.
  Kuhusu ulinzi inawezekana ni namna ya kujipanga tu
   
 8. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nadhani, ni kumwaga polisi. kama wa mzimbazi station hawatoshi, azima ilala au magomeni. Wanaweza hata kuazima polisi wa msasani na zile sehem zilizotulia. Hii ifanywe ilhali wanafundisha polisi wengine. Kama hela za kulipa mishahara hazitoshi basi waongeze kataksi kadogo sana kwenye sales, ili kuchangia mishahara ya polisi. Wazo la kufungua biashara mpaka usiku, sio baya.
   
 9. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wazo zuri and lenye FAIDA zaidi kwa Nnchi, Wafanya Biashara na Wezi,
  LItaongeza matumizi zaidi kwa Mtanzania (though haulazimishi kununua), Kwa namna moja au nyingine Itaboresha Kutokomeza Giza Dar es Salaa, Wazo, muda wa kazi uongezwe pia kumnufaisha Mfanyakazi,
   
 10. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ulinzi ni muhimu.. na kila kitu kinawezekana.
   
Loading...